Menu
in ,

Mo Farah matatani

Tanzania Sports

Mo Farah

Mwanariadha maarufu wa Uingereza, Mo Farah amejikuta katika matatizo.

Mwanariadha huyi anadaiwa kwenda kinyume na kanuni za mchezo kwa kutumia viongeza nguvu kabla ya mbio.

Taarifa zilizovuja zinaonesha kwamba Farah mwenye medali kadhaa za dhahabu alitumia dawa za kusisimua misuli.

Katika kuonesha lilikuwa tatizo la kweli, Farah anaelezwa kubadili akaunti yake ili wachunguzi wasipate mawasiliano yake.

Hata hivyo kwa mara kadhaa Farah amekuwa akikanusha kutumia sindano aina ya
L-carnitine.
Wanasheria wa Farah wamekuwa wakitetea vitendo vya mwanariadha huyo wakisema kwamba mteja wao si roboti na kwamba mahojiano si kipimo cha kumbukumbu.

Uadilifu wa Farah unazidi kuhojiwa hasa juu ya sababu za kuwakwepa wapelelezi wa Marekani waliokuwa wakifuatilia iwapo alitumia kiongeza nguvu husika.
Anadaiwa kutumia mchanganyiko tata wa virutubisho visivyoruhusiwa kwa njia ya sindano na muda mfupi baada ya hapo akabadili akaunti yake akiacha maswali mengi.

Kuna nyaraka zilizopatikana zikionesha mjadala miongoni mwa maofisa waandamizi wa Shirikisho la Riadha Uingereza, ikiwa ilikuwa sahihi kwa Farah kudungwa sindano nne za L-carnitine siku mbili kabla ya michuano ya marathon ya London 2014.
Kadhalika walijadiliana ikiwa kufanya hivyo kulilenga kuuenzi mchezo huo na kwa mujibu wa kanuni na maadili yake.
Watu wanne wazito – Mkuu wa Utabibu wa Shirikisho la Riadha Uingereza, Dk Rob Chakraverty, mkuu wa uhimilivu katika riadha, Barry Fudge, mkurugenzi wa zamani wa utendaji katika shirikisho, Neil Black, na kocha wa zamani wa Farah, Alberto Salazar – wanaelezwa walikuwapo wakati anapewa mseto huo wa kuongeza nguvu.

Inaelezwa kwamba walikubaliana kumpa amino acids ili kumwongezea ufanisi kwenye jaribio lake la kwanza kukimbia umbali wa maili 26.2.
Hata hivyo, inaelezwa kwamba Farah alipopimwa kwa ajili ya madawa siku sita baadaye hakurekodi L-carnitine kwenye fomu zake tofauti na ilivyotakiwa.
Inabainushwa zaidi kwamba, mwaka mmoja baadaye, alipohojuwa na maofisa wa Usada jijini London kwa karibu saa tano awali alikana kutumia virutubisho hivyo.

Aliulizwa iwapo mtu atasema alitumia (Farah) sindano za L-carnitine atakuwa hasemi ukweli, naye akajibu ndio arakuwa hasemi ukweli kwa sababu kwa asilimia 100% hakutumia kabisa.

Akakana kuwa kocha wake alipendekeza atumie sindano hizo.
Hata hivyio baadaye Farah alikutana na Fudge aliyehojiwa pia na Usada alisema alipeleka L-carnitine kutoka Uswisi kwa mkataba na Salazar.

Ndipo Farah akarudi chumba cha mahojiano wakati wahusika wakijiandaa kuondoka na kutoa maelezo tofauti juu ya matumizi yake ya L-carnitine.
“Kwa hiyo nilitaka niweke mambo sawa. Samahanini, niliitumia wakati ule lakini nikawa nadhani sikutumia,” Farah ananukuliwa akisema.

“Siku chache kabla ya mbio – na Alberto alikuwapo na daktari wako Barry Fudge – na sasa unatuambia hapa wote kwamba hukukumbuka wakati nikikusisitiza kukuuliza juu ya hili?” akasema kwa hasira ofisa mmoja wa Usada.
Farah anajibu: “Ndio kwanza nakumbuka lakini wakati ule sikukumbuka.”

Baadaye alipohojiwa na watu wa magazeti Farah akasema alisahau juu ya sindano na hata jina la dawa husika hadi alipokumbushwa na Fudge.

Mwaka 2017 kamati teule ya bunge iliambiwa kwamba Farah alipewa jumla ya milimita 13.5 za L-carnitine.
Wakati Farah akikataa kuhojiwa zaidi na waandishi, wanasheria wake wanadai hajatenda kosa lakini inaelezwa kwamba jitihada zinafanywa kusafisha jambo hilo.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version