Menu
in , , ,

Mlungula maofisa FIFA

Tanzania Sports

Qatar

Maofisa wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) walipokea kiasi kikubwa cha rushwa kwa ajili ya kupiga kura kwa Urusi na Qatar kuwa wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia, imebainika.

Wapelelezi wa Marekani wanaochimba undani wa uozo huo uliosababisha kuondolewa madarakani kwa Rais Sepp Blatter, wanaonesha kwamba wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya FIFA walifanya kazi hiyo baada ya kuwa wamepewa mamilioni ya dola kupitia kampuni mbalimbali.

Mjumbe mmojawapo, Jack Warner, anadaiwa kupokea kiasi cha dola milioni tano na kuahidi, kisha kutekeleza kuunga mkono Urusi wawe wenyeji wa fainali hizo 2018. Wengine – Nicolas Leoz na Ricardo Teixeira wanadaiwa kupokea kitita kikubwa ili kuhakikisha wanaunga mkono Qatar kuwa wenyeji 2022.

Wapelelezi na waendesha mashitaka wametoa maelezo mapya na ya kina nchini Marekani juu ya wajumbe hao wa zamani wa FIFA – baadhi wakiwa ndani bado kujihusisha na uozo ili kupindisha haki.

Tayari baadhi ya watendaji wa zamani wa kampuni ya 21st Century Fox nao wameunganishwa kwenye mashitaka, wakidaiwa kuidhinisha malipo batili na pia kupata haki za matangazo ya televisheni kwa michuano ya fainali za 2018 na 2022.

Jumatatu ya jana mashitaka yalifikishwa tena katika Mahakama Kuu ya Marekani – Kanda ya Brooklyn, yakieleza kwamba Nicolas Leoz, aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (CONMEBOL) na aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Brazil, Ricardo Teixeira, walipokea hongo kwa ajili ya kuwapigia Qatar kura kwenye mkutano uliofanyika 2010.

Warner wa Trinidad & Tobago aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Amerika Kaskazini, Kati na Caribbean (CONCACAF) anadaiwa kupokea fedha kwa ajili ya kuwavusha Urusi wawe wenyeji na kwamba alizipokea kutoka kampuni 10 tofauti za Mafuta, ikiwa ni pamoja na za Anguilla, Cyprus na British Virgin Islands.

Rais wa Shirikisho la Soka la Guatemala, Rafael Salguero, naye yumo kwenye sakata hiloakidaiwa kukatiwa $1m ili aipigie kura Urusi. Leoz aliyefariki dunia Julai mwaka jana amekwepa kitanzi hicho.

Alejandro Burzaco, Mkuu wa Masoko wa zamani wa Torneos y Competencias, alitoa Ushahidi mwaka 2017 kwamba jamaa hao wote watatu wa Amerika Kusini walipokea hongo za dola milioni moja moja ili kuunga mkono Qatar

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version