MANCHESTER CITY ni mabingwa wa EPL msimu huu. Pongezi nyingi kwao. Lakini
macho,akili na hisia zangu zimeona kitu kingine kutoka kwa wapinzani wao, Arsenal. Ni ukweli
usipoingika kuwa Arsenal walikuwa na kila sababu ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu England
msimu huu, lakini ajali ya mechi kadhaa kupata matokeo mabaya yaliwanyima ubingwa wa Ligi
Kuu.
Kwangu mimi Arsenal ni mabingwa ambao wanatakiwa kutembea kifua mbele. Timu hii ilianza
Ligi ikiwa haipewi nafasi ya kuingia hata nne bora. Wasiwasi dhidi ya Arsenal ulikuwa mkubwa
kwa watu, huku wapinzani wake wakiipuuza kwa kuamini hawawezi kupata hata nafasi ya
kuwakilisha Europa Lague au Conference League. Arsenal ni timu ambayo imeonekana kama
vile iliyumba tangu kuondoka kwa gwiji wake Arsene Wenger.
Pengine Arsene Wenger yungali katika viunga vya Arsenal. Ni timu ambayo inaoongozwa na
wachezaji wa zamani wa Arsene Wenger ndio waliokuwa na imani kuwa Arsenal inaweza
kuleta kitu cha kipeke EPL. Msimu unamalizika, Arsenal hii ikiwa chini ya kocha wake Mikel
Arteta, na Mkurugenzi wa Michezo,
Edu Gaspar wameleta kitu kizuri kwa Arsenal ambacho kitawafanya washabiki wake wafurahie
licha ya kuukosa ubingwa dakika za lala salama. Arteta ni raia wa Hispania, ameleta ufundi na
utamaduni wa Kihispaniola.
Edu Gaspar ni raia wa Brazil, ambaye ametoka taifa kubwa na lenye sifa nyingi katika
ulimwengu wa soka. Brazil ndio mabingwa wa dunia wenye mataji matano kuliko nchi nyingine
yoyote. Edu Gaspar ameleta utamaduni wa Kibrazil na amejifunza ule wa Kishipania ambako
aliichezea klabu ya Valencia.
Wawili hawa ndio wanatakiwa kupendwa, kuengwa engwa na mashabiki wa Arsenal ambao
walifanywa waamini kuwa timu yao ilikuwa kwenye mbio za ubingwa. Wakati wanawasajili
Alexandre Zinchenko, Tossard,Gabreil Jesus, na vijana wengine hakuna aliyedhania kuwa
Arsenal ingekuja kutikisa vigogo EPL.
Chini ya Arteta na Edu maelfu ya wanamichezo duniani wameona kitu walichokileta viongozi
hao wawili na wasaidizi wao. Licha ya wastani wa umri wa wachezaji wao kuwa chini ya miaka
25, Arsenal hii imepiga hatua kubwa na kurejesha tabasamu kwa mashabiki.
Ubingwa wa Arsenal umekuja katika kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Katika
kipindi cha Arsene Wenger, ilijulikana kuwa Arsenal haikuwa na shida katika kupigania nafasi
nne za kuwakilisha mashindano ya Ulaya. Ilikuwa hata vita iweje, lakini Wenger angeshinda
kiulaini.
Hata hivyo Arsenal ilipotea kwa muda kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa, jitihada zao
ziliishia kwenye Europa League. Hapo ndipo utaona Edu na Arteta watakuwa wenye wingi wa
furaha kuirudisha timu kwenye mashindano ambayo wao wakiwa wachezaji walikuwa
wamezoea na kuyacheza mara nyingi.
Arsenal ilikuwa mali ya Ligi ya Mabingwa, na Edu na Arteta wameipa kile inachostahili.
Naamini kati ya vipaumbele vikubwa vilivyokuwa mezani mwa Arteta na Edu, kikubwa
kilikuwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya. Wawili hawa wamefanya kazi kubwa ambayo
imevuka matarajio yao kwani Arsenal ilikuwa mshindani mkali wa taji la EPL dhidi ya
Manchester City.
Nina uhakika huenda Pep Guardiola na timu yao ya uongozi hawatakuwa tayari kuwauzia
mchezaji mwingine Arsenal. Msimu huu waliuza Zinchenko na Gabriel Jesus kwenda Arsenal,
ambao walikuwa chachu ya kuimarisha kikosi cha Arteta na Edu.
Hii ina maana Edu alileta kipaji cha Kibrazil (utamaduni wa kwao) na akaongeza ufundi wa
Zinchenko toka Ukraine. Bila kujali mifumo iliyotumika katika mbio za EPL, Arsenal
wanapaswa kufurahia matokeo waliyopata; wamekosa ubingwa lakini wamefuzu Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Kama kuna jambo ambalo Edu na Arteta wanapaswa kulifanya kwa sasa ni kuimarisha kikosi
chao katika maeneo haya; beki wa kati mmoja, kiungo mkabaji mmoja,mshambuliaji mmoja na
beki wa kushoto mmoja.
Lengo ni kuimarisha ubora wa idara hizo pamoja na kuipa machaguo ya kutosha inapoelekea
kwenye Ligi ya Mabingwa. Safu ya ushambuliaji inahitaji mshambuliaji mwingine ambaye
atakuwa mpango wa pili wa Gabreil Jesus, hii ina maana Eddie Nketiah bado anatakiwa
kuimarika na kwenye mashindano ya Ulaya muda huo haupo.
Ni wazi Arsenal lazima iingie sokoni katika eneo la ushambuliaji mwenye uwezo wa kufunga
mabao zaidi ya 20 kwa msimu. Vilevile eneo la beki wa kushoto Zinchenko anaonekana pia
kufaa kucheza kiungo au winga wa kushoto, kwahiyo katika mfumo wa kuimarisha ulinzi
anahitajika beki wa kushoto kumpa nafasi kocha kuwa na machaguo mazuri.
Eneo la kiungo mkabaji, Jorginho na Thomas Partey wanahitaji mshindani mwingine licha ya
umri wao kupaa zaidi. Ni eneo ambalo limewafanya Arsenal kupoteana pale wanaodhibitiwa
kwenye kiungo mkabaji.
Idara nyingine ni beki wa kati, ni eneo ambalo Edu na Mikel Arteta wanapaswa kufanyia kazi
kama njia ya kuboresha kikosi chao. Ifahamike Ligi ya Mabingwa hukutanisha timu zenye
viwango bora zaidi kuanzia mchezaji mmoja mmoja hadi makocha. Ni muhimu Arsenal kuwa
tayari katika ushindani huu. Vilevile, mashabiki waelewe ikiwa hawakutegemea kuona ushindani
wa timu yao kwenye EPL, ni kwa kiasi gani wanaweza kupunguza imani kwa Arsenal kufanya
vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa?
Ni lazima wawe tayari kuinga mkono timu hii na viongozi wawo hawa hawa. Washabiki
hawapaswi kuondoka uwanjani pale juhudi za wachezaji wao zinapokwama. Washabiki
wapambane kwa kuiunga mkono timu hadi dakika za mwisho.