LIGI kuu Tanzania Bara imekuwa na mvuto wake kila mara. Wakati wa msimu mechi zinasisimua mashabiki. Ingawa msimu huu umemalizika kwa mashabiki kutazama mechi wakiwa nyumbani kutokana na mlipuko wa homa ya Corona bado Ligi Kuu ilikuwa na mvuto wa aina yake.
Mijadala ya kusisimua mitandaoni imeshirikisha watu mbalimbali. Baada ya kumalizika Ligi Kuu shamrashamra zingine zinahamia kwenye usajili wa wachezaji. Mmoja ataondoka huku atakwenda kule, na mwingine itakuwa vilevile.
Jambo lingine linalonogesha Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa ni kuwepo kwa wasemaji wa timu za Ligi Kuu. Utaratibu wa kuajiri wasemaji umeasisiwa na shirikisho la Soka duniani kwa lengo la kuimarisha mifumo ya uongozi katika mchezo huo. Makala haya yanawachambua wasemaji watano wanaong’ara katika kipindi hiki cha usajili……
THOBIAS KIFARU
Ni msemaji mkongwe wa klabu ya Mtibwa Sugar, Turiani ya mkoani Morogoro. Mwanzoni wa miaka ya 2000 alikuwa aking’ara peke yake. Akihojiwa na redio mbalimbali kwenye vipindi vya michezo utamsikia namna anavyojitapa. Anaweza kuipamba timu yake, kocha wao na mchezaji mmoja mmoja. Anaweza kutumia mdomo wake kuitisha timu pinzani itakayokabiliana na Mtibwa Sugar.
Miaka ya nyuma mashabiki walitegemea redio kusikiliza mechi za Ligi Kuu kabla ya mapinduzi yua televisheni yaliyoletwa na Azam TV na shirikisho la Soka nchini, TFF.
Kifaru alisikika katika vipindi vya michezo katika redio mbalimbaili. Alijigamba kwa madoido, akaifanya Mtibwa Sugar iwe gumzo. Uzuri wa timu hiyo ilikuwa mahiri uwanjani, na ndiyo pekee kutoka mkoani kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo chini ya kocha John Simkoko.
Kifaru ni kifaru haswa. Kipinid hiki anaonekana kukabiliwa na changamoto kutoka kwa wasemaji wengine pamoja na kupanuka wigo wa upashanaji habari. Lakini Thobias Kifaru anabaki kuwa mmoja wa wasemaji wanaong’arisha Ligi Kuu Tanzania Bara.
MASAU BWIRE
Kijana mpya katika usemaji wa klabu ya Yanga, yenye makazi mitaa ya Jangwani na Twiga, Kariakoo jijini Dar es salaam. Nimepata kuifanya kazi na Bumbuli wakati akiwa mhariri wa gazeti la kila siku la michezo la Bingwa.
Uzuri anajua kuipanga safu yake, anapenda utendaji wa pamoja. Ni mahiri wa kuvumbua vipaji. Lakini sasa anatumikia klabu kubwa yenye historia kubwa. Ndiyo, Yanga ndiyo timu yenye historia ya kutwaa taji la Ligi Kuu mara nyingi zaidi kuliko zingine.
Bumbuli amekuwa akiinuka kila kukicha. Amekuwa akikabiliana na vyombo vya habari hasa waandishi wenzake ambao sasa anatakiwa kukabiliana nao; kwa maswali, vibweka na uchunguzi.
Ni msemaji ambaye amewakosha Yanga kwa sasa. Ni uvumilivu na hodari wa kupanga na kupangua hoja. Kitu kimopja ambacho amejinyima ni maneno yenye ngebe,tambo,vitisho kama wenzake. Lakini ni mwanazuoni wa taaluma ya uandishi wa habari ambaye amekuwa chachu ya ushindani katika usemaji wa klabu hapa nchini.
HAJI MANARA
Msemaji wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, wenye makazi katika mitaa ya Msimbazi Kariakoo jijini Dar es salaam. Haji Manara amekulia Kariakoo jijini Dar es salaam. Ni mtoto wa mjini kama wasemavyo wenyeji wa mijini yaani mjanja mjanja.
Ni mchokozi, ana utani mwingi, ana maudhi, anakera, anafurahisha, anachekesha, anahamasisha na kwa watu wengine wanaamini Haji Manara anamiliki ghala ya vituko ambavyo vimewafanya mashabiki wa Simba watembee kifua mbele.
Kwenye mchezo woewote amekuwa mtu wa kwanza kuhamasisha mashabiki kujaa uwanjani. Amewajaza imani na kujiamini mashabiki wa Simba. Matokeo ya mechi nyingi za Simba hadi ubingwa yamekuwa mazuri wakati wote na ambayo yanwapa vicheko mashabiki wake.
Nyuma ya amsha amsha ya Simba huwezi kuliacha jina la msemaji huyu. Anaweza kuwachokoza Yanga, kisha akawataka mashabiki wa Simba watulie. Azungumzapo na vyombo vya habari ni kivutio kingine.
Anaonesha hisia zake zote katika mchezo wa soka. Anawateka mashabiki kisaikolojia kiutokana na vitendo vyake. Viongozi wake bila shaka wanaona thamani ya msemaji wao. Mashabiki wa anmpenda. Viongozi wanampenda. Naye amewapenda mashabiki na viongozi wake.
Ni mwasisi wa majina ya utani dhidi ya Yanga kama vile nyura FC, Utopolo FC, Bwawani na kadhalika. Maneno ya Haji Manara yanaweza kuudhi na kufurahisha. Wapo walipwahi kukerwa na maneno yake, lakini kwa mtazamo wangu anachokifanya ni kuchangamsha mchezo wa soka. Anawaamisha waliolala. Anawakumbusha umuhimu wa mchezo wa soka kuwa amani,furaha na utani.
MASAU BWIRE
Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting, mkoani Pwani. Ni msemaji ambaye ametajwa kumiliki simu zaidi ya 5 kwa shughuli mbalimbali za usemaji na kijamii. Ni msemaji ambaye anasifika kwa kuhamasisha timu yake. majigambo, sifa,ngebe, misemo mikali inayosisimua. Ni msemaji kipenzi cha waandishi wa habari za michezo.
Anasifika kuwashambulia waamuzi wabovu, makocha na wachezaji wabovu wa timu pinzani. Anajulikana kwa matamshi yenye utata.
Watu wa karibu wameaniambia amewahi kuombwa kufanya kazi na mojawapo ya timu kubwa za Dar es salaam, lakini ofa hiyo alikatupilia mbali kwa madai anaishi vizuri na waajiri wke hivyo asingependa kuondoka. Naye kama alivyo Thhobias Kifaru amekuwa maarufu kwenye redio mbalimbali hususani vipindi vya michezo.
THABIT ZAKARIA
Ni msemaji mpya. Kijana mpya alioyekabidhiwa jukumu la kuwa msemaji wa matajiri wenye makazi yao viunga vya Chamanzi. Ni matajiri wa Azam Fc. Jia lake maarufu ZakaZakazi. Sifa yake kubwa ni mtakwimu mzuri mno katika soka la Tanzania. Anasifika kuwa mwandishi wa habari aliyejikita kwenye ukusanyaji wa historia na takwimu za