*kipindi hiki ni kwenye sekta binafsi*
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umezidi k”kupenya’ kwenye sekta binafsi na kuvuna wanachama zaidi kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, ambapo wanakikundi wajasiriamali wa kundi la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (Voice of Women Entrepreneurs Tanzania-VOWET).
![Wanachama wapya](https://i0.wp.com/s3.amazonaws.com/tanzaniasports.com/2015/10/13234412/New-members-1280x661.jpg?resize=640%2C331&ssl=1)
Wanachama hao wapya walijiunga baada ya kushiriki warsha ya siku moja ambayo ilifanyika kwenye ukumbi wa Belmonte ulioko jengo la makao makuu ya PSPF, jijini Dar es Salaam Oktoba 13, 2015, ambapo Mabalozi wa Mfuko huo, Msanii wa majigambo, Mrisho Mpoto na Mwanamitindo wa Kimataifa anayeishi na kufanyia kazi zake jijini New York Marekani, Flaviana Matata, walishiriki kutoa “Darasa” kuhusu umuhimu wa Watanzania walio katika sekta bionafsi kuchangamkia fursa kupitia kuiunga na uamancaha wa Mfuko huo kupitia mpango wa PSS.
![Mabalozi hao waliongozwa na Meneja wa Mpango wa PSS, Mwanjaa Sembe, na Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko huo, Magire Werema, ambao wote kwa pamoja walifafanua na kueleza kwa kina faida za kuwa mwanachama wa Mfuko huo, ambapo kwa muda mfupi baada ya kujiunga Mwanachama anawezakufaidi mafao mbalimbali yatolewayo na Mfuko huo ikiwemo mikopo ya nyumba, Fao la Elimu, na mengine mengi.](https://i0.wp.com/s3.amazonaws.com/tanzaniasports.com/2015/10/13234224/Magire-Werema3-e1444768971875.jpg?resize=662%2C441&ssl=1)
![Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Sembe, akitoa mada](https://i0.wp.com/s3.amazonaws.com/tanzaniasports.com/2015/10/13233453/Mwanjaa-Sembe1-e1444768533274.jpg?resize=662%2C441&ssl=1)
![Mjumbe wa Bodi ya Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania, VOWET, Anne A. Ottieno, akiuliza swali](https://i0.wp.com/s3.amazonaws.com/tanzaniasports.com/2015/10/13232611/Anne-A-Ottieno-e1444768007234.jpg?resize=662%2C441&ssl=1)
Mjumbe wa Bodi ya Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania, VOWET, Anne A. Ottieno, akiuliza swali
Wanachama wa VOWET, wakijaza fomu za kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari PSS, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakati wa Warsha hiyo
![wanachama wa VOWET, wakijaza fomu tayari kuwa wanachama wa PSPF, kupitia mpango wa PSS](https://i0.wp.com/s3.amazonaws.com/tanzaniasports.com/2015/10/13232936/Wanachama-wapya-1205x800.jpg?resize=640%2C425&ssl=1)
—————————————————————————————————————————————————————————
![Meneja wa Mpango wa PS, Mwanjaa Sembe, (kushoto), akimsikiliza Mjumbe wa Bodi ya VOWET, Anne Ottieno wakati akijiandaa kujaza fomu za kujiunga na Mpango huo](https://i0.wp.com/s3.amazonaws.com/tanzaniasports.com/2015/10/13233205/Mwanjaa_Aanne-Ottieno-1192x800.jpg?resize=640%2C430&ssl=1)