Menu
in , , ,

MECHI ZA YANGA, SIMBA ZAINGIZA MIL 182/-

Mechi za Yanga na Simba za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zilizochezwa wikiendi
iliyopita jijini Dar es Salaam zimeingiza jumla ya sh. 182,103,000.

Yanga katika mechi yake dhidi ya Ruvu Shooting iliyochezwa Jumamosi
(Septemba 28 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 imeingiza sh. 94,202,000.

Watazamaji 16,492 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo ambapo kila klabu
ilipata mgawo wa sh. 22,630,921.58. Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa
sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000, na Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 14,369,796.61.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,507,248.26,
tiketi sh. 3,117,215, gharama za mechi sh. 6,904,348.96, Kamati ya Ligi sh.
6,904,348.96, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,452,174.48
na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,685,024.59.

Nayo Simba ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu katika
mechi iliyochezwa Jumapili (Septemba 29 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam imeingiza sh. 87,901,000.

Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 41 walikuwa
15,780.* *Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh.
15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 21,051,025.92
wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 13,408,627.12.**

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 10,703,911.48,
tiketi sh. 3,132,963, gharama za mechi sh. 6,422,346.89, Kamati ya Ligi sh.
6,422,346.89, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,211,173.44,
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,248,789.67 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 1,248,789.67.

* *

*Wakati huo huo,* mechi ya ligi hiyo kati ya Mbeya City na Coastal
Union iliyochezwa
Jumamosi (Septemba 28 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini
Mbeya imeingiza sh. 16,959,000 huku kila klabu ikipata sh. 4,035,229.

Mgawo wa mechi hiyo ulikuwa ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
sh. 2,586,966, uwanja sh. 2,051,811.57, tiketi sh. 696,290, gharama za
mechi sh. 1,231,086, Kamati ya Ligi sh. 1,231,086, Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) sh. 615,543, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya
(MREFA) sh. 478,756.

* *

*MICHUANO YA CHALENJI KUANZA NOV 27*

Michuano ya Kombe la Chalenji inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa
Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) inafanyika Kenya kuanzia Novemba 27
hadi Desemba 12 mwaka huu.

Nchi wanachama ambazo zinataka kushiriki zinatakiwa kuthibitisha ushiriki
wao kwa Sekretarieti ya CECAFA kabla ya Oktoba 20 mwaka huu. Wanachama wa
CECAFA ni Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia,
Sudan, Sudan Kusini, Tanzania, Uganda na Zanzibar.

Michuano hiyo itatanguliwa na Mkutano Mkuu wa CECAFA utakaofanyika Novemba
26 mwaka huu ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na ajenda ya uchaguzi.
Uchaguzi huo ni kwa ajili ya kujaza nafasi nne za wajumbe wa Kamati ya
Utendaji.

Wajumbe wanaomaliza muda wao ni Sahilu Gebremarian wa Ethiopia ambaye pia
ni Makamu Mwenyekiti wa CECAFA, Abdigaani Saed Arab (Somalia), Tariq Atta
(Sudan) na Raoul Gisanura (Rwanda).

Majina ya wagombea yanatakiwa kuwa yamewasilishwa katika Sekretarieti ya
CECAFA kabla ya Oktoba 20 mwaka huu, na yakiwa yamethibitishwa na vyama
vyao vya mpira wa miguu.

*SUALA LA PAPIC, YANGA LASUBIRI UAMUZI WA FIFA*

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limewasilisha rasmi suala
la madai ya aliyekuwa Kocha wa Yanga, Kostadin Papic dhidi ya klabu hiyo
katika Kamati ya Hadhi ya Wachezaji.

FIFA imesema imepeleka rasmi suala hilo katika kamati yake hiyo baada ya
kupokea vielelezo vya Papic anayedai kuidai Yanga dola 10,000 za Marekani
pamoja na vile vya Yanga inayodai kumlipa kocha huyo fedha zote alizokuwa
akiidai klabu hiyo.

Kwa taratibu za FIFA, hivi sasa haitapokea vielelezo vingine kutoka pande
hizo mbili, na badala yake Kamati hiyo inayoongozwa na Theo Zwanziger
kutoka Ujerumani itafanya uamuzi na kuziarifu pande husika. Zwanziger
kitaaluma ni mwanasheria.

Papic aliyeinoa Yanga kwa vipindi viwili tofauti aliwasilisha malalamiko
yake FIFA akidai hadi mkataba wake unamalizika klabu hiyo ilikuwa
haijamlipa dola 10,000 za Marekani.

*LIPULI, MAJIMAJI KUUMANA WAMBI FDL*

Mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Lipuli ya Iringa na Majimaji
ya Songea sasa itachezwa kesho (Oktoba 2 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Wambi
uliopo Mafinga badala ya Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa.

Mabadiliko hayo yamefanyika kutokana na Serikali kuutumia Uwanja wa
Kumbukumbu ya Samora kwa ajili ya shughuli za mbio za Mwenge.

Mechi nyingine ya FDL kesho itakuwa kati ya Tessema FC ya Dar es Salaam na
Ndanda FC ya Mtwara, na itafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
jijini Dar es Salaam.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version