Kaimu kocha wa timu ya taifa Tanzania “Taifa Stars” Hemedi Suleiman “Morocco” leo amefanya mkutano wa waandishi wa habari makao makuu ya TFF yaliyopo Karume. Tanzania Sports ilikuwepo kwenye mkutano huo wa waandishi wa habari kushuhudia kutajwa kwa kikosi hicho.
Hemedi Suleiman “Morocco” amedai kuwa ameita wachezaji wengi wanaocheza ligi ya ndani kwa sababu ligi yetu inafanya vizuri ni ligi ya sita kwa ubora Afrika. Pia wachezaji wengi wanacheza kwenye michuano ya kimataifa na wanafanya vizuri.
Hemedi Suleiman “Morocco” amedai kuwa kwa sasa hatuna wachezaji bora wanaocheza nje ya nchi ila wachezaji hawa wa ndani kwa sasa wanafanya vizuri hivo inabidi wasukumwe ili waende nje kitu ambacho amedai kuwa inawezekana.
Kuhusu kurudishwa kwa nahodha Mbwana Ally Samatta amedai kuwa kwa sasa timu inatatizo la sehemu ya kushambulia kwa hiyo Mbwana Ally Samatta anakuja kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji.
Taifa Stars inakabiliwa na michezo miwili dhidi ya DR Congo, michezo ya kuwania kufuzu Afcon ya 2025 itakayochezwa nchini Morocco. Mechi hizi mbili zitakazochezwa dhidi ya DR Congo zitachezwa tarehe 10 mwezi wa 10 na tarehe 15 mwezi 10. Hiki ndicho kikosi kilichoitwa.
MAKIPA
Ally Salim (Simba SC)
Zuberi Foba (Azam FC)
Yona Amos (Pamba SC)
MABEKI
Mohamed Hussein (Simba SC)
Lusajo Mwaikenda (Azam FC)
Pascal Msindo (Azam FC)
Ibrahim Hammad (Yanga SC)
Bakari Nondo (Yanga SC)
Dickson Job (Yanga SC)
Abdulrazak Hamza (Simba SC)
Haji Mnoga (Salford City)
VIUNGO
Adolf Mtasingwa(Azam FC)
Habib Khalid(Singida Black Stars)
Himid Mao(Talaal El Geish)
Mudathiri Yahya(Yanga SC)
Feisal Salum(Azam FC)
WASHAMBULIAJI
Suleiman Mwalim (Fountain Gate FC)
Cyprian Kachwele (Vancouver Whitecaps)
Mbwana Samatta (PAOK FC)
Kibu Denis ( Simba SC)
Nassoro Saadun (Azam FC)
Abdullah Said (KMC FC)
Clement Mzize (Yanga SC)