Akiwa mkuu wa wilaya ya Hai alihakikisha timu nyingi za shule za msingi na sekondari zinashiki mashindano maarufu ya Kombe la Bonite kila mwaka.
Hivi majuzi nilishiriki mjadala mzito uliofanyika Chuo Kikuu Huria OUT Kitivo cha Sanaa katika kusherekea miaka ishirini tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.
Mtoa mada mkuu katika mjadala huo alikuwa Jenerali Twaha Halfani Ulimwengu.
Ndugu Ulimwengu alikuwa akizungumzia kuporomoka kwa kasi kwa maadili ya Watanazania hususani viongozi wetu. Akimkaribisha Ndugu Ulimwengu mmoja wa viongozi waandamizi wa Chuo Kikuu Huria Profesa Mbwiliza hakusita kumwagia sifa kedekede kwa mtoa mada na haswa misimamo yake katika utetezi wa wanyonge katika makala zake na hata kuwa tayari kujiuzulu pale anapoona haki haitendeki.
Sio nia yangu kujadili nini alichosema mtoa mada licha ya ukweli kukubaliana nae kwa yale aliyoyasema haswa kwa upande wa kuoza kwa maadili. Rushwa imekithiri mno miongoni kwa jamii kiasi cha kutisha.
Sio ajabu kuona baba, mama na watoto ndani ya nyumba moja wakishiriki kwa nguvu zote katika masuala ya rushwa. Ni kweli ukiona msitu au nyika hauna nyoka hata mmoja basi hapo kuna kasoro lakini ukiona msitu kuna nyoka wengi zaidi basi hapo lazima hatua madhubuti zichukuliwe kwani madhara yake yatakuwa makubwa. Ndugu Ulimwengu aliongelea mengi ikiwa pamoja na matumizi mabaya ya madaraka abuse of power ya viongozi wetu ikiwa pamoja na mauzo ya nyumba za serikali.
Lengo langu ni kuzungumzia yale aliyoniuliza mara tu aliponiona katika ghafla ile. Vipi mbona volleyball inakufa? Lilikuwa ni swali nzito kwangu na haswa ukuitilia maanani ndugu Ulimwengu alikuwa mdau mkubwa wa Volleyball nchini.
Akiwa mkuu wa wilaya ya Hai alihakikisha timu nyingi za shule msingi na sekuondari zinashiki mashindano maarufu ya Kombe la Bonite kila mwaka.
Akiwa naibu Mkurugenzi maendeleo ya michezo nchini alihakikisha timu za taifa na vilabu vinashiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo klabu bingwa Afrika.
Kuna wakati Ndugu Ulimwengu aliamua kuongozana na timu yetu hadi Lusaka kwa treni na kurudisha tiketi ya ndege aliopewa na serikali. Sina hakika lengo lake lilikuwa nini lakini labda alitaka nae apate shida kama sisi wakati tukienda kupigania taifa letu kimichezo mjini Lusaka. Ni viongozi wachache wanaodiriki kufanya hivyo
Nilichoweza kumjibu Ulimwengu ni kuwa Volleyball haijafa kwani tuna mpango wa miaka mitano tukishirikiana na Shirikisho la Dunia Mpira wa Wavu FIVB kundeleza waalimu na waamuzi .
Pia tuna mkakati mwingine wa kuendeleza vipazi vya watoto kupitia COOL VOLLEY .
Vifaa vya mpango huo tayari vimeshawasili na wakati wowote tutazindua rasmi mpango huo utakaolenga zaidi watoto wa shule za msingi.
Mwisho tuna mpango wa kufanya kongamano kubwa la wadau wetu wakiwemo waliowahi kuongoza volleyball mapema mwakani ili tupate mawazo yao katika maendeleo ya mpira wa wavu nchini. Miongoni mwa wadau hao ni Balozi Juma Volter Mwapachu, Major General Rowland Leslie Makunda, Patrick Jacob Sombe na Balozi Abdul Cisco Mtiro.
Pia kutakuwepo na wafanyabiashara maarufu kama Reginald Mengi waliofanikisha maendeleo ya volleyball kupitia kampuni yake tanzu ya BONITE BOTTLERS
Makala hii imeandikwa na Muharame Mchume