Karibu kila baada ya ndege kuondoka kutoka katika viwanja tofauti Maximo alikuwa akianza kusali hadi wakati mwingine alikuwa akisinzia.
Kocha huyo raia wa Brazil aliiambia Mwananchi kuwa alikuwa akifanya hivyo kumuomba Mungu kwa lengo la kuona anafanikiwa.
Ni kitu cha kawaida kabisa, kuomba Mungu kwa kila kitu ni bora lakini ninachokuhakikishia sipendi kuona timu hii inapoteza mchezo hata kama tutakuwa ugenini.
”Nataka kuona mafanikio zaidi na mechi iliyopita dhidi ya Mauritius haikunifurahisha, ilienda kinyume na mafanikio yangu ndio maana sitaki kupata hofu mfululizo”, alisema.
Kilichoshangaza zaidi, Maximo alikuwa akisali kwa muda mrefu huku akizungumza kwa sauti iliyokuwa ikisikika kwa mbali.
Mara nyingi alikuwa akifanya hivyo baada ya kutoa kitabu chake na kuandika mambo kadhaa ambako kuna majina ya wachezaji akionyesha kupanga mipango na atakachofanya.
Tayari ameeleza kocha huyo kuwa amepata ofa kutoka katika timu nne zikitaka ajiunge na timu hizo lakini mwenyewe amesisitiza kwamba anataka kubaki Tanzania kama Tanzania itakubali kumbakiza.
Kwa hisani ya Mwananchi.