Mechi 6 zimepita bila Arsenal kumfunga Tottenham Hotspur’s.
Hii yote ni kwa sababu Tottenham Hotspur’s inazidi kuimarika siku baada ya Siku.
Na hakuna ubishi kuwa Tottenham Hotspur’s kwa sasa ni bora kuzidi Arsenal.
Tottenham Hotspur’s imekuwa timu ambayo inacheza kwa kuelewana na ikionekana kukamirika zaidi kuliko Arsenal.
Msimu huu imeimarika zaidi hata baada ya nyota wao wengi kupatwa na majeruhi .
Mfano, kwa misimu miwili iliyopita Dembele na Wanyama wamekuwa mhimili mkubwa kwenye kiungo cha Tottenham Hotspur’s , lakini baada ya msimu huu kupata majeraha hakuna pengo la moja kwa moja lilionekana.
Utambulisho wa baadhi ya wachezaji katika eneo la kati ambao walifanya timu icheze bila kutetereka.
Danny Winks, Eric Dier , Sissoko kwa nyakati tofauti walicheza katika eneo la katikati na bila timu kuyumba.
Hii yote inaonesha kikosi chao kwa sasa ni kipana tofauti na misimu kadhaa nyuma.
*Leo wanaenda Emirates watafanikiwa kuwafunga Arsenal?*
Arsenal mpaka sasa amefikisha michezo kumi bila kupoteza nyumbani.
Timu yao inaonesha ni ngumu inapokuwa inacheza zaidi katika uwanja wake wa nyumbani.
Hivo huu utakuwa mtihani mgumu kwa Tottehnham Hotspurs kufanikiwa kupata ushindi mbele ya Arsenal.
*Kipi ambacho Spurs wafanye ili wawafunge Arsenal?*
Kitu pekee ambacho Tottenham Hotspurs kitakuwa silaha kwao, ni kumruhusu Erricksen acheze huru kuanzia eneo la katikati ya uwanja ili kuleta muunganiko wa kati ya eneo la katikati ya uwanja na eneo la mbele.
Na pia kuwaanzisha Son na Kane kwa pamoja kutakuwa na faida kwa Tottenham Hotspur’s kwa sababu, Son Mara nyingi ana kasi, kasi ambayo hufanya kuleta uwazi mkubwa eneo la nyuma ya washambuliaji.
Kwa sababu wakati Son anakimbia, huwalazimisha mabeki kumkaba, wanapomkaba huacha nafasi eneo lao, nafasi ambayo hutumiwa vzuri na Kane.
Hivo kumwanzisha Erricksen na kumwacha huru kutakuwa kunamsaidia kutengeneza nafasi kwenye uwazi ambao utakuwa unaachwa na mabeki wa Arsenal.
Kuna taarifa Hugo Lloris, Jan Vertonghen, Dele Alli na Harry Kane wanarudi kwenye mechi hii.
Hawa ni moja ya wachezaji mihimili mikubwa kwenye timu ya Tottenham Hotspurs kurejea kwao kutakuwa na faida kubwa sana.
*Je kutokuwepo kwa Toby Alderweireld kutakuwa na madhara kwa Tottenham Hotspur’s?*
Ingizo la beki wa Tottenham Hotspurs, Sanchez limekuwa jambo ambalo linaleta uhai eneo la nyuma .
Hii itampa nafasi Pochettino kuwaanzisha mabeki watatu.
*Arsene Wenger aanze na viungo wengi wa kuzuia?*
Mimi sioni sababu ya yeye kuingia kwa kujihami kwenye hii mechi.
Kumwanzisha Xhaka na Ramsey kutaleta uwiano mzuri.
Xhaka atatumika katika kuchukua mipira na kuanzisha mashmbulizi, huku Ramsey kwenda kila sehemu ambayo mpira upo na kuleta uwiano wa eneo la kushambulia na kuzuia.
Cha muhimu ni Ozil kuanzia katika benchi na kumpa nafasi Iwobi au Wilshere kwa sababu hawa wanaweza wakashuka chini kuchukua mipira na kuanzisha mashambulizi kwa uimara.
*Lacazzete anatakiwa kwenye hii mechi ?*
Mfungaji bora wa kikosi cha Arsenal mpaka sasa. Amekuwa mtu muhimu kwenye kikosi cha Arsenal kwa kuhusika kwenye magoli mengi.
Vivo kumwanzisha yeye pamoja na Alexie Sanchez kwa pamoja kutaleta uhai mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji ya Arsenal.
*Arsenal kuingia kama underdogs kwenye mechi ya leo itakuwa na madhara au hasara kwao?*
Hii inategemea ni kwa jinsi gani ambavyo watakavyoipokea hii hali ya wao kuwa underdog’s.
Wakiipokea kinyonge, wataingia na hofu kubwa uwanjani. Ukiingia na hofu uwanjani unakuwa unapunguza umakini ndani ya uwanja.
Unapopunguza umakini ndani ya uwanja unatoa nafasi kubwa ya kufanya makosa mengi binafsi.
Unapofanya makosa binafsi unakuwa na nafasi kubwa ya kuadhibiwa.
Ila kama wakiukubali hali ya wao kuwa underdog’s itakuwa na faida kubwa sana kwao, kwa sababu wataingia bila hofu wakiwa na utulivu.
Utulivu ambayo utawpa nafasi wao kufanya maamuzi sahihi zaidi uwanjani.
Mail to: martinKiyumbi@gmail.com