Wakati Simba wakiendelea kurandaranda barabarani kusherehekea ubingwa wao wa 21 wa ligi kuu Tanzania Bara.
Leo hii tuangalie namna ilivyopita japo sio kwqa ukubwa huo ila tunakukumbusha matukio muhimu.
Simba imeanza mikikimikiki ya ligi kuu Bara kwa kucheza na JKT Tanzania wakiibuka na ushindi wa magoli 3-1.
Hiyo ndio siku nzuri kwao ilikuwa siku ya jumapili ya Agusti 29 uwanja wa taia jijini Dar es Salaam.
Aliyefungua pazia la magoli ni Meddie Kagere ambapo alifunga magoli 2 na Miraji Athumani akifunga goli moja.
Safari ikaanza vizuri kabisa huku wakijiamini kutetea taji lao kwakuwa mwanzo ulikuwa mzuri na muelekeo mzuri.
Katika safari hakukosi machungu, jambo kubwa ambalo huwa linaviumiza vilabu viwili vikubwa hapa Tanzania ni pamoja na kufungwa na mpinzani wake.
Katika vichapo vitatu walivyovipata moja wapo ilikipata dhidi ya Yanga mchezo uliopigwa uwanja wa taifa Dar es Salaam ambapo Bernard Morrison alifunga goli lake la kwanza katika ‘Derby’ na goli la tatu la ligi kuu tangu ajiunge na timu hiyo Januari mwaka huu.
Katika hayo machungu Simba ilifungwa na timu tatu tu nyingine ni Ruvu Shooting ambapo nao walipata goli moja kwa nunge wakati Mwadui FC nao waliwagema Simba goli moja kwa yai.
Huenda hii ikawa historia hadi hii leo katika michezo 32 iliyocheza Simba imepoteza mara tatu tena kwa goli 1-0.
Simba ndio timu pekee ligi kuu Bara kwani hadi kufikia leo hii ikiwa na michezo 32 kushinda magoli mengi kwa mchezo mmoja. Iliitandika Singida United magoli 8 kwa sufuri.
Wekundi wa Msimbazi wamebadili makocha wawili katika msimu mmoja ambapo hata timu nyingine zimefanya hivyo makocha hao ni Patrick Aussems pamoja na Sven Vandenbroeck.
Lakini bao timu hiyo katika michezo 32 imetoa sare nne ikiwa dhidi yaYanga 2-2, Tanzania Prisons mara mbili ya kwanza ilikuwa 0-0 na yapili 0-0, ya nne dhidi ya Ruvu Shooting 1-1.
Ili kuona weledi unaendelea Kocha wa Yanga Luc Eymael amewapongeza wapinzani wake Simba kwa kuchukua Ubingwa wa ligi kuu Bara.
kocha huyo amesema anawapa pongezi Simba kwa kuweza kutwaa taji la ligi.
“Hongera kwa Simba kutwaa taji la ligi kwa msimu huu,” alisema.
Wakati huo huo Afisa Muhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amewapongeza Simba kwa ubingwa .
“Hongerini watani zetu kwa kutwaa ubingwa wa ligi kwa msimu wa 2019/20.”
Ili kuweza kukomaa na kuendelea kimataifa Yanga inahitajika ichukue ubingwa wa kombe la FA ambalo ni gumu kutokana na ubora wa vikosi vingine vilivyoingia hatua ya robo fainali.
Yanga itawavaa Kagera Sugar kesho jumanne wakati Simba yenyewe itacheza na Azam ambayo nayo inatafuta nafasi ya kucheza michuano ya kombe Shirikisho la Soka barani Afrika.
Hapa tueleweke kuwa bingwa ameshapatikana ila bado michezo mitano kila kila timu hivyo burudani bado inaendelea.
Pia takwimu za Simba zinaweza kubadilika huenda kutoka katika kupoteza michezo mitatu ikaongezeka au kubaki hapo, katika sare nne zinaweza kuongezaka au kubaki.
Ila takwimu hii hadi kufikia michezo 32 ambapo tayari Simba imetangaza ubingwa ilipocheza dhidi ya Tanzania Prisons katika uwanja wa Sokoine.
Maoni ya Mwandishi :-
Simba ilicheza vizuri na ilichanga vizuri karata zake tangu awali lakini pia ilikuwa na timu nzuri iliyokuwa na ushindani wa hali ya juu na ndio maana wamechukua ubingwa wa ligi haikuwa bahati.
Wasiwasi wangu huko waendako katika klabu bingwa Afrika watakuwa wamejiandaa vyema kwa namana ya timu yao iliyokuwa inacheza michezo ya ligi hapa ndani ?
Bado sioni mbali huenda wabadilike na usajili waangalie nafasi zinazohitajika sio kusajili kwa kufuata mkumbo.
Bado wanayo nafasi ya kufika mbali wakijipanga sawa sawa waliweza kufika robo fainali kwa sasa wafikirie hatua ya mbali zaidi ya hapo.
Ukweli ni kwamba kikosi cha Simba kilichofika robo fainali kina ubora mkubwa kuliko hiki kilichochukua ubingwa wa Bara msimu huu.
Kwa sasa macho na masikio yapo kwa mabingwa hao wa bara hivyo ni vizuri wajipange na watumie fursa vizuri.