Menu
in , , ,

Matatani kwa kupanga matokeo England


*DJ Campbell akamatwa na kuhojiwa
*Wanigeria waeleza walivyodaka noti

DJ Campbell aliyecheza Ligi Kuu ya England (EPL) ni mmoja wa watu sita wanaohojiwa kwa tuhuma za kuhusika kupanga matokeo ya mechi za soka.

Klabu yake ya Blackburn iliyo daraja la pili imethibitisha kwamba mchezaji wao huyo anahojiwa.
Watu sita walikamatwa Jumapili kwa kuhusishwa na makosa hayo, baada ya mchezaji wa zamani wa Portsmouth, Sam Sodje kusema alikuwa na uwezo wa kupanga wachezaji wapewe kadi za njano au nyekundu kwa malipo ya fedha.

Klabu yake ya Portsmouth imeeleza kushitushwa na habari hizo, kwamba wachezaji kadhaa walisuka mipango wacheze rafu ili wapewe kadi na timu zao zifungwe.

Campbell (32) ambaye jina lake kamili ni Dudley Junior Campbell amecheza EPL katika klabu za Birmingham, Blackpool na Queen Park Rangers (QPR).

“Kutokana na taarifa za leo kwenye vyombo vya habari, Blackburn Rovers tunathibitisha kwamba DJ Campbell amekamatwa na anahojiwa lakini klabu haitazungumzia tena suala hili kwa sababu sheria inachukua mkondo wake,” klabu hiyo imesema.

Majina ya wachezaji wengine watano waliokamatwa na kuhojiwa hayakuwa yamethibitishwa hadi asubuhi ya Jumatatu hii.
Sodje ambaye ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Nigeria, anasema aliwahi kumpiga mchezaji wa timu pinzani ili apewe kadi nyekundu na timu yake ifungwe, ambapo alilipwa dola 70,000.

Inatambulika kwamba alipewa kadi nyekundu kwenye dakika ya 50 katika mechi ya League One akichezea Portsmouth dhidi ya Oldham Athletic Februari 23.

Kadhalika, mchezaji wa Oldham, Cristian Montano anadaiwa kumwomba radhi Sodje kwa kushindwa kufanya faulo ambayo ingempatia kadi ya njano kwa mujibu wa makubaliano yao katika nusu ya kwanza ya mechi dhidi ya Wolves Oktoba 22.

Kaka yake Sodje anayeitwa Akpo, ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya Tranmere Rovers naye ameshuhudia kwamba alikuwa tayari kulipwa ili akishaingia uwanjani acheze rafu na kupewa kadi.

Tuhuma hizo zimesababisha Taasisi ya Taifa ya Kupambana na Uhalifu kuanza kufuatilia suala hilo linaloelekea kuitia doa soka ya England.

51.577411-0.154779

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version