Menu
in , , , ,

Manchester City wavuka Ulaya

Hatimaye Manchester City wamefanikiwa kuvuka kihunzi na kufuzukwa hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) baada ya kuwafunga Roma 2-0 na kufanya England waingize timu tatu, wakiwamo Arsenal na Chelsea.

Mabao yaliyofungwa na Samir Nasri dakika ya 60 na Pablo Zabaleta dakika ya 86 yaliwahakikishia vijana wa Manuel Pellegrini kusonga mbele, ukiwa ni ushindi wa kwanza kwao kuupata nchini Italia.

Walikuwa wakipewa nafasi ndogo kwani walianza vibaya michuano hii, ambapo baada ya mechi nne walikuwa na pointi mbili tu. Msimu uliopita walivuka pia kuingia hatua ya 16 bora, safari hii kwenye kundi lao wakivuka na Bayern Munich.

Joe Hart aliokoa mabao mawili, moja likiwa ni kiki ya Gervinho na jingine kichwa cha
Kostas Manolas, ambapo mpira uliishia kugonga mwamba na madhara kuepushwa. Bayern Munich usiku huo wa Jumatano waliwakung’uta CSKA Moscow 3-0 kuwahakikishia City wanasonga mbele, maana hatima haikuwa mikononi mwao.

Walitiwa kasi na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Bayern Munichi, ikiwamo hat-trick ya Sergio Aguero ambaye Jumatano hii hakucheza kutokana na kuumia, na anatarajiwa kuwa nje kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Kwenye kundi lao, City wamemaliza mechi zao sita wakiwa na point inane wakati Bayern wanazo 15, Roma na CSKA wakiachwa nyuma kwa pointi tano, lakini iwapo wangeshinda wangeweza kuwatupa nje City.

Pellegrini amesema kikosi chake kilicheza vyema na kilistahili ushindi huo na pia sifa zaidi kuliko ambavyo wanahabari wanakichukulia. Amesema kubwa walilofanya ni kujiamini. Ushindi huo umepatikana licha ya kutokuwapo pia kwa nahodha Vincent Kompany na Yaya Toure aliyekuwa na adhabu ya kadi. David Silva aliyetoka kuugua aliweza kucheza dakika 23 tu za mwisho.

Katika mechi nyingine, Ajax waliwafunga Apoel Nic 4-0, Barcelona wakawakandika Paris Saint-Germain 3-1, Chelsea waliokwishafuzu wakawafunga Sporting Lisbon 3-1, NK Maribor wakalala 1-0 kwa Schalke, Athletic Bilbao wakawazaba BATE Bor 2-0 huku Porto wakitoshana nguvu na Shaktar Donetsk kwa 1-1.

Waliovuka kwa kushika nafasi za kwanza kwenye makundi yao ni Atletico Madrid, Real Madrid, Monaco, Borussia Dortmund, Bayern Munich, Barcelona, Chelsea na Porto. Walioshika nafasi za pili na kufuzu ni Juventus, Basel, Bayer Leverkusen, Arsenal, Man City, PSG, Schalke na Shakhtar Donets. Droo kwa ajili ya mechi za mtoano itatangazwa mapema wiki ijayo.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version