Menu
in , , ,

MANCHESTER CITY KULIKONI?

Kutoka Timu Bora ya Dunia hadi Timu Kibonde Ndani ya Mwaka

Wiki tisa, mechi 13, vipigo 9 vinaonyesha kuporomoka kwa kiwango cha ajabu kwa Manchester City, kutoka kuwa timu bora duniani hadi kuwa timu ya kawaida inayoweza kuzuiwa ama kuchapwa na timu nyingine yoyote.

Safari ya kushuka kwao ilianza rasmi Oktoba 30, 2024, walipopoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Tottenham Hotspurs kwenye EFL Cup. Tangu wakati huo, City imeshinda mechi moja pekee, ushindi wa 3-0 dhidi ya Nottingham Forest kwenye Ligi Kuu. Hata hivyo, wamekumbana na vipigo 9 na kutoka sare 3 katika mashindano yote, ikiwa ni pamoja na sare ya 1-1 dhidi ya Everton kwenye siku ya Boxing Day, Disemba 26, 2024.

Angalau Meneja wake, Pep Guardiola, ameanza kubainisha chanzo cha tatizo.  

“Hatufungi mabao kama tulivyokuwa tukifunga, na tunaruhusu mabao ambayo hapo awali hatukuwa tukiruhusu,” Guardiola aliambia BBC baada ya kichapo cha 2-1 kutoka kwa Aston Villa kwenye Uwanja wa Villa Park wiki iliyopita.

Wakati huo anaourejea Pep Guardiola hoja ilikuwa: City itafunga ama itashinda kwa mabao mangapi? Lakini si kuhusu eti City itakwenda sare ama kupoteza.

Kwa hivyo, suluhisho liko wazi, kufunga mabao mengi zaidi na kuruhusu mabao machache. Kushinda mechi badala ya kupoteza. Hii ndiyo hoja ya msingi ya Pep kuhusu kipindi ambacho timu ilikua inamfunga kila mtu, nyumbani na ugenini, timu tishio na yenye soka la maana.

Lakini sasa imegeuka kuwa timu dhaifu, inayofungika kirahisi, isiyo na maelewano na isiyo tisha tena. Uchezaji wao wa kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa sasa unaonekana kama ishara ya kupotea, badala ya kuwa mbinu ya kuwapatia ushindi. 

Swali kubwa hapa Je nini kimetokea? Nini kimeikumba City, je tunaweza kumtupia lawama meneja mwenyewe kwa hili?  

Jambo la kushangaza zaidi ni kuporomoka kwao kwa haraka na kwa kiasi kikubwa na kwa muda mfupi. Hii inaweza kuwa anguko la ajabu zaidi kwa timu bingwa katika historia ya kisasa ya soka.

Nikukumbushe, ni karibu mwaka mmoja uliopita, kikosi kilichojumuisha wachezaji 10 waliocheza dhidi ya Aston Villa Juma lililopita huko Villa Park kiliichapa Fluminense kwa mabao 4-0 kule Jeddah.

Ushindi uliowafanya, City kutwaa mataji yote makubwa na kuwa klabu ya kwanza kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu ya Uingereza, Kombe la Dunia la Klabu, Kombe la FA, na Super Cup ya UEFA kwa wakati mmoja. Walikuwa wamefika kilele cha mafanikio. 

Kwa ngazi ya klabu huo ni ukomo wa kilele cha mafanikio. Walitwaa kila kitu walichoshindania. Lakini sasa, wanaanguka. Tena wanaanguka vibaya na kwa muda mfupi. Wakati City ikienda sare na Everton kwenye mechi ya Boxing Day, kuna nadharia mbili muhimu za kuzingatia kuhusu kuporomoka kwao:  

Tanzania Sports
Kawa Mpole Sana…

Nadhari ya kwanza ya ndani ni timu hiyo kukumbwa na majeruhi wengi. Lakini kuumia kwa kiungo wake, Rodri, mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia ni msiba zaidi.

Tangu aumie kwenye mchezo dhidi ya Arsenal, City imepoteza alama 26 zikiwemo dhidi ya Arsenal yenyewe mpaka mchezo wa hivi Boxing Day dhidi ya Everton.

Ukiacha uwezo wake zikiwemo pasi zake, ukabaji wake na maamuzi yake akiwa na asipokuwa na mpira, nafasi ya Rodri ya kiungo wa chini ni muhimu sana katika uchezaji mzima wa City. Kutokuwepo kwake bila shaka kumeathiri mwenendo wao kwenye ligi na michuano mingine. 

Nadharia ya pili ni ya nje ya uwanja: Sintofahamu ya  kesi ya uvunjifu wa kanuni za kifedha inayoikabili klabu hiyo . Kesi hii si suala dogo, si wachezaji, viongozi wala washabiki wanaweza kutuliza vichwa huku ukikabiliwa na mashtaka 115 ya tuhuma zilizotokea kati ya mwaka 2009  na 2018.

Ingawa wachezaji wana uwezo wa kujielekeza kwenye soka na kuweka kando masuala ya nje ya soka, lakini na wao ni binadamu.Wanafuatilia mijadala, mipango na kufikiria kuhusu mustakabali wao wa baadae. litakua jambo la kushangaza,  kesi hii isiwe na athari kwa namna fulani kwa wachezaji  na timu. 

Nadharia nyingine inamgusa Pep mwenyewe kwamba ndiye chanzo cha kukosekana kwa ari na nguvu ya awali ya City. Baada ya kusainiwa kwa mkataba wake mpya kwa kishindo, ni nadharia ya kawaida kwamba baadhi ya wachezaji wakongwe walikuwa wakitarajia mabadiliko ya kawaida ya morari na nguvu mpya kwenye timu. Kuna uchovu na kuchoka kwa namna Fulani. Guardiola  anashinda kwa kukusukuma ujitoe mpaka tone la mwisho. Kama unashinda hilo ni sawa. Inakuwaje ukiwa unatoa jasho lako mpaka tone la mwisho na haushindi? 

Lakini pia kuna hoja rahisi zaidi ya Guardiola hapa. Hata kocha mwenye mafanikio makubwa zaidi, mwenye ushawishi mkubwa zaidi wa wakati huu anaweza kufikia mwisho wake. Kuna hisia pengine Pep amefikia mwisho kwenye mradi huu wa City ambao umempa mafanikio na kufikia kilele mwaka jana.

Anakosa mkwaju wa tuta..

Kusajiliwa kwa Erling Haaland ambaye ni pendekezo lake ni msumari mwingine wa kuchoma na kujichoma kwa Pep. Haaland anajulikana kwa uwazo wake wa kufunga lakini si aina ya mchezaji anayehusika sana kwenye mchezo. Kwa ufupi yeye ni, mashine ya kufunga mabao. Wazo la Guardiola kujenga timu kumzunguka Haaland linabaki kuwa la ajabu kidogo. 

Haaland anatoa mchango mdogo sana City inapomiliki mpira. Lakini pia ni mzigo kwa sehemu zingine. Ana wastani wa pasi fupi saba kwa mchezo. Kwa mfumo wa sasa unahitaji kila mchango wa mchezaji kwenye kufunga, kuchezesha na kuzuia..Je Halaand atakuwa msaada wa hayo kwa muda mrefu?

Kingine hata takwimu zinaongea tofauti kuhusu Haaland. Katika misimu mitano iliyopita kabla ya kusajiliwa, City walifunga mabao mengi  zaidi kuliko walivyofanya katika misimu miwili na nusu baada ya kumsajili. Wakiwa na Haaland City inafunga wastani wa mabao 2.3 kwa kila mchezo. Kala ya kusaiiwa City  ilikuwa na wastani wa juu wa mabao 2.6 kwa mchezo. Pia wanaruhusu mabao mengi zaidi wakiwa naHaaland katika timu. Unaweza kujiuliza kuna faida gani ya kuwa na muuaji, mwenye makali ya wembe, ikiwa haufungi mabao zaidi, jambo ambalo limejionyesha hata kabla ya kuanza kuporomoka kwao msimu huu?

Ukicha kulega kwa viungo wa kati wa City kunakohusishwa na baadhi kuwa na umri mkubwa, usajili duni pia unatajwa. Josko Gvardiol aliyesajiliwa kwa £77m amekuwa na mafanikio ya kustahili. Kabla ya hapo wapo Manuel Akanji miaka miwili iliyopita, Nathan Aké na Rúben Dias miaka minne iliyopita, Rodri mwaka wa 2019.

Lakini katika miezi 12 iliyopita huoni usajili wa kubadilisha na kuimarisha timu. Wachezai waliopo viwango vyao havijajaboreshwa. Na Pep kama ameridhika. “Hakuna kingine cha kushinda; Nina hisia kwamba kazi imekamilika, imekwisha,” Guardiola alisema wakati alipotwaa kombe la mwisho msimu uliopita., ujumbe ambao unaonekana kuwa wa kinabii zaidi kila wiki inapopita wakati huu City inapoporomoka kwa kasi ya ajabu. .

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version