Menu
in

Manara katudaganya mchana kweupe!!

SIMBA

SIMBA

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha mabingwa watetezi ligi kuu Tanzania  Bara Haji Manara ametudanganya mchana kweupe juu ya upana wa kikosi cha timu hiyo.

Manara aliwahi kusema katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Wasafi Media kuwa kwa kikosi cha pili cha Simba kina uwezo mkubwa wa kuweza kuifunga timu yoyote hapa Tanzania.

Kauli hiyo aliianza muda mrefu akiwa anairudia mara kwa mara ila baada  ya mchezo wa Simba na Mbao FC, ndio imedhihirisha kuwa ubora wa kikosi cha kwanza cha Simba na ule wa kikosi cha pili ni tofuati kubwa sana.

Tuanzie hapa kwanza, kikosi cha awali cha Simba ni pamoja na Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni, Kenedy Juma/Pascal Wawa, Jonas Mkude, Francis Kahata/Hassan Dilunga,  Gerson Fraga,  John Bocco/Meddie Kagere, Clatous Chama na Luís Miquissone .

Hiko ndicho kikosi cha kwanza ambacho huwa kinapata nafasi mara kwa mara.

Manara

Huku kikosi cha pili kikiwa na nyota kama Beno Kakolanya, Shamte, Gadiel Michael, Yusuph Mlipili,  Nyoni, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Ibrahim Ajib, Meddie Kagere, Hassan Dilunga, Miraji Athumani na Deo Kanda.

Katika vikosi hivyo viwili japo kuna baadhi  ya wachezaji huwa wanaingia kikosi cha kwanza kutokana na vita ya namba, kama umeangalia hapo Meddie Kagere baada ya corona hakuwa anapata nafasi.

Kikosi hiki cha pili ukimtoa Kakolanya kilipoteza magoli 3-2 ambapo kilionekana ni kikosi cha kawaida kabisa na huenda kama kingecheza na Namungo au Azam ambao wako vizuri zaidi yao wangefungwa nyingi.

Hii ina maana kuwa ndani ya Simba ‘rotation’ ya wachezaji sio ndefu sana na ndio maana huwezi kuwapa dhamana kikosi cha pili.

Angalia mchezo walioshinda magoli 5 dhidi ya Alliance kikosi cha kwanza kikichanganyika kidogo na kile cha pili.

Manara anaposema kikosi cha pili kikali kuliko cha kwanza hapa hakuna ukweli wowote.

Nachokubali kuwa kwa siasa za mchezo wa soka Manara yuko sahihi kabisa.

Ila uhalisia bado timu hiyo inahitajika ifanye kitu cha ziada kwa kikosi cha pili.

Ni kweli kikosi cha Simba kwa mechi za ligi kuu Bara kiko vizuri na hakuna mpinzani ila huko wanapoendea sasa ndio tutaweza kuona habari tofuati.

Kwa Simba hii yenye kikosi cha kwanza imara ila cha pili kikiwa hafifu kuna kazi kubwa sana ya kuweza kuwaambia Wana Simba  juu ya kauli za kuwa na vikosi viwili bora wakati huo hakuna ukweli.

Mimi ni miongoni mwa mashabiki wazuri wa Manara hasa kwa kauli zake za kishujaa pia hakuna ubishi kuwa yeye ndio msemaji bora Tanzania,  kwa kauli ya kusema Simba ina vikosi viwili bora wakati uhalisia hauko hivyo hapo ndipo nilipo mkataa ila mengine tunaenda sawa.

Kuna wakati furaha ikizidi wanasema usiongee kitu, pia ukiwa na hasira nako usifanye kitu chochote cha kutoa maamuzi.

Uzuri wa shabiki wa Tanzania huwa wanashika hii misemo ya wasemaji wao wakiamini kuwa ndio timu inaenda hivyo  itafika wakati watachoka kama hakuna uhalisia wa wakisemacho hapo sasa ndio atatafutwa mchawi.

Inapoelekea kimataifa Simba inatakiwa ijiangalie kwanza katika kikosi chake je wamejiimarisha ?

Manara aliwahi kusema kiweledi kabisa kuwa timu hiyo itasajili wachezaji  wanne katika dirisha la usjaili lijalo.

Hii inamanisha kuwa wanaenda kuziba nafasi ambazo hazikufanya vizuri msimu  huu.

Hapo sasa inatakiwa ichague mchezaji ambaye atakuja kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Hii itasaidia ule ukubwa wa kikosi unaozungunzwa uwe sahihi sasa, katika hao wanne tumeambiwa wawili wa ndani na wawili wa kimataifa.

Kazi kwao sasa kuchagua mchezaji gani anawafaa kwa ajiri ya kuunganisha nguvu kuelekea mechi za kimataifa.

Simba ile iliyoingia robo fainali ya michuano ya kombe la vilabu Afrika ina utofauti mkubwa nah ii licha ya kujaa mafundi wengi.

Utofauti uliopo ile ilipambana  sana kwa kujitolea ndio maana katika kipindi kile hata mtani wao wa jadi Yanga aliambulia sare tu katika mechi zote.

Hii ya sasa licha ya kuwa na mafundi inakosa ari ya kupambana na ndio kitu muhimu sana kwa timu.

Yanga mbovu ila kinachoisaidia timu hiyo kupambana kwa kujitolea,.

Hapa sasa utapata tafasiri ya Waswahili inayosema kuwa kipaji bila jitihada sawa na bure.

Inatakiwa katika wale watano wanaokaa benchi wawe na viwango sawa au kubaribia na wanaoanza.

Mfano Meddie Kagere ana kiwango sawa na John Bocco,  Kahata ana kiwango kinachofanana na Dilunga wengine pia wanatakiwa wawe hivyo.

Ukweli ni kwamba ubora wa Simba hatuwezi kuubeza lakini wachezaji wasilewe sifa na kuvimba vichwa vyao wakiamini kuwa akiumia Chama, Luis na Mkude kuna mwingine nje anaweza kufanya yale ya Jonas hilo wasahau kwanza.

Ninachoelewa kwa timu ya Simba baada ya mabadiliko sasa wanaangalia kujenga timu.

Wamefaulu kwa soka la bongo sasa safari ya kupambana na TP Mazembe, Al Ahly na Mamelodi Sundowns na nyingine kali.

Naamini usajili wanaoufanya weledi uliojawa na watu wanaojua mpira.

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

Leave a Reply

Exit mobile version