*Wazidi kupoteza mechi, Chelsea pia hoi
Mambo yamezidi kwenda harijojo kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England (EPL), Manchester United licha ya kuwa na mshambuliaji wao mahiri, Robin van Persie.
Man U ambao mechi iliyopita ya EPL walikanyagwa bao 1-0 na Liverpool, Jumamosi hii wameshindwa tena kulinda hadhi yao chini ya kocha David Moyes, kwa kuwaruhusu Newcastle United kuwazaba bao 1-0.
Yohan Cabaye ndiye aliwapa simanzi mashabiki lukuki kwenye dimba la Old Trafford kwa kufunga bao peke lililowatenganisha.
Kwa Newcastle ni zaidi ya ushindi, kwani ni mara ya kwanza tangu 1972 kushinda Old Trafford na kocha wa Man U, David Moyes amesema timu yake inahitaji mabao ili kujipa matumaini na kujiamini.
Katika mechi nyingine, vigogo Chelsea walikubali kicapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Stoke. Wafungaji wao walikuwa Peter Crouch, Stephen Ireland na Oussama Assaidi. Chelsea walipata mabao kupitia kwa Andre Schürrle lakini bahati mbaya hawakuweza kumaliza tofauti yao hiyo.
Katika mechi nyingine, Liverpool wamefanikiwa kuwasambaratisha West Ham kwa mabao 4-1.
Liverpool walionesha kiu ya ushindi dimbani ambapo hatimaye walifanikiwa kupata ushindi wao mnono.
Katika mechi nyingine, Manchester City na Southampton walikwenda sare ya 1-1, Crystal Palace wakawafunga Cardiff 2-0.
Sunderland waliloa mabao 2-1 kutota kwa Tottenham Hotspur lakini West Bromwich Albion walionesha maajabu kwa njia hasi baada ya kuruhusu Norwich wawatandike mabao 2-0.
Nafasi nne za juu kwenye EPL zinashikwa na Arsenal, Liverpool, Chelsea na Manchester City.