Menu
in , , ,

Man City wawapopoa Southampton

*Spurs wawazima Everton

Ligi Kuu ya England (EPL) imeendelea kwa mechi mbili kwa timu zenye ushindani mkubwa, ambapo Manchester City wamefanikiwa kuwashusha Southampton kutoka nafasi ya pili baada ya kuwatandika mabao 3-0.

Kipindi cha kwanza kilikuwa doro, ambapo hakuna bao lililopatikana, lakini baada ya nusu ya pili kaunza, walikuwa City waliocheka, wakiwasababishia Saints kichapo cha kwanza nyumbani kwao kwa msimu huu.

Pamoja na ushindi huo, City walipata pigo kwa beki wao mpya aliyesajiliwa kwa pauni milioni 32 kutoka Porto ya Ureno, Eliaquim Mangala kupewa kadi nyekundu. Tangu asajiliwe hajacheza vyema na inaelekea maisha ni magumu kwake hapa EPL.

Sergio Aguero naye, akicheza mechi ya 100 kwenye ligi hii alipewa kadi ya njano kwa bahati mbaya, mwamuzi akidhani alikuwa amejirusha, lakini yote hayo hayakuwazuia vijana wa Manuel Pellegrini kuondoka na ushindi mnono ugenini.

Mabao yalitiwa kimiani na viungo Yaya Toure, Frank Lampard na beki wa pembeni, Gael Clichy. City sasa wamepunguza pengo la pointi walizokuwa wakiongoza nazo Chelsea hadi sita.
 
SPURS WAWAZIDI NGUVU EVERTON

Tottenham Hotspur wamefanikiwa kutoka nyuma kwa bao 1-0 na kuwafunga Everton 2-1 kwenye mechi ngumu iliyochezwa nyumbani kwa Spurs, White Hart Lane.

Everton walifungua lango kwa bao la kiki kali ya Kevin Mirallas dakika ya 15 tu ya mchezo, lakini dakika sita baadaye Christian Eriksen akasawazisha kabla ya Roberto Soldado kupachika la ushindi, likiwa ni bao lake la kwanza msimu huu.

Kocha wa Everton, Roberto Martinez alisikitishwa kwa mwamuzi Michael Oliver kuwakatalia penati dakika za mwisho baada ya mchezaji wa Spurs kuunawa mpira ndani ya kasha la penati.

Chelsea wanabaki kileleni kwa pointi zao 33, wakifuatiwa na City, Southampton, Manchester United, West Ham, Arsenal na Spurs. Walio katika nafasi mbaya ni Queen Park Rangers na Burnley wenye pointi 11 wakati mkia unashikiliwa na Leicester wenye pointi 10.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version