Menu
in , , ,

Man City wawanyuka Liverpool

Liverpool wamepata kisago cha kwanza msimu huu, baada ya mabingwa watetezi kuwacharaza 3-1 kwenye mechi iliyopigwa Etihad Stadium usiku wa Jumatatu.

Stevan Jovetic alifunga mabao mawili katika mechi moja kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu ya England (EPL), kwenye mechi ambayo mshambuliaji mpya wa liverpool, Mario Balotelli alitazama wakiadhibiwa kutoka kwenye kizimba cha wakurugenzi. Alifunga dakika za 41 na 55.

Man City walicheza kawaida na kuelekea kuwazidi kirahisi Liverpool ambao msimu uliopita walishika nafasi ya pili. Hata hivyo, Liverpool walitawala zaidi kwenye kipindi cha kwanza pasipo kutengeneza nafasi za maana za kufunga mabao.

Liverpool walijaribu kurudi mchezoni baada ya kukandikwa mabao hayo mawili, lakini walizidi kulemewa baada ya Sergio Aguero kufinga bao sekunde 23 tu tangu alipoingia kuchukua nafasi ya Edin Dzeko katika dakika ya 69.

Washambuliaji wa Liverpool hawakuweza kufunga hata bao moja, kwani hata hilo la kufutia machozi lilifungwa na Pablo Zabaleta wa Man City akiwa ametiwa shinikizo na mshambuliaji wa Liverpool, Rickie Lambert alipokuwa katika harakati za kuokoa dakika ya 83.

Jovetic alisajiliwa msimu uliopita lakini hakuweza kung’ara kwa sababu msimu ulitawaliwa na majeraha na alifunga mabao matatu tu kwa Man City. Liverpool watamweka alama, kwa sababu mwaka 2009 aliwafunga mabao mawili pia kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, enzi hizo akiwa Fiorentina.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version