Timu kongwe ya Yanga ambayo msimu uliomalizika karibuni ilipoteza nafasi ya Ubingwa wa Tanzania bara, sasa inakabiliwa na mambo matatu makubwa ambayo yana uzito Mkubwa kwa time hii nguli.
Mambo hayo ni kupata kocha ,kupanga safu ya uongozi na kuunda kikosi imara cha wachezaji watakaorudisha heshima ya timu hiyo ambayo ilishika nafasi ya tatu katika msimu ulioipa ubingwa timu ya Simba.
Wachambuzi wa masuala ya soka wanasema kazi hizo mbili zinaweza kujenga timu imara ama kupata timu mbovu kama viongozi wenye fedha wanaoomba uongozi watashindwa.
Mpaka sasa wapenzi wa soka mashuhuri kadhaa walitajwa kutaka kuongoza Yanga nafasi ya Mwenyekiti, huku Mfadhili wake mkuu Manji naye akitajwa kutaka nafasi hiyo ama kupanga safu ya uongozi.
Waliotajwa kuombwa nafasi ya Mwenyekiti ni aliyekuwa Katibu wa TFF , Frederick Mwakalebela, Idd Kipingu, Kifukwe Francvis na Bin Kleb.
Wakati timu ikiihangaika kupanga safu ya uongozi, Katibu wa klabu hiyo, Celestine Mwesigwa amekuwa akihaha kutafuta wachezaji wa timu hiyo.
Karibu wiki mbili sasa wanachama na mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakitaja majina ya wachezaji wengi kuwasainisha fomu za usajili ingawa hayajadhibitishwa.
Wanaotajwa ni wachezaji mahiri wa Simba akiwamo Kelvin Yondani Emmaneul Okwi na hata Hassan Mgosi ambaye alikuwa timu ya Motema Pembe nchini DRC Congo.
Naye mwenyekiti kamati ya usajili anahangaika kusaka kocha wa timu pamoja na wachezaji imara.
Vyombo vya habari vimekuwa vikitaja kusakwa kwa mkocha Mfaransa huku vingine vikisema atarudishwa Mbraziri Maxcio Maximo ambaye alikuwa kocha wa Taifa Stars.
Lakini Yanga pia inadaiwa kukabiliwa na madeni ya makocha waliomaliza muda wake pamoja na baadhi ya wachezaji ambao wanaendelea kuidai..
Ni ukweli usiofichika kwamba Yanga sasa ina kazi ngumu zaidi kutetea ubingwa wake wa kombe la Kagame kwani inakabiliwa na mambo matatu ambayo yote ni muhimu.