MSIMU wa 2019/2020 utabaki kwenye kumbukumbu za mashabiki wa soka Tanzania pamoja na milioni ya raia wake baada ya kushuhudia kijana wao na nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta akifanikiwa kutimiza ndoto yake ya kucheza Ligi Kuu England. Samatta alinunuliwa na klabu ya Aston Villa chini ya kocha Dean Smith aliweka rekodi ya kiwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza Ligi Kuu England. Makala haya yanaeleza mambo 10 yaliyomkabili msimu huu.
PRESHA YA ASTON VILLA
Samatta alijiunga Asto Villa yenye presh kubwa mno. Timu kuwa na presha kubwa kipindi cha mwishoni kulitokana na kufanya vibaya hivyo kuhitaji suluhisho la haraka. Mpango ulikuwa kuinusuru timu isishuke daraja, hivyo presha ya Aston Villa ilikuwa ya juu zaidi huku maandalizi ya mipango yakiwa finyu. Presha ilisababisha Aston Villa waingie sokoni kwa plan A tu. Dean Smith akalazimika kuweka matumaini kwa Samatta lakini hakuwa amemwandalia majukumu kikosini. Kwahiyo presha ya kutoshuka daraja iliwafanya watumie
TIMU MPYA, MBINU MPYA
Samatta alikuwa mchezaji mpya katika timu mpya. Chini ya Dean Smith alikutana na mbinu mpya kutoka kwa wachezaji wapya ambao hafahamiani nao kimbinu.
Katika timu hakupewa muda wa kumudu kuzoea mazingira mapya. Samatta amecheza miezi mitatu Aston Villa. Hapo hapo Villa walimpoteza mchezaji wao muhimu Jonathan Kodjia aliyejiunga na Al-Gharafa ya Qatar. Halafu ujio wa Borja Baston kutoka Swansea City uliongeza idadi bila mafanikio.
‘WAGONJWA WENGI’
Villa ni timu iliyokutana na changamoto nyingi. Mojawapo ni kuwa na wachezaji wengi wagonjwa na kuharibu muunganiko wa timu nzima. Hata kama mchezaji mpya anaongezwa bado anahitaji huduma ya wachezaji waliofiti kiafya. Kila mchezaji angekuwa fiti kwa 100% tusingeona mapungufu mengi kama waliyonayo sasa.
MATARAJIO MAKUBWA
Matarajio makubwa ya mashabiki,makocha kuliko uhalisia. Samatta aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza Afrika mashariki kuchezea klabu ya Aston Villa. Sifa zingine za Samatta ni kuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Mfungaji bora wa Ligi Kuu Ubelgiji maarufu kama Jupter League na pia amewahi kuwa mchezaji bora wa Afrika akicheza Ligi za ndani wakati akikipiga katika klabu ya TP Mazembe. Kwa sasa Samatta ni mali ya Aston Villa, akiwa amemaliza miezi 6 kuitumikia klabu yake.
‘PRE SEASON’
Mipango mingi ya timu za Ulaya hufanyika wakati wa maandalizi ya msimu. Hapo benchi la ufundi wanahakikisha mipango na mikakati inaandaliwa vizuri ili Ligi Kuu ikianza iwe inatumika kutafutia ushindi. Hata hivyo Samatta hakuwa sehemu ya mipango ya Villa kwenye maandalizi ya msimu ni wazi anahitaji kujifunza upya klabuni hapo. Hakuwa sehemu ya maandalizi ya msimu uliopita.
UGONJWA WA CORONA
Januari mwaka huu 2020 Samatta alijiunga Aston Villa. Wakati anajiunga tayari kulishakuwa na dalili za hekaheka za mlipuko wa ugonjwa wa Corona. Mlipuko wa ugonjwa wa Corona uliingilia kati, hakuweza kuwa na muda wa kutosha kuzoeana na wenzake. Corona ilizuia kabisa mtiririko ambao ungeweza kumsaidia Samatta kuelewa falsafa ya Aston Villa. Ligi iliposimama ilisababisha kuvurigika kila kitu. Kama benchi la ufundi liliandaa program maalumu kwa ajili yake maana yake wasingweza kufanikisha kipindi cha Corona.
UBELGII vs ENGLAND
Tofauti za Ligi ya Ubelgiji na England ambayo ina ushindani mkubwa zaidi. Ligi aliyotoka Samatta haifanani kwa uwezo na EPL. Jupiter League na EPL ni tofauti sana kwa kuwa zimepishana mbali kiubora. Ndiyo maana katika mahojiano ya kwanza alipotua Astona Vilaa alisema kama kasi ya kazi aliyokuwa anaifanya Jupiter League basi inamlazimu kuongeza zaidi akiwa EPL.
WAPISHI KIDUCHU
Mbwana anahitaji kulishwa,kutengewa,yeye sio mtafitaji,weka kwenye njia apite nao, dondosha cross amalizie. Villa hawana uwezo huo na wanahitaji mabadiliko makubwa kama wanataka kufaidi kipaji cha samatta. Samatta ni amewahi kuwa mfungji bora wa Ubelgiji, mfungaji bora wa ligi ya mabingwa barani afrika
KUKOSA VIUNGO VISHETI
Uzalishaji wa eneo la kiungo ni hafifu. Nahodha wake Jack Grealish amekuwa mwingi wa kuharibu muvu za mchezo. Nafasi za mabao 357 zimetengenezwa lakini mabao hayaingia wavuni. Kwahiyo Villa wanalo tatizo kubwa la kutatua katika timu yao. Mahali pa kuanzia ni benchi la ufundi kisha kikosi chao. Hili limemnyima nafasi Samatta kuwa na mabao ya kutosha katika mechi chache alizocheza.
MAJUKUMU HAFIFU
Aston Villa haijampa Samatta majukumu ya kucheka na nyavu. Mfumo wa Aston Villa hauwafanyi wacheze kwa mtindo wa kumtegemea Samatta. Magoli yao mengi yanapitia kwa Jack Grealish. Tatizo lipo kwa timu sio mchezaji.
Villa wana mpira mgumu sana ule wa pasi mbili golini ambao hautaki ‘playmaker’ aupake rangi na kuremba kisha alete ubunifu wake. Goli nyingi alizofunga Samatta na staili yake anafaa kuwa mchezaji wa Southampton, Burnley au Newcastle ambazo zingekuwa mahala sahihi kwake. Mwisho wa siku ahakikishe haondoki EPL.
MAPITO YA WAKONGWE
Samatta sio mchezaji wa kwanza kukutana na changamoto EPL. Wapo mastaa waliokutana na wakati mgumu EPL. Samatta amepita njia ya akina Radamel Falcao, Juan Sebastian Veron, Andriy Chevchenko, Max Meyer, Marko Marin na wengine wengi zaidi.