RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi, amesemamisha uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba, mpaka itakapaundwa Kamati ya Maadili..
Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam jana Malinzi, alisema mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Simba hadi hapo klabu hiyo itakapounda Kamati ya Maadili ambayo itasikiliza masuala ya kimaadili kuelekea uchaguzi huo.
Malinzi alisema kwamba Simba inatakiwa kuwa imekwishaunda Kamati ya Maadili hadi kufika Juni 30, mwaka huu.
Alisema kwamba hatua hiyo imefua
tia TFF kupokea malalamiko mengi juu ya ukiukwaji wa maadili kwa baadhi ya wagombea na waachama wa klabu hiyo.
Malinzi alisema kwamba kwa mujibu wa Katiba ya TFF kifungu cha 50, Katiba ya Simba ibara ya 1(6) na kanuni za uchaguzi za TFF kifungu cha 1(2) inaagiza klabu ya Simba, ifuate hayo.
Alisema kuwa baada ya kuundwa kwa Kamati hiyo Maadili itasikiliza malalamiko yote ya kimaadili yanayougubika mchakato wa udhaguzi huo, ambao awali ulipangwa kufanyika Juni 29, mwaka huu.
Malinzi alisema kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa TFF Ibara ya 2 kifungu cha (4) kamati ya utendaji ya Simba, chini ya Mwenyeiiti wake, Ismail Rage itaendelea kuiongoza klabu hiyo hadi hapo mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.
Pia Malinzi amewataka wanachama wa klabu ya Simba, kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho TFF inataka ijihakikishie haki inatendeka katika kuelekea uchaguzi wa klabu hiyo.
Katika hatua nyingine Malinzi alisema ameuwa akisikia tuhuma dhidi yake kuwa anamtetea Wambura, ili aingie madarakani, ambapo alisema si kweli.
Alisema kuwa hata kwenye uchaguzi wa TFF ambao yeye aliingia madarakani Wambura, hakuwa meneja wake kama inavyozungumzwa.
“Nimepata habari za kuwa Wambura alikuwa meneja wangu ukweli ni kwamba nimesikitishwa sana, mimi sikuwa na meneja hata mmoja, hivyo tuhuma hizo dhidi yangu sio kweli”alisema Malinzi.
Alisema wakati mchakato wa uchaguzi wa Simba, ukianza yeye aliwaita Kamati ya Uchaguzi ya Simba pamoja na ya TFF, na kuzungumza nao, lakini iikiwa si kwa nia mbaya.
Malinzi ametangaza kusimamisha uchaguzi huo huku zikiwa zimebaki wiki mbili tu, kabla ya uchaguzi huo.
Hatua ya Malinzi imekuja wakati tayari zoezi la mwisho la Kamati ya maadili kukaa likiwa limebakisha siku moja ya kukaa, ambapo kwa mujibu wa vyonzo maalum ilikuwa ikitane kesho Jumanne.
mwisho