Droo ya hatua ya makundi ya kombe la shirikisho pamoja na ligi ya mabingwa Afrika imefanyika hii leo huku kwa Tanzania ikiwa na wawakilishi wawili ambao kwa upande wa Ligi ya mabingwa Afrika akiwa ni Yanga huku kwa upande wa kombe la shirikisho mwakilishi akiwa ni Simba.
Msimu wa mwaka huu katika makundi ya kombe la shirikisho la Afrika kumekua na msisimko mkubwa zaidi baada ya vigogo wa Tunisia CS Sfaxien, Enyimba wa Nigeria, Simba ya Tanzania na Bravos do Maquis wa Angola kupangwa kundi moja ambapo ni kundi D.
Mabingwa watetezi Zamalek ya Misri wamepewa kundi gumu ambapo watakabiliana na vigogo wa Ivory Coast ASEC Mimomas katika Kundi B.
Kundi A lina mabingwa wa zamani USM Alger ya Algeria ambao watacheza dhidi ya Stade Malien kutoka Mali, ASC Jaraaf ya Senegal, na Stellenbosch ya Afrika Kusini ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza katika michuano ya kombe la shirikisho la Afrika
Hatua ya makundi itaanza kuchezwa Novemba ambapo ndio njia ya klabu kadhaa kuonesha ubabe waokatika soka la Afrika.
Hapa chini ni makundi jinsi yalivyo katika kombe la shirikisho la Afrika
Kundi A: USM Alger, Stade Malien, ASC Jaraaf, Stellenbosch
Kundi B: Zamalek SC, ASEC Mimosas, Black Bulls, Orapa United
Kundi C: RS Berkane, Al Masry, CD Lundal Sul, CS Constantine
Kundi D: Simba SC, CS Sfaxien, Enyimba FC, FC Bravos do Maquis
Kwa upande wa ligi ya mabingwa Afrika ambapo kwa Tanzania inawakilishwa na Yanga ama ukipenda unaweza kuwaita wananchi watakutana na upunzani mkali kutoka kwa klabu kama TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bila kusahau AL Hilal Omdurman ya Sudan pamoja na MC Alger ya Algeria.
Bingwa mtetezi wa michuano hii klabu ya Al Ahly wamepangwa kundi C ambapo watacheza na CR Belouizadad ya Algeria lakini pia watacheza na Orlando Pirates ya Afrika Kusini pamoja na Stade d’Abidjan ya Ivory Coast.
Makundi kwa upande wa ligi ya mabingwa Afrika yapo katika muundo huu
Kundi A: TP Mazembe, Young Africans, Al Hilal , MC Alger
Kundi B : Mamelodi Sundowns, Raja AC, ASFAR ,Maniema Union
Kundi C: Al Ahly , CR Belouizadad , Orlando Pirates , Stade d’Abidjan
Kundi D: Esperance, Pyramids FC ,Sagrada Esperança , Djoliba
ReplyForward |