Kuthibitishwa habari za kufukuzwa Ole Gunnar Solskjaer ni tangazo la kwamba nafasi ya kazi ipo Old Traford. Na sasa Manchester United wapo katika msako wa kocha mpya ambaye atakiongoza kikosi hicho katika mafanikio zaidi. Tangu aondoke gwiji wao Sir Alex Ferguson hakuna kocha aliyeleta mafanikio klabuni hapo, na wengi wao wanaishi kufukuzwa. Hata hivyo sifa ya Man United ni kuwavumilia zaidi makocha wake.
Kwa namna ambavyo Ole alivyoboronga ilitarajiwa angefukuzwa mapema sana, lakini badala yake akaongezewa mkataba wa kubaki klabuni hapo. Muda aliopewa na kile kilichotokea ni vitu viwili tofauti, ambavyo vinawafanya mashabiki wawe na hasira na kuona waziwazi kocha wao huyo hakuwa na umahiri kuinoa klabu hiyo. Kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Watford kilihitimisha kibarua cha kocha Ole Gunnar Solskjaer ambapo s asa wapo makocha watano wanaowindwa na mabosi wa Man United ili wakubali ofa za kuinoa timu hiyo.
ZINEDINE ZIDANE
Ni raia wa Ufaransa. Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid hana kibarua tanu Mei mwaka huu alipojiuzulu nafasi ya ukocha kwa mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi ya Mbaingwa Ulaya na La Liga. Zidane anahusishwa na Man United kwa sababu anazo sifa kubwa ambazo zinahitajika Old Traford. Mafanikio yake akiwa Real Madrid ndiyo yanawavutia mabosi wa Man United.
Ametwaa mataji mawili ya La Liga, mawili Supercopa de Espana, mawili ya UEFA Super cup na mawili ya klabu bingwa dunia. na zaidi anametaa mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwahiyo ni kocha mwenye uzoefu wa mashindano mbalimbali barani ulaya kuanzia ligi za ndani hadi kimataifa. Taarifa zaidi zinasema uwezekano wa kumpa Zidane ni mdogo kwa sababu hana mpango huo kwa sasa na familia yake inatajwa kuweka ngumu kuishi England.
BRENDAN RODGERS
Huyu ni raia wa Ireland kaskazini ambaye kwa sasa anaifundisha Leicester City, na amewahi kuzinoa timu za Swansea City,Liverpool na Celtic. Anapendwa na mashabiki na wachezaji wengi kutokana na kazi yake, na ameiongoza Leicester kutwaa mataji mawili ya Ngao ya Hisani na FA. Pia alikiongoza kikosi hicho msimu uliopita kumaliza Ligi ikiwa nafasi ya tano ambayo iliwawezesha kushiriki michuano ya Europa League. Uwezekano wa kumpata kocha huyo ni mkubwa ikiwa mabosi wa Man United watalipa gharama za kuvunja mkataba wake na Leicester.
MICHAEL CARRICK
Nyota huyu wa zamani naye ni miongoni mwa wanaotajw akuchukua nafasi ya ukocha Man United. Kwa sasa anapewa jukumu la kukiongoza kikosi hicho kwa muda hadi pale atakapotangazwa kocha mkuu. Kiungo huyo atakuwa na kibarua cha kuongoza Man United katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Villareal. Kama Carrick atapata matokeo mazuri huenda akafikiriwa kuchukua mkataba wa kudumu wa kuinoa Manchester United. Kwakuwa anaifahamu kalbu hiyo na akiwa kocha msaidizi inampa nafasi ya kurithi mikoba ya Ole Gunnar.
ERIK TEN HAG
Kocha huyo wa Ajax Amsterdam naye amekuwa miongoni mwa wanaohusishwa na kibarua cha kuinoa Man United. Hag amekuwa kocha wa Ajaz tangu mwaka 2017, akisifika kufundisha soka la burudani na ushindi ambalo limempa mataji mawili ya Ligi Kuu Uholanzi, pamoja na kukiongoza kikosi hicho hadi nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita. Kumshawishi kocha huyu si suala dogo kwa sababu presha za Ajax na Man United zinatofautiana. Akiwa ametulia Ajax na kutengeneza falsafa yake iliyohitaji muda hadi kuleta mafanikio, haifahamiki kama mabosi wa Man United watamvulia hadi kuunda falsafa yake Olkd Traford na changamoto ya kufanya kazi na wachezaji wakubwa.
LAURENT BLANC
Mfaransa huyu amewahi kuwa kuichezea Man United mwaka 2003. Alikuwa beki mahiri wakati akicheza soka. amewahi kumkochi Edinson Cavani alipokuwa kocha wa PSG ambako walitwaa mataji matatu ya Ligi Kuu Ufaransa. Kwa sasa anafanya kazi kama kocha wa Al Rayyan nchini Qatar. Blanc amewahi kuiongoza klabu ya Bordeaux kutwaa taji la Ligi Kuu Ufaransa mwaka 2009 na alikuwa kocha wa timu ya taifa baada ya fainali za Kombe la dunia mwaka 2010.
MAURICIO POCHETTINO
Ni miongoni mwa makocha wanaotawa kuwa tayari kuchukua kibarua cha Man United. Pochettino kwa sasa ni kocha wa PSG, lakini anahusishwa na kibarua hicho kwa sababu familia yake yote iko jijini London, wakati yeye akiwa Paris. Ana uwezo wa kuwaongoza wachezaji wakubwa kwa sasa ambako yuko na Lionel Messi, Neymar,Kylian Mbappe na wengineo ndani ya PSG hivyo huenda kawa mtu sahihi kupokea jahazi la Man United.