ILE timu iliyonolewa na makocha wenye majina makubwa kama vile Gianluca Vialli,Gianfranco Zola, Jose Mourinho, Felipe Scolari imekabiliwa na hali mbaya ya matokeo kwa msimu mzima wa 2022/2023. Kudidimia kwa Chelsea kulianza pale serikali ilipoamua kumtimua Bilionea Roman Abramovich aliyekuwa akimilikiwa timu hiyo. Chelsea iliporomoka kwa kasi, ilizuiwa kusajili, matokeo uwanjani nayo yakagoma kuleta furaha.
Lakini Chelsea hiyo hiyo ikawa imeuzwa kwa wamiliki wengine na sasa imesajili wachezaji kuluki katika dirisha dogo la mwezi Januari baad aya vibopa wapya kulipa madeni ya timu hiyo. Kutoelewana kati ya wamiliki na kocha Thomas Tuchel ilibidi pande hizo zisambaratike kila mmoja kushika njia yake. Graham Potter akapewa timu ya Chelsea ili kuleta matokea chache. Hata hivyo hakufanikiwa, akatimuliwa na kurudishwa Frank Lampard ambaye naye amewahi kufukuzwa kazi hapo hapo. Je ni mambo gani ambayo yanaikabili Chelsea wakati ambao imeajiri kocha mpya?
Ari ya timu kuwa chini ya kiwnago
Moja ya sababua mabyo inatakiwa kutolewa majibu ni kwanini Chelsea imeshuka kiwango na ari yake kuporomoka kwa kasi kubwa. Kocha wa muda mfupi Frank Lampard wakati akiondoka kibaruani alibainisha Chelsea inakabiliwa na tatizo la kushuka ari kila idata uwanjani. Lampard alisema kila kitu kipo chini, na haionekani kama kinawezesha kurudishwa kwa urahisi. Lampard alisisitiza kuwa kazi ya kwanza kocha mpya wa Mauricio Pochettino ni kuinua ari na viwango vya timu hiyo. Akizungumza kwa masikito Lampard alisema ameshangazwa na hali ya kushuka ari lakini anaamini inawezekana kurudishwa.
Safu ya ulinzi ina utata
Chelsea walifungwa mabao kwa urahisi. Timu yao ikaruhusu mabao mengi kiasi kwamba iliwawia vigumu kulinda lango lao. Wangeweza kufunga mabao lakini safu ulinzi ingeweza kukutana na changamoto hivyo kushindwa kustahimili. Beki kisiki wa kati Thiago Silva ana umri wa miaka 39 sasa, na bila shaka umri unamtupa mkono. Kinacholinda uchezaji wake ni mifumo ya kisasa ambayo wachezaji wanatumikia zaidi mifumo iliyopangwa kuliko kuruhusu vipaji binafsi kuongoza mifumo hiyo. Thiago Silva bado ameonesha shauku kubaki klabuni hapo, lakini wamiliki wanaonekana kukubaliana na kocha mpya kuwa baadhi ya wachezaji lazima waondolowe.
Mbali ya Thiago Silva, Chelsea wanaye kinda Challobah ambaye ameonekana kuimarika lakini msimu mbaya wa klabu hiyo ikaonekana kama vile timu imemfelisha kwa kiasi kikubwa. Safu hiyo pia ina mlinzi mkongwe Azplicuetta ambaye kwa kiasi kikubwa anaelekea ukingoni mwa uchezaji wake. Kubaki klabuni hapo itategemea uamuzi wa Pochettino. Je nini atakachokifanya kocha huyo? Atabaki na vijana wapya waliosajiliwa Januari mfano Fofana?
Viungo wa sasa ni nyanya
Safu ya kiungo cha Chelsea misimu ya karibuni ilikuwa ikimtegemea zaidi Ngolo Kante na Mateo Kovacic na Jorginho. Hata hivyo msimu uliopita Jorginho aliuzwa kwenda Arsenal, wakabaki Kante na Kovacic. Hata hivyo huenda msimu mpya ukashuhudia nyota hao wawili wakakosekana kikosini. Manchester City inahusishwa na kumsajili kiungo Mateo Kovacic huku Ngolo Kante akidaiwa kukubali dili la kuhamia Ligi Kuu Saudia Arabi ambayo ni maarufu kwa jina la Saudi Pro League.
Pochettino anakabiliwa na kibarua cha kuijenga safu ya kiungo wa ulinzi na ushambuliaji ambako kuna hatari timu yake ikazidi kuwa nyanya zaidi ikiwa injini ya timu haitaimarishwa. Ule umahiri wa akina Claude Makelele, Michael Essien na wengineo umeyeyuka kabisa katika safu hiyo. Pochettino wakati wa uchezaji wa soka alikuwa kiungo, hivyo anafahamu umuhimu wa injini ya timu ikiwa laini au ngangari. Je ni nani watakuwa injini ya timu?
Mawinga hatari bila matokeo chanya
Pulisic ni mojawapo ya viungo wa pembeni ambao wana vipaji vikubwa. Ni mchezaji ambaye anaweza kucheza nafasi ya winga wa kulia au kushoto. Hii ina maana mawinga wawili Mudryk na Pulisic wanaweza kuwa silaha muhimu ya Chelsea katika msimu ujao. Tatizo lililopo ni kwamba Pulisic anaweza kucheza mechi tatu vizuri lakini atakosekana zingine tatu kwa kuugua.
Kimisngi usajili wa Mudryk ulikuwa bora na muhimu kwa maendeleo ya Chelsea, lakini kilichotokea ni kwamba hakuwa na mchango mkubwa chanya wa timu hiyo. Pili hakuwa mchezaji tegemeo ndani ya kikosi cha Graham Potter wala Frank Lampard. Hali kadhalika Chelsea wanaelekea kumkosa Mason Mount ambaye mawinga wawili hao ni tishio kwa nafasi yake. Iwapo Mason Mountu atajiunga Chelsea au Manchester United maana yake kocha mpya Pochettino ameruhusu nyota huyo kuondoka ili kupata nafasi ya kujenga timu mpya.
Ni nani Didier Drogba mpya?
Chelsea wana safu finyu ya ushambuliaji. Mbali ya Kai Havertz, walikuwa na Joao Felix ambaye amepewa ruhusa ya kuondoka klabu hapo. Inashangaza Chelsea kutomsajili jumla Joao Felix lakini huenda kocha wao Pochettino anao mpango wa pili wa kuleta mshambuliaji mpya au kukisuka kikosi chake kwa namna nyingine. Kimsingi Chelsea ya sasa inakabiliwa na uhaba wa washambuliaji.
Haijapata mshambuliaji kariba ya nyota wao wa zamani Didier Drogba. Hii si Chelsea iliyokuwa inatamba na nyota kama Mateja Kezman, kwa sasa imebaki kuwa na washambuliaji ambao hawana matokeo chanya kwa timu. Pochettino atakuja na njia gani mbadala ya kuifanya Chelsea ipachike mabao ya kutosha na kuondoka kwenye jinamizi ambalo limewafaya msimu ulioisha kukosa hata nafasi ya kushiriki mashindao ya Ligi ya Mabingwa au Europa League?
Nani kuwa kipa namba moja?
Mjadala mwingine unaomkabili Pochettino ni kuamua nani atakuwa golikipa nambari moja wa Chelsea kwa msimu ujao? Chelsea wana makipa mawili wenye viwango vya juu, Eduardo Mendy raia wa Senegal na Kepa raia wa Hispania. Mara kadhaa kumekuwa na kubadilishana nafasi hizo. Awali Kepa alikuwa namba moja lakini makosa ya mara kwa mara na kushuka kiwango yalisababisha Frank Lampard alipokuwa kocha mkuu kumsajili Eduardo Mendy.
Tangu kuwasili kwa Eduardo Mendy hali ya mambo ilibadilika. Lakini Mendy naye amepata kufanya makosa kadhaa ambayo yaliyozua hofu. Hata hivyo kuumia kwa Mendy kukamrudisha Kepa langoni ambako ameonesha umahiri mkubwa hadi kumalizika kwa msimu licha ya matokeo mabaya waliyokuwa nayo timu hiyo. Sasa ni nani ataanza kikosi cha kwanza cha Pochettino kati ya Kepa na Mendy? Nalo ni jukumu lingine ya Mauricio.