Huwezi izungumzia Everton ukaacha kumtaja Lukaku, huyu ndiye nembo ya
timu ya Everton kwa sasa, yupo katika kiwango bora àmbacho hajawahi
kuwa nacho katika maisha yake ya soka. Katika mechi sita zilizopita
kafunga goli 9 na ndiye anayeongoza kwenye orodha ya ufungaji bora
akiwa na goli 21. Ni aibu kutokusema kuwa ni mshambuliaji bora kwa
sasa na anaenda kukutana na moja ya safu dhaifu ya ulinzi.
Safu ya Ulinzi ya Liverpool imekuwa haiko imara msimu huu na moja ya
magoli ambayo wamekuwa wakifungwa sana msimu huu ni magoli ya vichwa
yanayotokana na krosi au kona, pia magoli ya mashambulizï ya moja kwa
moja.
Lukaku kwa kushirikiana na Kevin Mirallas na Ross Barkley watakuwa na
madhara katika maeneo hayo na ukizingatia safu ya ulinzi ya Liverpool
haiko dhabiti inaweza ikawa na madhara makubwa kwao.
Upweke wa kumkosa Henderson bado haujawatoka, wamekuwa na kipindi
kigumu cha bila huyu bwana, Léo hii wanamkosa tena Adam Lallana. Ni
pengo kubwa kwa Liverpool kwa sababu Adam lallana amekuwa akihusika
kwa kiasi kikubwa katika mijongeo mingi ya timu ya Liverpool ambayo
imekuwa ikisababisha magoli ,pamoja na kuhusika kwenye ufungaji wa
magoli pia amekuwa akitoa pasi za mwisho za magoli kwa kiasi kikubwa.
Mechi za timu za Taifa zilizokuwa zinachezwa wiki hii zilionesha bado
Simon Mignolet anafanya makosa mengi yanayoigharimu timu, kitu hiki
anatakiwa kuwa nacho makini kwani Everton wana mshambuliaji ambaye
hutakiwi kufanya makosa mengi binafsi mbele yake.
Wakati michezo ya kimataifa inayohusisha timu za taifa ikituonesha
makosa mengi binafs ya Simon Mignolet kwa Liverpool, Everton wamepata
pigo kubwa kwa Seamus Coleman ambaye amepata majeraha ya muda mrefu,
Morgan Holgate ana nafasi kubwa ya kuziba pengo lake lakini kutokana
na umri wake mdogo unaweza ukawa kikwazo kwake yeye kupambana na kina
Phillipe Countinho.
Ni mechi ambayo inamwihitaji Philippe Countinho awe katika kiwango
bora ili aweze kuibeba Liverpool. Kasi ya kina Firminoo ,Mane na
Countinho itakuwa kikwazo kikubwa kwa kina Jagelka na Williams.
Emre Can na Idrissa Gueye Gana ndiyo watu pekee ambao wataamua mechi
ya leo kwa sababu kupitia kwao, mmoja wao ambaye atakuwa na uwezo
mkubwa wa kutembeza mipira kwa kasi ndiye atakayesababisha timu yake
kuwa na asilimia kubwa ya ushindi.
Emre Can akifanikiwa kucheza mipira ya kasi kwenda mbele itamsababisha
Georgino Wijnaldum kuwa na uwezo mkubwa wa kusukuma mashabulizi kwa
kina Philippe Countinho, Saido Mane na Firminoo.
Vivyo hivo kwa Gana ambaye yeye pamoja Tom Davies wanatakiwa kufanya
kasi ya kina Kevin Mirallas na Ross Barkley ionekane na faida ndani
yake