Menu
in , , ,

MAENEO MUHIMU KWENYE MECHI YA SIMBA NA YANGA

Tanzania Sports

Homa ya pambano la watani wa jadi inazidi kupanda kwelikweli. Zikiwa zimebaki siku mbili tuu ili mtanange huu upigwe huku timu zote zikiweka kambi Morogoro zikijiandaa na mchezo huo.

Kandandacotz inakuletea “battle” kali zitakazotokea katika uwanja wa Taifa Dar es salaam endapo walimu wa pande zote mbili hawatobadili sana vikosi vyao:

John Bocco vs Andrew Vicent “Dante”

Mpaka sasa John Bocco ana magoli 14 katika VPL akishika nafasi ya pili katika chati ya ufungaji. Andrew Vicent akiwa amerudi kutoka katika majeraha na akiwa kamili.

Katika mchezo huo huenda beki kisiki Andrew Vicent akapewa kazi maalum ya kumdhibiti mshambuliaji John Bocco ambae ataanza katika safu ya ushambilliaji wa SimbaSc.

John Bocco amekua akipewa mipira mirefu kutoka eneo la katikati ya uwanja lakini pia Andrew Vicent anasifika kwa kucheza mipira ya juu.

Obrey Chirwa vs Yusuph Mlipili

Chirwa mpaka sasa ana mabao 13 katika VPL na ndie kinara wa mabao katika klabu ya Yanga. Yusuph Mlipili kwa sasa amekua akiaminiwa katika safu ya ulinzi ya Simba na akiwa katika kiwango kizuri.

Chirwa anasifika kwa soka la nguvu na spidi akiwa analielekea lango lá mpinzani. Lakini pia atakutana na mlinzii Yusuph Mlipili anaependa kucheza kibabe na kutumia nguvu nyingi akiwa analinda lango lake.

Wawili hao kutokana na aina ya mchezo wanaocheza haitoshangaza kwa mmoja wao au wote wawili kuonywa au kuonyeshwa kadi na mwamuzi katika mchezo.

Emmanuel Okwi vs Kelvin Yondani

Kinara wa mabao wa VPL akiwa na mabao 19 anakwenda kukutana na beki kisiki katika VPL.

Emmanuel Okwi anasifika kwa uwezo wake wa kuweka kambani lakini pia uwezo wake mkubwa katika kucheza mechi kubwa kama hizi. Kelvin Yondani ndie beki bora mpaka sasa katika VPL huku akiwa na uwezo wa kuwadhibiti washambuliaji wasumbufu kama Okwi.

Katika mpambano wa wawili hawa huenda ndio ukaamua mchezo huo. Uiamara wa kila mmoja na kucheza vizuri ndivyo vitapa faida timu yake na kuweza kupata ushindi.

Ibrahim Ajib vs Shomari Kapombe

“Ibra Cadabra” fundi wa mpira kipemzi cha Wanayanga anaeunda safu ya ushambilliaji ya Yanga akisaidiana na Chirwa. Anakwenda kukutana na Shomari Kapombe alie kwenye form ya hali ya juu baada ya kutoka kwenye majeraha.

Wote wawili wamekua wakisifika kwa soka la kutumia akili na uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani. Kwa mfumo wa Simba Shomari Kapombe huenda akatumika kama wing-back wa upande wa kulia, huku kwa upande wa Yanga Ajibu akitumika kama mshambuliaji wa pembeni akitokea winga ya kushoto.

Kwa aina ya uchezaji wa wote wawili uwanjani upande wa kulia wa Simba na kushoto wa Yanga utakua na burudani kubwa siku ya tarehe 29!

Jonas Mkude vs Papy Tshishimbi

Moja ya maeneo yanayotegemewa kuamua mechi siku ya April 29 ni katikati ya uwanja. Huku Jonas Mkude kule Papy Tshishimbi.

Wote wanasifika kwa uwezo wao wa kupiga pasi, kucontrol mchezo, kutumia nguvu na akili wawapo uwanjani. Kitu pekee kitakachowatofautisha siku hiyo ni pacha watakaopangwa nao katika mchezo huo.

Kwa Yanga huenda Papy akacheza na Kamusoko au Said Makapu hivyo itategemea uwiano wa uchezaji wao katika eneo la kiungo.

Kwa upande wa Simba Jonas Mkude amekua akifurahia zaidi kucheza na Said Ndemla katika mechi za watani. Lakini siku hiyo huenda akaanza katikati na Mdhamiru Yasin au hata Shomari Kapombe pia.

Atakaeshinda vita katika eneo hili huenda akawa mshindi wa mchezo huu.

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya martinkiyumbi@gmail.com

Exit mobile version