Menu
in

MAENEO MANNE YANAYOISUMBUA LIVERPOOL

Tanzania Sports

Liverpool players are left dejected after they let slip a three-goal lead with Sevilla equalising in added time.

Jana kulikuwa na mechi za klabu Bingwa barani ulaya katika miji mbalimbali barani ulaya.

Moja ya mechi ambayo ilichezwa jana ni ya Sevilla dhidi ya Liverpool.

Mechi ambayo ilienda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa magoli 3, lakini baada ya kuingia kipindi cha pili walisawazishiwa magoli yote matatu.

Liverpool imekuwa timu ambayo haina mwendelezo mzuri wa matokeo mazuri msimu huu.

Hii inasababishwa na nini mpaka Liverpool iwe timu ambayo haijaimarika kwa kiwango kikubwa?

*Ni kweli wanakosa golikipa imara na beki wa kati imara?*

Golikipa Simon Mignolet, amekuwa kipa ambaye akihusika kwenye saves nyingi sana kwenye mechi.

Pamoja na kufanya saves nyingi kwenye mechi lakini kuna baadhi ya mechi ambazo amekuwa akifanya makosa mengi binafsi.

Makosa haya Mara nyingi yamekuwa yakisababishwa na makosa mengi ya safu ya ulinzi.

Safu ya ulinzi ya Liverpool imekuwa chanzo kikubwa kwa golikipa Simon Mignolet kufanya makosa mengi ya binafsi.

Presha ambayo safu ya ulinzi imekuwa ikiruhusu katika eneo la nyuma limekuwa likipelekea Mignolet kufanya makosa binafsi.

Kwenye mpira timu inapokuwa inaruhusu presha kubwa katika eneo lao,inakuwa inakaribisha uwezekano mkubwa wa kufanya makosa mengi binafsi.

Ndicho kitu ambacho kinatokea kwa Liverpool.

Safu ya ulinzi ya Liverpool imekuwa ikiruhusu sana presha langoni mwao na inashindwa kupunguza presha hiyo.

Imekuwa ikifungwa magoli mengi ambayo yanatokana na mipira ya juu, kona na krosi ambazo zimekuwa zikija katika eneo lao.

Hata namna ambavyo wanavyojipanga Lovren na Matip wamekuwa wakijipanga vibaya kitu ambacho kinawapa nafasi kubwa wapinzani kuwapita kirahisi.

*Presha inayotokea kwenye safu ya ulinzi ya Liverpool inaanzia wapi?*

Liverpool kiasilia hawana kiungo mwenye asili ya kuzuia.

Ukiwaangalia Henderson , Can na Wijnaldum siyo wazuri kwa kiasi kikubwa linapokuja suala la kuzuia.

Henderson amekuwa kiungo mzuri ambaye anacommand timu kwenda mbele kwa pasi zake.

Pia Can ni box to box ambaye anatakiwa kutimiza majukumu yake nusu kwenye kushambulia na nusu kwenye kuzuia.

Wijnaldum amekuwa akitumia muda mwingi sana katika kusaidia mashambulizi mbele.

Hivo kwa picha hii inaonesha kabisa hakuna mtu sahihi katika eneo la kati ambaye atasaidia kukaba kwa nguvu kuanzia eneo la kati ili kupunguza mashambulizi na presha katika eneo la nyuma ya timu.

Pia ukiangalia viungo hawa watatu hawana ubunifu mkubwa sana katika eneo la kutengeza nafasi za magoli.

Mzigo huu huachiwa Countihno peke yake, hali ambayo inamfanya kuna wakati aelemewe kutoka na timu pinzani inapomkamia.

*Firmino anatosha kuwa mshambuliaji wa kati wa kutumainiwa?*

Amekuwa akicheza kama false 9, nafasi ambayo imekuwa ikiwapa nafasi kina Salah na Mane kuhusika kwenye magoli.

Ingawa Mane na Salah kiasili ni wafungaji wazuri pia.

Ukiangalia takwimu , Firmino hafungi sana kama inavyotakiwa kwa mshambuliaji wa kati kufunga.

Hivo kama wataweza kupata mshambuliaji mmoja ambaye anauwezo mkubwa wa kufunga.

Magoli ya Salah na Mane yakiungana na magoli ya mshambuaji wa kati mwenye uwezo mkubwa wa kufunga inaweza kuwasaidia sana Liverpool.

*Ukosefu wa viongozi wengi ndani ya timu inaweza ikawa moja ya tatizo linalowakabiri Liverpool?*

Kuna wakati Liverpool ishawahi kuwa na Steven Gerrad, Dirk Kuyt, Jammie Carragher, Xavi Alonso, Pepe Reina, Riise Mascherano.

Wote hawa kwa pamoja walikuwa viongozi kiasili.

Kitu ambacho kilikuwa kinawasaidia sana kuhamasishana kipindi ambacho timu ikiwa imekata tamaa, nguvu ya kupigana ikiwa imepungua.

Hata kama timu ikiwa nyuma ya goli tatu watu hawa walikuwa wanahamasisha wenzao kupigana sana.

Hali imekuwa tofauti sana, Liverpool imekuwa timu ambayo inasawazishiwa goli 3.

Na timu kuwahi kushuka morali ya kupigana kwenye mchezo.

Hii ni kutokana na kuwa na idadi chache ya wachezaji ambao ni viongozi kulinganisha na kipindi cha nyuma.

mail to martinkiyumbi@gmail.com

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya martinkiyumbi@gmail.com

Exit mobile version