Hali ya hewa imechafuka katika Klabu Bingwa ya Soka Hispania – Barcelona, baada ya wajumbe sita wa bodi ya wakurugenzi kujiuzulu, wakipingana na Rais Jose Maria Bartomeru.
Wajumbe hao wanasema kwamba wamekasirishwa na jinsi klabu inavyoendeshwa, wakisaini barua na kutoa ujumbe wa pamoja. Wamesikitishwa na usimamizi wa masuala ya fedha hasa wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu.
Wanasema kwamba athari za virusi hivyo na masuala ya fedha klabuni ni hasi kwa sababu ya uongozi mbovu wa Rais Bartomeru. Vinara hao pia wanapinga jinsi kashfa iliyotokea Februari ilivyoshughuliwa, ambapo klabu ililazimika kukanusha taarifa kwamba waliajiri kampuni kwa ajili ya kushambulia wachezaji wao wenyewe kwenye mitandao ya jamii.
Sasa wanamtaka Rais Bartomeru kuitisha uchaguzi ili wachague mtu mwingine kwenye nafasi hiyo ya urais. Walioachia ngazi na kurusha ‘makombora’ kwa rais ni makamu wawili war ais, Emili Rousaud naEnrique Tombas. Wamebaki makamu wengine wawili. Wengine walioondokan ni wakurugenzi wane: Silvio Elias, Josep Pont, Jordi Calsamiglia na Maria Teixidor.
“Tumefikia uamuzi na hatua hii kwa sababu hatuwezi kubadili au kutengua namna klabu inavyosimamiwa wakati huu wa changamoto kubwa na wala kwa wakati ujao, hasa baada ya janga hili la virusi vya corona na athari zake,’ wakasema wakurugenzi hao sita kwenye barua yao.
Wakasema pia kwamba wanataka kuonesha kutoridhishwa kwao na kashfa iliyotokea na kwenda kana kwamba ni mchezo wa kuigiza, ambapo Bartomeru anadaiwa kuajiri watu ambao pamoja na mambo mengine, walitakiwa kumshambulia nyota wao, Lionel Messi kwenye mitandao ya jamii.
Watu hao, wandaiwa, walikuwa walihusika na kile kilichoitwa’Barcagate’, kashfa iliyokuwa siri lakini ikaja kufichuliwa na vyombo vikubwa vya habari na klabu ikajumuishwa kana kwamba bodi ndiyo ilitoa uamuzi na kuchukua hatua hiyo.
“Likuwa ni tukio letu la mwisho kwa utumishi katika klabu hii, tunapendekeza kuitishwa uchaguzi mpya haraka iwezekanavyo na kadiri mazingira yatakavyoruhusu ili kwamba klabu iweze kuongozwa katika njia bora kabisa na kushughulikia changamoto muhimu mapema ili kuijenga klabu kwa mambo ya baadaye,” wakasema wakurugenzi hao.
Wachezaji wa Barcelona watakatwa asilimia 70 ya mishahara yao wakati huu wa janga la virusi vya corona na kutakiwa pia kutoa michango mingine ili kuhakikisha kwamba wafanyakazi wengine ambao si wachezaji hawapotezi kazi na wanasonga mbele na maisha. Hao hulipwa kima kidogo cha mishahara kulinganisha na wachezaji.
Wakurugenzi wa bodi ya klabu hiyo kubwa Ulaya, waandamizi kwenye timu zao na wengi miongoni mwa wana timu ya kikapu wamekubali kupunguzwa mishahara yao wakati huu mgumu.
Pamekuwapo sintofahamu na utata kwenye mitandao ya jamii juu ya ‘Barcaget’ ambapo mmoja wa wakurugenzi walio karibu na Rais Bartomeru – Eric Abidal – amepata kuchangia humo, akitoa maoni ya kushambulia wachezaji waandamizi kama Messi, akidai kwamba wamekuwa hasi katika kukubali kukatwa mishahara wakati huu wa matatizo.
Messi na washirika wake wameonesha hasira juu ya uamuzi wa Rais Bartomeru wa kukata kwa kiasi kikubwa mishahara yao bila mashauriano ya wazi.
Wakati huo huo, Messi amekanusha madai kwamba ana mpango wa kuihama klabu hiyo na kujiunga a Inter Milan wa Italia. Katika maelezo yake aliyotundika kwenye mtandao wa Instagram, Messi (32) raia wa Argentina ambaye ni mshambuliaji wa Timu ya Taifa pia, alisema habari hizo ni potofu