Menu
in

Luc Aymael kajinyima ajira mwenyewe

Kocha wa Yanga

Yanga wamemfuta kazi kocha mkuu wa timu hiyo kwa maneno ya kashfa aliyoyatoa baada ya mchezo wao dhidi ya Lipuli FC uliofanyika mkoani Iringa.

Kimsingi Aymael alijua kabisa kuwa angetimuliwa kazi licha ya kuongea maneno ya hovyo.

Alichokifanya yeye ni kujipalilia mkaa ili ubwabwa utoke na matandu.

Kitendo chake kinaashiria kabisa kuwa timu nyingi zitaogopa kumuajiri hivyo kajinyima mwenyewe ajira kwa maneno yake ya hovyo.

Kauli yake haina haja ya kuirejea maana itakuwa tunafanya makosa mengine katika kuwaeleza wananchi.

Ila alitajia kitu kama Nyani, Mbwana na kejeli nyingine kwa shabiki waYanga.

Ninachofurahi  Shirikisho la mchezo wa mpira Tanzania tayari imechukua hatua baada ya kashfa ya kocha huyo.

Taarifa ya TFF inasema kuwa tayari wameyachukua maelezo yake na kuripoti FIFA juu ya udhalimu wa kibaguzi alioufanya kocha huyu.

Hadi sasa Yanga na timu nyingine zitakuwa zinajua juu ya aina ya watu wanaotakiwa kufanya nao kazi katika timu zao.

Sio rahisi kumpima akili ila inawezkeana Eyamel ana tatizo la akili.

Lakini pia Yanga na viongozi wengine wa mpira wanaweza kuangalia rekodi mbalimbali za watu wanaotaka kuja kuwafanyia kazi.

Rekodi ya Eymael ilifahamika kabla hata hajafika kuwa hakuwahi kumaliza mkataba wa timu alizowahi kuzifundisha.

Kikubwa kinachotajwa ni ukorofi wa kocha huyo ndio sababu ya kushindwa kuendelea na kazi katika timu mbalimbali.

Kitendo chake cha kututukana licha ya mengine yana ukweli mfano viwanja haviko katika hali nzuri , labda kauli yake aliyoitumia kuwa wanatakiwa wacheze wanyama.

Labda Eymal angetuambia vitu tofuati na tusivyovijua ila vyote alivyoongea hakuna kipya alichoongeza yeye matusi.

Labda angejenga hoja ya msingi katika utetea maslahi yake sio kutoa maneno ya hovyo.

Kila mwanamichezo amechukia hii , ukitaka kujua kuwa Aymael kazingua na kaizingua Afrika kwa ujumla.

Aliyekuwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera aliweka wazi kuwa huyu kocha anatatizo la akili kwa kukosa busara katikamazungunzo yake.

Mwinyi Zahera ameibuka na kumchana Mbelgiji huyo kuwa sio kocha.

Eymael ameachishwa kazi kutokana na vitendo vyake vya kibaguzi pamoja na matamshi yasiyo ya kiuungwana ambayo aliyasambaza jana, Julai 26 baada ya kumaliza kusimamia mchezo wa ligi dhidi ya Lipuli na kushinda bao 1-0.

 Zahera amesema kuwa kwa mwenendo wa  Eymael ulivyokuwa hakuwa na maisha marefu ndani ya kikosi cha Yanga hata nje hawezi kudumu akipata timu.

“Aina ya makocha kama yule wa Yanga ambaye amefukuzwa ni miongoni mwa makocha ambao hawawezi kufanya kazi Ulaya kwani hakuwa na maneno mazuri kwa waandishi pamoja na vitendo vyake.

Tanzania Sports
Matamshi ya kibaguzi, yanayosemekana yametolewa na kocha wa Yanga

“Kwa kuwa amefukuzwa basi ni wazi kuwa akipata timu sehemu nyingine hawezi kudumu, ili uwe kocha mzuri ni lazima uwe na nidhamu katika kile unachoongea,” amesema.

Lakini amekosa stamala ya kubakisha maneno  maana hajui kesho yake.

Hajui kuwa huenda timu nyingine zinaweza kutaka huduma yake ila zikashindwa kutokana na kauli mbovu za kocha huyo zikamnyima ajira.

Ngoja tubakishe maneno tuone swala hili likifika FIFA watachukua hatua gani kwa chiba huyu wa Kibelgiji.

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

Leave a Reply

Exit mobile version