Menu
in , , ,

Liverpool wamtimua kocha

 

*Advocaat aachia ngazi

Liverpool wamemfukuza kocha wao, Brendan Rodgers baada ya kuwa Anfield kwa miaka mitatu unusu.

Kulikuwa na tetesi za nafasi ya kocha huyo kuwa katika hatihati na baada ya kwenda sare ya 1-1 na watani wao wa jadi, Everton Jumapili hii, wamiliki wameamua kuachana naye.

Rodgers, raia wa Ireland Kaskazini, alisema wiki jana kwamba kulikuwa na njama zilizokuwa zikisukwa na baadhi ya watu kwa ajili ya kuhakikisha anaondoka klabuni. Timu hiyo imeanza vibaya msimu huu na ule uliopita pia haikuwa vyema.

Matokeo ya Jumapili hii yamewaacha Liver katika nafasi ya 10, lakini taarifa zinasema kwamba uamuzi wa kuachana na kocha huyo ulishafanywa, lakini haukuwekwa wazi, kabla ya mechi hiyo.

“Japokuwa huu umekuwa uamuzi mgumu, tunaamini kwamba unatupa fursa nzuri zaidi kwa ajili ya kupata mafanikio uwanjani,” taarifa ya klabu imesema.

Kuna tetesi kwamba wanaotafutwa kwa ajili ya kuchukua nafasi hiyo sasa ni kocha wa zamani wa RealMadrid, Carlo Ancelotti na yule aliyeachia ngazi Borussia Dortmund na kwenda mapumziko, Jurgen Klopp. Anatajwa pia Frank de Boer wa Ajax, Walter Mazzarri aliyepata kuwa Inter Milan na kocha wa Timu ya Taifa ya Marekani,

Jurgen Klinsmann.

Hata hivyo, klabu inasema kwamba utafutaji wa kocha mpya unaendelea na kwamba wanarajia kufanya uamuzi na uteuzi ndani ya muda mwafaka. Liverpool wameshinda meci zao nne tu kati ya 11 kwenye mashindano yote msimu huu, ikiwa ni pamoja na kupata ushindi kwa penati dhidi ya timu ya Ligi Daraja la Pili ya Carlisle kwenye michuano ya Capital One Cup.

ADVOCAAT SUNDERLAND SASA BASI

Dick Advocaat, aachia ngazi na kurejea kwao.
Dick Advocaat, aachia ngazi na kurejea kwao.

Kocha wa Sunderland, Dick Advocaat ameamua kuachia ngazi.
“Nimefanya uamuzi wa kuondoka baada ya mechi nane tu kwa sababu nimeona kwamba ni muhimu kumoa mtu mwingine fursa ya kubadilisha mambo,” anasema Advocaat.

Mwenyekiti wa Sunderland, Ellis Short anasema kwamba ameskitishwa sana na uamzi wa Advocaat lakini anauheshimu kutokana na kocha huyo kuwa mwaminifu, ambapo anaondoka bila kudai fedha zozote, kitu ambacho si cha kawaida kwenye soka.

Mdachi huyu aliyewanusuru kushuka daraja msimu uliopita na aliyeshawishiwa sana hadi kuingia mkataba mpya wa kuwanoa Black Cats, ameshuhudia timu yake ikikosa ushindi walau mmoja kwenye ligi katika mizunguko nane.

Sunderland wanasihika mkia wakiwa na pointi tatu tu sawa na Newcastle wanaoburuza mkia. Sunderland wana uwiano wa mabao -10.

Advocaat, 68, alipewa kazi hiyo ya ukocha Machi mwaka huu wakiwa na pointi moja tu juu ya eneo la kushuka daraja, na alifanikiwa kuwavusha. Mkewe alikuwa amempa hadi mwisho wa msimu uliomalizika Mei kurudi kwao, lakini alifanikiwa kumshawishi na kuongeza mkataba wa msimu mmoja, jambo ililowafanya washabiki wa Sunderland kumchangia mama huyo maua kama zawadi ya kumruhusu mumewe abaki London.

Kocha Msaidizi, Zeljko Petrovic naye ameamua kuondoka klabuni hapo. Sunderland walikwenda sare na West Ham Jumamosi, na sasa watakuwa wakitafuta kocha wao wa sita katika miaka minne tu.

Kocha Steve Bruce alifukuzwa Novemba 2011, huku wengine waliofundisha timu hiyo baada yake wakiwa ni Martin O’Neill, Paolo di Canio, Gus Poyet na Advocaat.

Advertisement

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version