Menu
in , , , ,

Liverpool, Spurs nje Ulaya

Liverpool na Tottenham Hotspurs zimetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Europa, Liver wakitolewa kwa penati 5-4 walipocheza na Besiktas.

Spurs kwa upande wao wametolewa na Fiorentina kwenye mechi iliyomalizika kwa Spurs kufungwa 2-1 na kutolewa kwa uwiano wa mabao 3-1.

Beki wa kati Dejan Lovren wa Liverpool alitoka uwanjani akiwa na masikitiko zaidi kwa kukosa penati muhimu. Bao la Tolgay Arslan alilofunga akiwa umbali wa yadi 20 lilipeleka mechi hiyo hadi dakika za ziada.

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Demba Ba aligonga mwamba katika mechi ambayo Besiktas walikuwa wazuri zaidi ya vijana wa Brendan Rodgers na nusura wamalize mambo ndani ya dakika 90 za mchezo.

Besiktas ni timu ya tatu kuwatoa Liverpool kwa mikwaju ya penati kwenye mechi za ushindani, wengine wakiwa ni Wimbledon waliowafurusha kwenye michuano ya Kombe la Ligi 1993 na Northampton waliowashinda kwenye raundi ya tatu ya mashindano hayo hayo 2010.

Mario Balotelli alicheza kwa dakika 82, ikiwa ni mara ya kwanza kuanza mechi tangu Novemba 8, akajitahidi kuwa na nidhamu, japokuwa alilambwa kadi ya njano mapema kwa mchezo mbaya dhidi ya Veli Kavlak.

Liverpool waliwakosa wachezaji wake kadhaa walio majeruhi, wakiwamo Steven Gerrard, Jordan Henderson, Mamadou Sakho na Philippe Coutinho. Hata hivyo walitakiwa kucheza vyema zaidi, ambapo wachezaji wake, Raheem Sterling na Daniel Sturridge walikosa nafasi kadhaa.

image

Spurs kwa upande wao walipoteza mechi ya pili kati ya 11 zilizopita za Europa, na kocha wao, Mauricio Pochettino amesema vijana wake lazima warudie hali nzuri mapema kadiri iwezekanavyo wanapojiandaa kuendelea na mechi za ligi kuu.

Mabao ya Fiorentina yalitiwa kimiani na Mario Gomez baada ya makosa yaFederico Fazio na kipa Hugo Lloris hakuwa na la kufanya. Bao la pili lilifungwa na mshambuliaji wa Chelsea, aliye Italia kwa mkopo, Mohamed Salah kutokana na makosa ya Jan Vertonghen.

Mshambuliaji wa Spurs, Roberto Soldado alipoteza nafasi nzuri alipotiliwa mpira na Erik Lamela. Jumapili hii Spurs watacheza na Chelsea kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Ligi.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version