Menu
in , , ,

Liverpool, Man U safi

Arsenal wabanwa na Southampton

 

Mzunguko wa 23 wa Ligi Kuu ya England umeanza vibaya kwa Arsenal waliopoteza pointi mbili ugenini kwa Southampton.
Arsenal walibanwa tangu mwanzo walipoanza kufungwa kabla ya kusawazisha na kuongeza bao la pili ambapo hata hivyo lilisawzishwa tena na wenyeji.

Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa vijana wa Arsene Wenger pale kiungo Mathieu Flamini alipopewa kadi nyekundu na kuwapunguza nguvu.

Mabao ya Saints yalifungwa na Jose Fonte na Adam Lalana wakati ya Arsenal yaliwekwa kimiani na Santi Cazorla na Olivier Giroud.
Bado Arsenal wanaongoza ligi kwa pointi 52 wakifuatiwa na Manchester City wenye 50 na Chelsea 49 lakini timu mbili hizo zina mchezo mmoja mkononi.

Katika mechi nyingine ya kuvutia, Liverpool waliwasasambua Everton 4-0, kipigo ambacho hawajapata kupokea msimu huu.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na nahodha Steven Gerrard, Daniel Sturridge mawili na Luis Suarez.

Hiyo ilikuwa mechi muhimu na ya watani wa jadi wa Merseyside iliyopigwa katika uwanja wa Anfield.
Machungu ya Everton yaliongezeka pale mshambuliaji wao tegemeo aliye kwa mkopo kutoka Chelsea, Romelu Lukaku alipiumia enka na kutolewa nje kwa machela.

Kwa matokeo hayo Liverpool wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi 46 wakati Everton ni wa sita kwa pointi zao 42.
Katika mechi nyingine, Manchester United walipata faraja kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Cardiff kwenye mechi ambayo Juan Mata alicheza kwa mara ya kwanza na kufanya vizuri.

Kadhalika ni mechi ambayo mshambuliaji wao Robin van Persie alirejea uwanjani baada ya majeraha ya muda mrefu na alifunga bao dakika ya sita tu kabla ya Ashley Young kufunga dakika ya 59.

Manchester wanabaki nafasi ya saba wakiwa na pointi 40.
Katika mechi nyingine Norwich walikwenda suluhu na Newcastle, Swansea wakawafunga Fulham 2-0 na Crystal Palace wakawafunga Hull 1-0.

51.584743-0.125803

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version