Menu
in , ,

Lilian Thuram azungumzia ubaguzi


*Ataka wachezaji weupe waonyeshe ushirikiano

Mchezaji wa zamani wa Ufaransa, Lilian Thuram anaamini wachezaji weupe wanatakiwa kuungana na weusi kupinga ubaguzi.

Thuram aliyepata kutwaa kombe la dunia na taifa lake anaamini hapatakuwapo mafanikio ya kweli iwapo weupe hao hawataonesha mshikamano wa kweli.

Beki huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 41 anasema wanatakiwa kukemea ubaguzi pale weusi, kama Yaya Toure, wanapobaguliwa.

“Imekuwa kawaida kuwaendea wachezaji walioathiriwa na ubaguzi, lakini nahisi kwamba wale wengine ndio wanaoweza kubadili hali hii,” anasema Thuram.

Pamekuwa na mlolongo wa wachezaji weusi kubaguliwa ama na wachezaji weupe au washabiki, ambapo wiki mbili zilizopita, Toure wa Manchester City alidai kutukanwa na washabiki wa CSKA Moscow nchini Urusi.

Thuram alikuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia 1998 na pia ubingwa wa Ulaya mwaka 2000, na anasema wachezaji weusi wasiachwe wenyewe mambo ya ubaguzi yanapotokea.

Toure alipendekeza wachezaji weusi wanaweza kugomea Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, akasema ikitokea hivyo, basi mashindano hayo hayataweza kufanyika kwa ufanisi na yakifanyika halitakuwa Kombe la Dunia.

Uefa ilichukua hatua kuchunguza suala hilo na kuagiza kufungwa sehemu ya uwanja wa CSKA Moscow kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Bayern Munich Novemba 27 mwaka huu kama adhabu kwa washabiki hao.

Katika tukio jingine la Februari mwaka huu, mchezaji wa Milan, Kevin-Prince Boateng alitoka uwanjani na mchezo kuvunjika katika mechi ya kirafiki nchini Italia dhidi ya timu ndogo ya Pro Patria, baada ya baadhi ya washabiki kumzomea kibaguzi.

Thuram ambaye amekipiga Barcelona na Juventus amegundulika kuwa na ugonjwa wa moyo tangu 2008 anaamini wachezaji weupe wakija juu, Uefa na Fifa watachukua hatua kali zaidi dhidi ya wabaguzi na kumaliza tatizo hilo.

“Mimi ninizungumzia ubaguzi au Yaya Toure au Kevin-Prince Boateng kila mtu anajua tutakachozungumza.

“Lakini kesho, wachezaji weupe wa Manchester City wakisema iwapo mwenzetu atabaguliwa tena tutakataa kubaki uwanjani, ikiwa hivyo pia kwa wale waAC Milan, Inter Milan na klabu zote kubwa, basi utaona tunapata suluhu mapema,” anasema Thuram.

Hata hivyo, Rais wa Fifa, Sepp Blatter ana mtazamo tofauti, akisema kwamba wachezaji kugombea kucheza kwa sababu ya ubaguzi ni kuwapa ushindi wabaguzi, na kinachotakiwa ni kuwaadhibu na soka iendelee.

Blatter alikutana na Prince-Boateng baada ya tukio la Italia wakati msaidizi wake alikutana na Toure jijini London baada ya tukio la Moscow.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version