Menu
in , , ,

LIGI YA MABINGWA ULAYA:

 

Man City wavuka
Manchester City wamevuka hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) baada ya kuwafunga Sevilla 3-1.

Vijana wa Manuel Pellegrini walicheza kwa kasi hasa kwenye ushambuliaji wakiwa ugenini, ambapo nyota wa mchezo alikuwa Raheem Sterling.

Alifunga bao moja kutoka wkenye kona ambayo haikutarajiwa kuzaa bao, dakika nane tu tangu kuanza kwa mechi hiyo, jingine likitiwa kimiani na Fernandinho dakika tatu tu baadaye.

Sevilla walijibu kwa Benoit Tremoulinas kuchomoa moja, lakini Wilfried Bony akamalizia kazi kabla hata timu kwenda mapumziko.

City wamejihakikishia kuvuka hadi hatua ya 16 bora wakiwa bado wana mechi mbili mkononi. Ushindi huo ulikuja huku Juventus wakitoka 1-1 nyumbani kwa Borussia Monchengladbach, katika mechi nyingine ya kundi hilo.

 

 

MAN UNITED WASHINDA KWA TABU

Rooney na goli...
Rooney na goli…

 

Manchester United wamefanikiwa kupata ushindi mwembamba wa 1-0 lakini muhimu kwenye kundi lao gumu.

Nahodha wao na England, Wayne Rooney ndiye alifunga bao kwa kichwa dakika 11 kabla ya mpira kumalizika dhidi ya CSKA Moscow, lakini walibusurika kufungwa mabao mawili dakika za lala salama.

Katika mechi hiyo ya kundi D, kipa David de Gea na Chris Smalling waliokoa mabao kwenye mstari wa goli baada ya Seydou Doumbia kuonekana angefunga waziwazi.

Kwa ushindi huo, Man United wamefikisha pointi sana, wakishika nafasi ya kwanza huku PSV Eindhoven na Wolfsburg wakiwa nafasi ya pili kwa pointi sita na kufungana kila kitu, mkiani wakiwapo Moscow wenye pointi nne, hivyo lolote laweza kutokea kwa yeyote kuvuka kutegemeana na matokeo ya mechi mbili zilizosalia kwa kila timu.

Wolfsburg waliokuwa wakiongoza kundi hilo kabla ya mechi za Jumanne hii, walipigwa 2-0 ugenini kwa PSV Eindhoven. Kocha Louis van Gaal alizomewa na washabiki wa klabu yake, wakilalamikia aina duni ya ushambuliaji kwa timu ambayo haikuwa imepata bao kwa dakika 104.

 

MATOKEO MENGINE ULAYA

Real Madrid na ushindi kiduchu..

 

Katika matokeo mengine, Real Madrid waliwafunga Paris Saint-Germain (PSG) 1-0, FC Astana wakaenda suluhu na Atletico Madrid, Shakthar Donetsk wakawapiga Malmo FF 4 – 0 na Benfica wakawapiga Galatasaray 2-1.

Advertisement

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version