Rekodi zipo kwa ajili ya kuvunjwa. Huo ni msemo maarufu duniani. Msemo huo unafaa kutumika katika mafanikio ya mwendesha magari maarufu Lewis Hamilton, ambaye anaelekea kuvunja rekodi za mkali wa mashindano ya magari Michael Schumacher.
Ushindi wa Hamilton kwenye mashindano ya magari ya nchini Ureno maarufu Pourtuguse Grand Prix wikiendi iliyipita ulikuwa wa 92 tangu alipoanza kushiriki mashindano yam bio za magari. Kwa ushindi huo ina maana Hamilton amevuka nafasi moja ya bingwa wa zamani wa mbiuo za magari Michael Schumacher aliyeweka rekodi ya kushinda mara 91 kwenye mashindano hayo. Schumacher aliweka rekodi hiyo miaka 14 iliyopita, ambayo wengi walidhani hakuna mwenye uwezo wa kuvunja.
Hakuna aliyetegemea kuona bingwa mwingine ananyakua mataji 7 ya mbio za magari. Hata hivyo rekodi ya Schumacher inaelekea ukingoni, kwa sababu sasa Hamilton anayo nafasi ya kuweka rekodi mpya zaidi ambayo itamfanya afikishe mataji 7 ya mbio za magari kabla ya kufika mwaka 2021, huku akiwa na nafasi ya kuongeza taji lingine.
Ukitazama orodha ya mbio za magari, takwimu baina ya nyota hao wawili na mafanikio yao, kwanza zinaonesha namna madereva hao walivyokaribiana kimafanikio na kupata heshima kubwa duniani. Lakini zipo tofauti muhimu ambazo zinaonesha uwezo na ubora wa madereva hao.
Mbali ya hapo pa kukaribiana mataji kwenye mashindano na ushindi wao, takwimu zonaonesha kuwa hata muda wanaotumia kumaliza mashindano unakaribiana.
JE TOFAUTI ZAO ZIPOJE?
Kwanza, nafasi zao. Hamilton amepata wastani wa asilimia 50 ya ushindi zaidi ya Schumacher katika historia yake, ambayo ameipata kwa muda mfupi zaidi. Tathmini inaonesha ni dereva mwenye kasi zaidi katika kizazi cha sasa, pengine anaweza kuwa dereva mwenye kasi duniani kuwahi kutokea. Namba zao za kuanzia mashindano nazo zinafanana.
Hamilton amethibitisha kuwa imara zaidi linapofika suala la kusaka mataji yambio za magari. Ameshinda mara 56 kulinganisha na ushindi wa mara 40 aliopta Schumacher. Lakini kwa upande mwingine namba zinampa usnindi Schumacher, mara nyingi ameibuka mshindi akitoka kushika nafasi ya pili kwenye hatua za awali. Na zaidi mara mbili ameibuka bingwa baada ya kushika nafasi ya tatu katika hatua za awali.
Mwanzoni ilisemekana Michael Schumacher ni mbabe kwenye mashindano ya mbio za magari. Lakii mtu yeyote ambaye amefuatilia mwenendo wa Hamilton jinsi anavyoshinda mbio hizo ni wazi anamzidi Schumacher kwa mbali mno.
Kiukweli, hizi takwimu ni ushahidi unaotokana na mashindano waliyoshiriki sehemu mbalimbali duniani. Wakati Schumacher akiwa kwenye mbio hizo, alikuta timu ya Forumula 1 ikitamba. Lilikuwa jambo la kawaida kusikia timu ya Formula 1 ikitamba kwenye mbio za magari, kwani ndio walikuwa vinara kipindi hicho. Michael Schumacher aliingia kwenye mbio za magari akiwa na timu ya Benetton, kisha akajiunga na timu ya Ferrari ambayo ilikuwa bingwa wa mabingwa, ambao walishindikanika kwenye mashindano hayo. Haikuwa rahisi kuwashinda Ferrari kwenye mashindano hayo.
Kuanzia mwaka 2003 hadi miaka minne baada ya mafanikio makubwa akiwa Ferrari, magari yalifuzu kwenye mashindano kwa kuanzia kuongoza hatua za awali, ikiwa na maana wakati wote ilikuwa faida kwa magari hayo kuanza mstari wa mbele. Ushindi mzuri wa magari unaweza kupatikana kwa kuanzia kasi kubwa mwanzoni ili kupata nafasi ya kubadilisha matairi kwa wakati ili kuendelea na mashindano na kulinda nafasi ya ushindi.
Katika njiangumu zote, takwimu zinaonesha bayana, ujumbe uko wazi kuwa katika mbio za magari duniani Lewis Hamilton na Michael Schumacher ni madereva wa kiwango cha juu kuwahi kutokea katika mashindano hayo. Yawezekana hawa ndiyo madereva bora zaidi kuwani kutokea duniani.
MASHINDANO
Kwa ujumla tangu wlaipoanza kushiriki mashindano, orodha ya ushindi wao kwenye mashindano ya viwango vya juu yanaonesha kuwa wao ni madereva maalumu wlaiokuja kutikisa kwenye mbio za magari.
Kwanza, hatua ya Hamilton kushinda kufanya vizuri kwenye mashindano yam bio za magari jijini Monaco yalizua mjadala na kumpa nafasi ya kujirekebisha zaidi. vivyo hivyo kwa Michael Schumacher kushindwa kufanya vizuri katika mashindano ya mbio za magari za Silverstone, kwa mtu ambaye alikuwa imara na hodari wa mbio hizo kushindwa mbele ya Suzuka na Spa, pengine ndiyo chachu ya kufanikiwa zaidi. Inawezekana ni mashindano yaliyompa somo la kuongeza spidi na mwelekeo mpya kimashindano.
Lakini ni maeneo mawili ambayo madereva wote wawili wameweka rekodi ya mafanikio zaidi kwenye mashindano ya mbio za magari.
Siku zote Hamilton alizunguka, na hilo kuwa sababu ya mkusanyiko wa nafasi za ubingwa, spidi,uwezo wa kukata kona na ufundi wa hali ya juu, ambapo ni wachache sana wanaweza kufikiwa kiwango na uwezo alionao dereva huyo.
Wote Schumacher na Hamilton wameshinda mataji 7 ya mbio za magari nchini Canada. Huo ni ushindi ambao unawapa manufaa na kuweka rekodi duniani, kutimiza wajibu,kuboresha viwango,mbinu za kuendesha,ufundi na kuwashinda wapinzani wao kwenye kona mbalimbali. Hizo ni tabia ambazo zinawafanya Michael Schumacher na Hamilton kuwashinda wapinzani wao na kuonesha kwa uwazi kupitia takwimu zao za ushindi kwenye mashindano yam bio za magari maeneo mbalimbali.