Menu
in

Lewis Hamilton: Jasiri tangu utoto

Lewis Hamilton

Lewis Hamilton

Ushujaa wa Lewis Hamilton kwenye mbio za langalanga haukuanza leo wala jana, bali tangu akiwa mtoto, alipoapia mbingu kwamba siku moja ataendesha kwa mafanikio magari hayo kwenye mashindano.

Tangu akiwa na umri wa miaka 10 tu alisema na sasa amewaonesha Watoto wote kwamba haijalishi asili au changamoto, kinachotakiwa ni kujielekeza kuhakikisha wanatimiza ndoto zao.

Haiwezekani kuwalinganisha madereva katika zama tofauti za mbio za langalanga na ukweli ni kwamba wanaweza tu kuhukumiwa kwa nyakati zao husika. Lakini ninachoweza kusema bila kupepesa macho ni kwamba juu ya Hamilton sasa wakati huu akiwa amepata ubingwa wa saba wa dunia ni kwamba, kwa maili milioni moja, ndiye dereva bora zaidi wa kizazi chake na unaweza kutetea hoja kwamba atabaki kuwa ndiye bora kabisa kwenye Formular One wa wakati wote. 

Hadi sasa, aliye mkali zaidi alikuwa Juan Manuel Fangio kwa sababu nilipokuwa mtoto enzi za Fangio alishinda ubingwa huo mara tano wakati madereva wengine walikuwa wakiuawa na magari yao barabarani, tena yeye akatwaa ubingwa akiwa na wazalishaji wanne tofauti wa magari hayo ya mbio za langalanga. Hiyo ilikuwa rekodi ya aina yake na hakuna aliyedhani kwamba ingekuja kuvunjwa.

Baada ya hapo akaja Michael Schumacher akatwaa ubingwa mara saba katika mserereko ulioonekana kwamba si halisia. Sasa kuna Hamilton ambaye si tu anafungana na Schumacher bali pia ana kila nafasi ya kumpita na kuwa dereva aliyefanikiwa zaidi kwenye F1. Naona urahisi wa yeye kutwaa ubingwa wa nane na wa tisa kutokana na kipaji na utaalamu wake kwenye ufanisi ambao Mercedes wameonesha kwenye uhandisi.

Hakuna aliyedhani kwamba Hamilton angefika mbali hivyo lakini sifa zilizomleta kwenye ngazi za juu kiasi hiki zimekuwa wazi tangu akiwa mdogo. Nilianza kumtambua wakati wa tuzo za Autosport 1995. 

Ni wakati huo, akiwa mtoto alikwenda kwa Mkuu wa McLaren, Ron Denis na kusema: “Nataka kuandesha magari yenu siku moja.” Hapa palikuwapo mtoto aliyekuwa na ujasiri wa kumwndea Ron aliyekuwa akiogopwa huku Hamilton akiwa na umri wa miaka 10 tu alionesha ni tofauti sana na wengine.

Yote yaliyofuata baada ya hapo yameonesha wazi kufuata matakwa hayo na dhamira yake, akiunganisha na kipaji chake cha asili ambacho alichofanya ni kukinoa tu zaidi kwa miaka kadhaa.

Alipoanza F1 alionesha uwezo mkubwa na msimu wa kwanza tu watu hawawezi kusahau. Mie ni shabiki mkubwa wa Fernando Alonso ambapo alikwenda McLaren 2007 akiwa bingwa mara mbili wa dunia, lakini Hamilton alipoingia nyota yake ilionesha mng’ao mara. Kwa wengi, kumkuta Alonso kungewaogofya wala asingeshindana naye lakini haikuwa hivyo kwa Hamilton.

Huyu alichuana na mkubwa wake, badala ya kumwogopa, akamfanya kama lengo ili apae juu yake. Baadaye akaondoka akaenda Mercedes nayo ilikuwa 2013. Ulikuwa uamuzi wa kijasiri pia maana ilikuwa hatari kuhama vile. Ana ubingwa mara sit ana Mercedes hivyo ni wazi ulikuwa uamuzi sahihi.

Ametawala sana sasa mbio za langalanga, akishinda tena na tena na sasa amekuwa mtu wa kupigiwa mfano, ambapo awali mbio za magari zilikuwa zinachukuliwa kwamba ni mchezo wa Wazungu, mwenyewe akaja kuvunja hilo na kuzama ndani akitoka Stevenage kwenye jumuiya watu weusi. Ukiwa na ndoto na kujiamini binafsi, mambo yanakwenda tu.  

Wakati madereva wengine huonekana kuwa na wasiwasi, kiakili na hata kimwili huweza kuwa na matatizo lakini Hamilton siku zote akitoka kwenye gari yake huonekana akiwa ametulia kwa kujiamini kama anavyolikimbiza gari lake ambako pia hukaa mkao mzuri bila kuhaha.

Anajua kudhibiti mambo na ndiyo sababu amekuwa tofauti na wengine, akikaa juu sana sasa kimafanikio na anasonga mbele kifua juu, mwaka mmoja baada ya mwingine, na si tu kuwapita madereva wengine mara moja. Ni ngumu kuwa na mafanikio endelevu kama yeye, lakini kwa ushupavu wake amefanikisha.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version