Menu
in , ,

Kwanini Simba wataifunga Ah Ahli Tripoli?

Tanzania Sports

Leo majira ya Saa kumi, Simba SC itacheza mchezo wake wa marudiano na Al Ahli Tripoli kwenye uwanja wa Benjamin William Mkapa. Mechi ya kwanza iliyochezwa Tripoli iliisha kwa suluhu. Zifuatazo ni sababu tano kwanini Simba SC wataifunga Al Ahli Tripoli ya Libya.

KWA MKAPA HATOKI MTU

Hii ni kauli ya kutisha ni kauli yenye ukatili mwingi ndani yake. Kauli hii ilijengwa na Simba Sc kwenye michuano hii ya kimataifa.  Simba Sc ilihakikisha kuwa uwanja wa Benjamini Mkapa ni ngome ngumu kwa mpinzani kutoboa.

Chini ya kauli hii tumeshuhudia timu kubwa kama As Vita, Al Ahly, Wydad Casablanca ya Morocco na vigongo wengi kupigwa kwenye dimba la Benjamini William Mkapa.

Silaha kubwa ambayo Simba SC hujivunia nayo kwenye dimba hili ni mashabiki wao. Mashabiki wa Simba SC wamekuwa wakiwapa nguvu wachezaji wao.

Nguvu ambayo imekuwa ndiyo chanzo cha wapinzani wao kutotoka salama kwa Mkapa. Leo hii pia  Al Ahli Tripoli wapo kwa Kwa Mkapa, wanakutana na mashabiki wa Simba SC, mashabiki ambao wanaamini si rahisi mtu kutoka salama kwa Mkapa.

MATOKEO YA YANGA JANA.

Jana Yanga walifanikiwa kuingia hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika kwa kuifunga CBE ya Ethiopia. Matokeo haya yanawapa chachu kubwa sana Simba Sc kwao wao kufanya vyema kwenye mchezo wa leo.

Kwanini nasema hivo ? Simba SC na Yanga SC wamekuwa watani wakubwa sana wa jadi. Utani ambao unaongeza chachu kwenye ushindani. Kama Simba SC itafanya vibaya leo itakaribisha fedheha kubwa kwao, fedheha ambayo hawaitamani ndiyo maana watakuwa na nguvu ya kupambana kuepukana na fedheha hiyo.

KIKOSI CHENYE NJAA.

Msimu huu Simba SC imesajili wachezaji wengi ambao ni vijana. Vijana ambao wanaonekana wana njaa ya mafanikio kwa kiasi kikubwa. Simba SC ishafanya vyema kwenye michuano ya kimataifa ikiwa na wachezaji wengine.

Wachezaji hawa wapya wanaona kwao ni nafasi ya kuandika kurasa mpya ya mafanikio kwa kufanya vyema na wao kwenye michuano ya kimataifa. Msukumo huu wa njaa ya mafanikio unanipa kuamini kuwa ni sababu kubwa kwao wao kufanya vyema kwenye mechi ya leo.

Upi mtazamo wako ? Simba SC watafanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho ?

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya martinkiyumbi@gmail.com

Leave a Reply

Exit mobile version