1. Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika kikao chake kilichofanyika tarehe 03-04 Oktoba 2012 ilijadili michakato ya chaguzi za vyama vya mpira wa miguu vya Mikoa ya Rukwa (RUREFA), Arusha (ARFA), Shinyanga (SHIREFA), Pwani (COREFA), Dar es Salaam (DRFA) na Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT). Kamati iliamua yafuatayo: (a) Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Arusha (ARFA) (b) Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) (c) Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) (d) Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) Kutokana na udanganyifu uliofanyika katika uteuzi wa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA, Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 26(2) na (3) na Katiba ya TFF Ibara ya 49(1), imeamua yafuatayo: (i) Imeifuta Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA. TFF itateua Kamati mpya ya Uchaguzi ya RUREFA itakayoandaa na kusimamia uchaguzi wa RUREFA. (ii)Uteuzi wa Kamati mpya ya Uchaguzi ya RUREFA utafanyika wakati muafaka baada ya TFF kukamilisha taratibu za uteuzi, na ratiba ya uchaguzi ya RUREFA itatangazwa baada ya zoezi hilo. (e) Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) (f) Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) 2. Kuzingatia Kanuni za Uchaguzi: (i) Kamati ya Uchaguzi ya TFF itaishauri Mamlaka husika ya TFF kuwachukulia hatua za kinidhamu viongozi wa Kamati za Utendaji walioko madarakani wanaoingilia michakato ya chaguzi za wanachama wa TFF na kusababisha mikanganyiko katika chaguzi ili ama wandelee kuwa madarakani kinyume na matakwa ya Katiba ya TFF Ibara ya 12(2)(a) au wapitishwe kugombea uongozi kinyume na taratibu zilizowekwa na TFF. (ii)Kamati ya Uchaguzi ya TFF inasisitiza na kuzitaka Kamati za Uchaguzi za vyama wanachama wa TFF kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF wakati wote wa michakato ya uchaguzi wa viongozi wa vyama hivyo. SERENGETI BOYS KUVUNJA KAMBI KWA MECHI Mechi hiyo itachezwa kesho (Oktoba 6 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni. Kiingilio kwenye mechi hiyo kitakuwa sh. 2,000 tu. TAFCA YAONGEZA MUDA WA KUCHUKUA FOMU Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan Mambosasa, jana ndiyo ilikuwa mwisho wa kuchukua fomu lakini mwitikio wa wagombea umekuwa mdogo ambapo ni watano tu waliojitokeza. Hivyo, amesema wameongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu ambapo mwisho itakuwa ni Oktoba 9 mwaka huu saa 10 kamili alasiri. Fomu zinapatikana ofisi za TAFCA ambazo ziko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, Mhazini na wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji. Boniface Wambura |