Menu
in , ,

Kutoka TBF…

KOMBE LA TAIFA (TAIFA CUP) NA UJIO WA WALIMU WA KIKAPU TOKA MAREKANI

 

1.        Kombe la Taifa (Taifa Cup 2012) kufanyika Tanga

Nachukua fursa hii kukutaarifu kuwa mashindano ya  kombe la Taifa (Taifa Cup) mwaka huu yatafanyika Tanga tarehe 29 /10/2012 hadi 4/11, 2012.

Mashindano haya ya Kombe la Taifa kwa kawaida ndio hutumika kuchagua timu zetu za Taifa, hvyo ni muhimu kwa mikoa yote kushiriki ili kuwapa nafasi wanamichezo kutoka mikoa yao kuonekana katika ngazi ya Taifa.

Mikoa iliyothibitisha hadi sasa ni Iringa, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Singida, Mara, Dodoma, Pemba, Unguja, Tanga, Mtwara, Lindi na Dar Es Salaam.
Bado nafasi ya kuthibitisha kushiriki ipo kwa wanaopenda kushiriki katika mashindano haya na ratiba ya mashindano itapangwa tarehe 28/10/2012 katika kikao ambacho wawakilishi wa mikoa yote lazima wawepo na ndo itakuwa mwisho wa kuthibitisha kushiriki.

 

2.        Walimu wa Taifa wa Mpira wa Kikapu toka Marekani:

Awali tulitangaza kuhusu ujio wa Makocha wa kikapu toka Marekani kuja kufundisha timu yetu ya Taifa, ambao ni Albert Sokaitis (Kocha Mkuu) ambaye ni Kocha mwenye uzoefu wa miaka 24 kwa sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya Chuo Kikuu cha Post huko huko Marekani katika jimbo la Connecticut. Pia amewahi kufundisha timu na kuendesha mafunzo nchi za Uchina, Lebanon, Ugiriki na Japan.

Ambaye  atasaidiwa na Kocha Jocquis L. Sconiers ambaye nae ana uzoefu wa miaka mingi na kwa sasa ni Kocha Mkuu Msaidizi wa timu ya Chuo Kikuu cha Post huko Marekani katika jimbo la Connecticut.

Walimu wote hawa wana shahada za juu kutoka vyuo vikuu  mbali mbali vya Marekani.
Katika utekelezaji wa mpango huo katika awamu ya kwanza Kocha Sconiers anatarajiwa kuwasili nchini  tarehe 30/10/2012 na ataelekea Tanga siku inayofuata katika Mashindano ya Kombe la Taifa ili kuchagua wachezaji watakaonda timu za Taifa (wanawake na wanaume) na baada ya hapo ataanza mafunzo rasmi kwa timu zote 2 tarehe 5/11/2012.
Awamu hii ya kwanza ya mpango wa mafunzo unadhaminiwa na watu wa Marekani kupitia ubalozi wao hapa Tanzania, tunawashukuru sana watu wa Marekani.

 

3.        Mashindano ya Kanda ya tano ya FIBA Afrika

Kama mipango yote ikienda vizuri tunatarajia Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano ya kanda ya 5 ya FIBA. Mashindano haya yanayotarajiwa kufanyika hapa Dar Es Salaam kuanzia 15 hadi 22 Desemba, 2012.

Hivyo basi Kocha huyo atatumia nafasi hii kuanza maandalizi ya timu zetu za Taifa kuziandaa kwa mashindano haya yanayotarajiwa kushirikisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Misri Sudan na Sudani ya kusini.

 

4.        Mkutano Mkuu wa TBF

Tunatarajia pia kufanya Mkutano mkuu wa TBF na wa bodi kwa mujibu wa katiba siku ya tarehe 1 hadi 2 Novemba, 2012. Viongozi wote wa Mikoa na wawakilishi wachezaji,  vyama shiriki wanaombwa kushiriki bila kukosa katika mkutano huu utakaofanyika Tanga.

Tunaomba wadau wote mtuunge mkono kwa hali na mali kufanikisha malengo yetu ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu kwa faida ya vijana wetu na Taifa letu.

 

Mungu Ibariki Tanzania

 

PHARES MAGESA

MAKAMU WA RAIS-TBF

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version