Menu
in , , , ,

Kutoka kuwa Staa wa Chelsea hadi mwanajeshi

Tanzania Sports

KATIKA Ligi Kuu Tanzania inafahamika kuwa wapo wachezaji ambao ni waajiriwa na majeshi. Lakini pia wapo wachezaji ambao walikuwa raia wa kawaida na wakajiunga na majeshi. Shizya Kichuwa ni miongoni mwa nyota wa Tanzania waliojiunga na jeshi. Winga huyo wa zamani wa Simba anafahamika kama mchezaji mahiri sana lakini maisha yake kwenye kandanda yalibadilika na kujiunga na jeshi. Wakati maelfu ya watanzania wamezoea kuona wachezaji hao wakijiunga na majeshi, barani Ulaya habari inayonguruma kwa sasa ni staa wa zamani wa Chelsea aliyeamua kujiunga na jeshi na kupatiwa mafunzo huko misitu ya Amazon. Akiwa nguzo ya ushindi katika klabu ya Chelsea, nyota amegeukia taaluma nyingine ambayo imezidisha kuwa maarufu huku maelfu ya mashabiki duniani wakiwa na shauku ya kutaka kufahamu nini hasa kilichotokea katika maisha yake hadi kujiunga na jeshi. 

Je ni nani huyu staa wa Chelsea?

Tanzania Sports

Florent Malouda ni nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea, na wengi wanafahamu namna alivyokuwa winga machachari katika kikosi cha Jose Murinho pamoja na makocha wengine. Malouda alikuwa miongoni mwa nyota wa Chelsea waliounda kikosi kikali sambamba na akina Didier Drogba, Frank Lampard, John Terry, John Obi Mikel, Alex, na wengineo. Jina lake limekuwa gumzo zaidi kwa sasa kutokana na uamuzi wake wa kujiunga na jeshi, huku wengi wa mashabiki wakibakiwa na kumbukumbu za umahiri wake alipokuwa kwenye dimba la Stamford Bridge. Florent Malouda amekamilisha mafunzo yake jeshini katika nchi yake ya kuzaliwa ya Guyana (Guiana) ambayo ni sehemu ya Ufaransa, na amekuwa mchezaji ambaye anatumika kama mfano wa kuigwa wa kizazi kingine. Akiwa na umri wa miaka 44 sasa, nyota huyo wakati akiwa mchezaji wa kandanda alitwaa mataji sita, lakini katika msimu wake wa mwisho pale Chelsea alilazimishwa kucheza kwenye kikosi cha vijana cha timu hiyo baada ya kushinikiza kuhama klabu hapo pamoja na kukataa of azote zilizopelekwa kwake kwa sababu ya kuwa na malipo madogo ya fedha.

Kwanini Malouda aliamua kujiunga na jeshi?

Katika miaka ya hivi karibuni Malouda amekuwa akitambuliwa mtu muhimu katika mchezo wa kandanda ambapo amekuwa akifundisha katika vituo vya mpira wa miguu huko Kazakhstan. Hata hivyo uamuzi w akujiunga na jeshi umeongeza umaarufu wake kutokana na kuwa mchezaji mkubwa mwenye mafanikio tangu mwanozni mwa miaka 2000 na mapema mwaka 2010. Malouda amekuwa akiitwa Chui huko Dubai. Katika utaratibu wa jeshi, Malouda amekuwa kikosi cha tatu ambacho ni mahsusi kwa wananchi ambao wanapokea mafunzo ya kijeshi kama askari wa akiba. Mafunzo hayo yanaendeshwa msituni, ambako wanasafiri umbali mrefu kwenda maeneo mbalimbali, kuvuka mito na mabonde, kutengeneza mahema,kukimbia, na kuishi msituni kwa malengo ya kupata mafunzo ya utayari wa kuwa askari wa akiba pamoja na askari vijana wanaochukuliwa kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi. Kwa mujibu wa sheria za Ufaransa, askari wa akiba ni mpango ambao unawaruhusu wananchi kujiunga na jeshi kwa hiari yao ili kutoa mchango na kuhamasisha maadili na misheni za taasisi za kijeshi bila kuwa wanajeshi kamili ambao wanaweza kupelekwa vitani. 

Malouda amesema nini?

Malouda akiwa Chelsea

Akizungumzia kuhusu kuhitimu mafunzo hayo, Florent Malouda alisema “asanteni sana kwa fursa hii na heshima niliyopewa na timu nzima ya mafunzo. Huu ni msingi wa maadili wa kiwango cha juu katika michezo,” aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

Nyota huyo kwa kuhitimu mafunzo hayo ametunukiwa medali ya utumishi jeshini. Guiana ni si mwanachama wa FIFA kwahiyo Malouda alishindwa kuiwakilisha kwenye mashindano ya Kimataifa ndiyo maana aliichezea timu ya Taifa ya Ufaransa. Akiwa timu ya taifa ya Ufaransa alicheza mechi 80 katika kipindi chake cha usakati kandanda. Mwaka 2017 miaka mitano tangu alipocheza mchezo wa kwanza timu ya Taifa alifanya jaribio la kutaka kuicheza timu ya Taifa ya Guiana lakini alinyimwa nafasi hiyo. Guiana walimpanga katika kikosi chao akiwa kama nahodha kwenye mashindano ya CONCACAF dhidi ya Honduras ambapo mchezo huo ulimalizika kwa kutoka suluhu. Hata hivyo matokeo ya mchezo huo yalifutwa kwa sababu ya ushiriki wa Florent Malouda. Miaka nane baadaye Malouda alikidhi vigezo vya kujiunga na jeshi la Guiana.

Akiwa kwenye uzi wa klabu

Malouda akiwa mchezaji wa ngazi ya klabu alifanikiwa kucheza michezo 706, alifunga mabao 119 katika kipindi cha uchezaji wake kwenye ligi za Ufaransa, England, Uturuki, India, Misri, na Luxembourg. Katika kikosi cha Chelsea alifunga mabao 29 kwa misimu miwili kuanzia 2009 hadi 2011.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version