Menu
in ,

KUNA WACHEZAJI WANA MAJERAHA-GAMONDI

Tanzania Sports

Leo kocha mkuu wa Young Africans,  Miguel Gamondi alikuwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya watani na wapinzani wao wakubwa Simba SC. Tanzania Sports ilikuwa moja ya vyombo vya habari vilivyofika katika mkutano huo na kwenye mkutano huo Miguel Gamondi alionesha kufurahia kurudi kwa ligi kuu.

Miguel Gamondi alidai kuwa ni jambo zuri tumerudi kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara baada ya ratiba ya FIFA. Ni ngumu sana kuiandaa timu kipindi kama hiki kwa sababu kuna wachezaji wamekuja kambini jana na kuna wengine wanakuja leo kutoka kwenye timu zao za Taifa.

Pia Miguel Gamondi alibainisha kuwa hakuna kitu kipya cha kuiandaa timu yake. Maandalizi yatakuwa yale yale hata kama mechi inahusisha timu kubwa mbili hapa Tanzania na akabainisha kuwa anaiheshimu Simba SC kwa sababu ina wachezaji wakubwa na kocha mzuri.

Miguel Gamondi alipoulizwa kuhusu jeraha la Ibrahim Bacca hakudhibitisha moja kwa moja kama kweli beki huyo ni majeruhi ila Miguel Gamondi aliongeza kuwa kwenye kikosi chake kuna baadhi ya wachezaji wana majeraha.

Alipoulizwa kama ni rahisi kwake yeye kucheza na Simba SC. Miguel Gamondi amedai kuwa hakuna mechi rahisi kwenye ligi kuu Tanzania bara. Kila timu hujiandaa kimbinu, wengine hujilinda, wengine hushambulia na ni kuwakosea heshima kusema kuwa ni mchezo mwepesi kucheza nao.

Mwishoni mwa mkutano wake na waandishi wa habari, Miguel Gamondi alisisitiza kuwa kuna wachezaji wake muhimu ambao wana majeraha na aligoma kuwataja mbele ya waandishi wa habari. Pia Miguel Gamondi alidai kuwa mechi za kuzufu Afcon zinaathiri maandalizi na hataki kutumia kama kisingizio lakini anaamini wachezaji wake watapigana.

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya martinkiyumbi@gmail.com

Leave a Reply

Exit mobile version