Mwaka 1914 mpaka mwaka 1918 kulikuwa na vitu kuu ya kwanza ya dunia.
Vita ambayo ilikuwa kubwa na ndiyo vita ambayo ilifanyika kumaliza vita zote.
Pande mbili ambayo zilikuwa zinapigana zilikuwa pande ambazo ni imara
sana kwa sababu upande wa kwanza ulikuwa unaitwa “Triple Entente”
uliokuwa na nchi kama Urusi, Ufaransa na Uingereza.
Wakati upande wa pili ulikuwa unaitwa “Triple Alliance” ambao ulikuwa
na nchi kama Ujerumani, Austria-Hungary na Italy.
Kila upande ulitaka kuonesha ni imara kuzidi upande mwingine.
Mbinu mbalimbali zilitumika kila upande ili kushinda hii vita ila
mwisho wa siku mpira wa miguu ukawakutanisha maadui wakubwa vita hii.
Uingereza na Ujerumani waliamua kuweka silaha chini na kucheza mpira
wa miguu kwa amani.
Ikawa ishara kubwa kuwa mpira wa miguu unaweza ukatumika kuwakutanisha
maadui sehemu moja na wakafurahia.
Kuanzia hapo ukawa utamaduni wa ligi ya England kutokuwa na
mapumziko kipindi cha majira ya baridi ukaanza.
Timu zikaanza kuwa na ratiba ndefu kipindi hiki cha majira ya baridi
kuanzia mwezi wa kumi na mbili mpaka mwezi wa kwanza.
Idadi za mechi zikawa nyingi sana, timu inaweza ikacheza mechi nane
mpaka tisa ndani ya wiki nne.
Ni kitu cha kawaida sana katika ligi kuu ya England kwa sababu ya
utamaduni wao ulioanza kipindi cha vita ya kwanza ya dunia.
Utamaduni ambao ulibebwa na sababu ya pili inayofanya ligi hii isiwe
na mapumziko, nayo ni sababu ya kibiashara baada ya mabadiliko ya
mwaka 1992 katika ligi.
Wawekezaji wengi walikuja kuwekeza katika ligi kuu ya England.
Vituo mbalimbali vya habari vinavyorusha matangazo vikatumia kama
faida kubwa ya kibiashara, kwa sababu kipindi hiki ligi mbalimbali
ulaya huwa zinasimama hivo kusimama kwa ligi hizo kunaipa nafasi kubwa
ligi ya England kufuatiliwa kwa ukubwa dunia nzima.
Vituo vya habari vinavyorusha matangazo moja kwa moja hunufaika
kibiashara, vilabu navyo hunufaika na mgawanyo mzuri wa haki ya
matangazo.
Ndiyo maana vilabu vya ligi kuu ya England hupata mgawanyo mzuri wa
haki ya matangazo kuzidi vilabu vya ligi yoyote.
Pamoja na kwamba vilabu huingiza pesa lakini malalamiko mengi kutoka
kwa makocha huzidi kipindi hiki cha majira ya baridi.
Timu zao hucheza michezo mingi bila kupumzika hali ambayo huatarisha
afya za wachezaji.
Ndicho kipindi ambacho wachezaji wengi hupata majeraha, majeraha
ambayo huleta athari kwenye mwenendo wa timu husika kwenye ligi.
Ndiyo maana huwezi shangaa kocha kama Pep Guardiola akilalamika kuhusu hili.
Asilimia kubwa ya wachezaji utakaowauliza kama kuna umuhimu wa kuwa na
mapumziko kwenye kipindi cha majira ya baridi watakujibu “ndiyo”.
Kwa sababu hawapati nafasi ya kupumzika na familia zao kama wachezaji
wenzao wa ligi mbalimbali.
Inauma kuona Ronaldo ameweka picha zake katika mitandao ya kijamii
akiwa Dubai amepumzika na familia yake.
Kuna wakati mwili unatakiwa kupumzika na akili kuiruhusu ifurahie na
familia yako hasa hasa kipindi hiki cha Christmas.
Timu inaweza ikapata kiasi kikubwa cha pesa kwenye haki za matangazo
ya televisheni.
Ikatumia pesa hizo kuongeza upana wa kikosi, na wakati mwingine
ikatumia wachezaji wa timu za vijana kwenye baadhi ya mashindano,
lakini kama mchezaji hapati nafasi ya kupumzika na familia yake
kipindi cha sikukuu unamnyima kitu kikubwa katika akili yake.
Akili yake inatakiwa ipumzike, mwili wake unatakiwa upumzike pia, ili
kupata nguvu mpya ya kuendelea kupambana katika kiwango cha juu.
Ligi kuu ya Ufaransa huwa ina mapumziko ya mwezi mmoja, ligi kuu ya
Ujerumani huwa ina mapumziko ya mwezi mmoja pia, ligi kuu ya Hispania
huwa na mapumziko ya wiki mbili na Ligi kuu ya Italy huwa na mapumziko
ya wiki mbili mpaka tatu.
Na ukiangalia vilabu vinavyofanya vizuri katika mashindano ya ligi ya
mabingwa barani ulaya kwa kiasi kikubwa zinatoka kwenye ligi ambazo
zinapata nafasi kubwa ya kupumzika kwenye kipindi cha majira ya
baridi.
Miguu ya wachezaji hupata nafasi kubwa za kupumzika, na wanaporudi
miguu huwa haina uchovu ukilinganisha na miguu ya wachezaji wengi wa
timu za ligi kuu ya England.
Wakati timu za ligi nyingine za ulaya hasa hasa zile ligi tano bora
ulaya zikiwa na nyota wake muhimu ndani ya kikosi, timu nyingi za
Uingereza (United Kingdom) hupoteza nyota wake wengi kutokana na majeraha wanayoyapata
katika kipindi hiki cha majira ya joto.
Kitu ambacho hupelekea ushindani wao hupungua katika michuano ya klabu
bingwa ulaya.
Lakini hili halionekani kama jambo kubwa England.
Kwao wao kikubwa ni kudumisha utamaduni wao ulioanza kipindi cha vita
kuu ya kwanza ya dunia kuliko kutunza afya ya miili ya wachezaji.
Kwao biashara ni kila kitu kuliko kitu chochote, ndiyo maana
wataifanya ligi yao iangaliwe na ipendwe dunia nzima kwa kutompa
nafasi mtazamaji kuwa na likizo ya kuangalia mpira.
Kwao mpira ni ulevi, na wengi wameufanya kuwa sehemu ya burudani kwao,
sehemu ambayo unaweza kutoka na familia yako ili ukaburudike.
Ndiyo maana hawana likizo katika utoaji wa burudani hii.
Imefikia wakati mpira wa miguu wamefanya kama mpira wa kikapu au
mchezo wa Tenesi kwa sababu ya kibiashara na kudumisha utamaduni wao,
bila kusikiliza vilio vya wachezaji na makocha husika.
Ni wakati sahihi kwa ligi hii kuangalia upya ratiba katika kipindi
hiki cha majira ya baridi.
Ratiba ambayo haitoharibu utamaduni wa England na biashara ya ligi hii.
Kuna uwezekano wa kupunguza idadi ya mechi kipindi hiki ili kuwapa
nafasi wachezaji kucheza mechi chache na kuwapa nafasi ya kupumzika
vizuri.
Hii itasaidia kudumisha utamaduni wao na kuendelea kuingiza pesa kwa
sababu ligi itakuwa haisimami ingawa itakuwa na mechi chache
ukilinganisha na sasa.
Na hii utasaidia kupunguza uwezekano wa wachezaji kupata majeraha kwa
wingi kama wanavyopata sasa.
Kwa sasa timu inaweza ikacheza mechi nane ndani ya wiki nne, siyo
mbaya idadi za mechi zikapunguzwa bila kuathiri utamaduni wa Uingereza
na biashara ya ligi zao, hii italeta ahueni kubwa kwa makocha na
wachezaji.