Menu
in , , , ,

Kuelekea Mechi Ya Watani Simba Dhidi Ya Yanga

Tanzania Sports

Wakati tunaelekea katika moja kati ya mchezo ambao unavuta hisia kubwa sana za mashabiki wa soka hapa Tanzania na wenye msisimuo mkubwa zaidi Afrika Mashariki na kati, mchezo ambao unawakutanisha vigogo wa soka la Tanzania yaani Simba na Yanga Kuna baadhi ya mambo ambayo sitegemei kuyaona kabisa na naomba nikiri wazi kuwa huwa yananichukiza.

Huu ni Moja kati ya mchezo ambao unawakutanisha watanzania wengi na wageni ambao mara nyingi sio Watanzania unakuta ni wale ambao ni watalii au wametoka nchi nyingine kuja kuona ukubwa wa mechi hii na kufurahia soka la Afrika.

Nimeshiriki mechi kadhaa za Kariakoo Derby ingawa ni tukio ambalo  linavutia mashabiki wengi lakini kuna changamoto kadhaa zinazokera mashabiki wakati wa mechi hizi na Mimi nikiwa ni mmoja wao ambaye nimekutana na changamoto hizo.

Sitegemei Kuyaona Haya Simba dhidi Ya Yanga:

Foleni za nje ya uwanja ni moja ya kero kubwa kwa mashabiki wanaotaka kuingia uwanjani. Mashabiki wengi hufika uwanjani masaa kadhaa kabla ya mechi kuanza lakini pamoja na kujitahidi kwao mara nyingi hujikuta wakikumbana na foleni ndefu.

Hii inasababishwa na udhibiti wa ulinzi mkali, ukaguzi wa tiketi, na mara nyingine idadi kubwa ya watu wanaotaka kuingia kwa wakati mmoja. Hali hii huleta usumbufu mkubwa, na wakati mwingine mashabiki hufika kuchelewa kushuhudia mechi kwahiyo nadhani ni jambo ambalo wanatakiwa kujipanga nalo mapema ili kuona kwamba halijirudii kabisa katika mechi inayofuata.

Lakini pia ubora wa huduma za vyoo ndani ya uwanja wa Mkapa huwa ni kero kwani vyoo vingi huwa havina huduma bora za usafi na wakati wa mechi kubwa kama Simba na Yanga hujaa haraka kutokana na idadi kubwa ya mashabiki wanaohudhuria. Hii huleta hali ya usumbufu, na kufanya mashabiki wengi kushindwa kupata huduma za msingi kwa urahisi. Wakati mwingine vyoo hivyo huwa vichache na havikidhi mahitaji ya mashabiki waliopo uwanjani, jambo linalofanya hali kuwa mbaya zaidi.

Tabia ya watu kuchelewa kununua tiketi kabla ya siku ya mechi inasababisha vurugu nyingi siku yenyewe ya mechi. Mashabiki wengi hujikuta wakihangaika kutafuta tiketi dakika za mwisho  hali ambayo huongeza msongamano kwenye vituo vya mauzo.

Vilevile kuna wale ambao hujaribu kununua tiketi kupitia njia zisizo rasmi jambo linaloleta udanganyifu na wakati mwingine kupelekea watu kutapeliwa hili ni kwa mashabiki kuhakikisha kuwa wanakua na tiketi zao mapema kabla ya Siku ya mechi husika.

Haya yote ni mambo yanayoweza kuharibu ladha ya kushuhudia moja ya mechi kubwa zaidi barani Afrika. Ni muhimu kwa mamlaka zinazohusika, kama vile klabu za Simba na Yanga pamoja na vyombo vya usimamizi wa michezo, kuangalia jinsi ya kuboresha huduma kwa mashabiki ili kuepuka changamoto hizi. Uboreshaji wa miundombinu ya viwanja, kuimarisha udhibiti wa tiketi, na kuweka utaratibu mzuri wa ulinzi vinaweza kusaidia kuondoa kero hizi na kuboresha uzoefu wa mashabiki. 

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version