Menu
in

Kriketi Tanzania inafelishwa na viongozi

Tanzania Sports

Mchezo wa KRIKETI nchini Tanzania unachukuliwa poa sana hasa hauzungunziwi, pia hautangazwi sana hii pia inawezekana tatizo kubwa lipo kwa viongozi wa mchezo huo ambao hawana utaratibu mzuri.

Niweke wazi kuwa viongozi wa Kriketi kutokuwa wawazi pamoja na kutotoa hamasa kwa mashabiki wa Tanzaia ndio sababu kubwa ya kuzorota kwa mchezo huo.

Hata kama hatujawahoji juu ya bajeti lakini pia ni jukumu lao kuweka wazi kila mwaka juu ya maendeleo ya mchezo na kama kuna fedha imeingia wameitumiaje.

Mchezo huu unahitajika zaidi vifaa kama wanahitaji kuuendeleza pamoja na sehemu za kuchezea.

Nchi ya Afrika Kusini  iko vizuri sana kwani wanashinda medali nyingi kwanini hawasomi kupitia hapo hawa viongozi wa Kriketi na walete utaalaamu.

Australia,Dernmark na hata pale ulipoanzia England mchezo huu unafanya vizuri sana na unateka kama si kukonga hisia za mashabiki wa mchezo huo.

Kwa sasa mchezo huo unachezwa katika mikoa michache kabisa ambayo ni mitano na kama kiza tu mchezo huo huchezwa zaidi hapa Dar es Salaam kutokana na miundombinu iliyopo hapo, swali la kujiuliza wanashindwaje kuunganisha mikoa yote ?

Kuna michezo mingine hata haihitajiki nguvu, harafu unaweza ukashangaa viongozi wa chama hicho wanatoka katika Nchi zinazofanya vizuri sana ulimwenguni ambapo ni India, wana asili ya India ambaye Mwenyekiti Primji Pindoria  na makamu wake Shaheed  Mustafa Dhanani kipi kinawashinda kusogeza mbele ?

Kuna wakati unaweza ukalalamikia sana vyombo vya habari lakini umetengeneza mfumo mzuri na waandishi wa habari kupata habari kwa wakati, unatengeneza hamasa, hapa simaanishi bahasha kama wengi walivyozoea bali namna ya utoaji habari ukoje unapopigiwa simu, mikutano ya mara kwa mara ikoje.

Ukitaka kujua kama kuna kitu hapa ndani yake angalia katika uchaguzi wao, kunakuwa na vita kubwa ya uhasama, lazima hapa kuna kitu wanagombania, kama si ulaji basi kuna jambo kubwa sasa kama hivyo kwanini wasipange mipango sahihi ya kuupeleka mbele mchezo huo.

Naamini mchezo huu pia una bajeti kubwa duniani kwani umesajiliwa kisheria bajeti yake watu walishawahi kuhoji inaendaje, kwanini isifike wakati kutumia mwanya huo kutengeneza mfumo mzuri ambao utakuwa rafiki kwa watoto wadogo ambao ndio nguzo muhimu katika michezo duniani kote.

Kwa wazazi nako kuna ugumu sana kuamini katika mchezo huu, basi katika zile ratiba zenu fanyeni kila wiki kwenda na familia zenu katika viwanja vya mchezo huo ili kuwafanya watoto wenu waweze kupenda na huenda baadae wakaingia humo.

Sio watoto wote watakuwa wanasoka bali kuna michezo mingi inaweza kuwatoa kimaisha na baadae kuwasogeza maisha yao mazuri.

Huku kuna fursa kubwa kwani watu wenyewe ni wachache zaidi unawezakumpeleka mtoto wako na akapata tobo la kutusua kupitia Kriketi.

Serikali nao basi ingieni wekeni mkazo kidogo huku nako mbona kuna michezo mingine rahisi mno watu wengi kupata ajira, uzuri wa Kriketi unaweza ukacheza hata ukiwa na miaka 35 hadi 40 tofauti na michezo mingine.

Afrika ni Bara pekee ambalo lina mchezo michache kuliko yote duniani, hii inatokana na miundombinu yake ilivyo mibovu pamoja na kutotaka kubadilisha  mapenzi yao juu ya michezo mingine.

Hii iko wazi kuwa hata mtoto akianza kupata ufahamu tu wazo lake la awali anafikiria kuja kuwa Aubamayang  kuliko kuwa Hasheem Thabeet , ni mfumo tu ambao nchi nyingi za Afrika umejipangia.

Utofauti uliopo hata hizo timu zao wanazozipenda huwa wanachagua timu mbili kubwa basi mapenzi yao yana lala hapo, tofauti na Ulaya pale ulipozaliwa ndipo mapenzi yako yanalalia hapo, mfano ukiwa umezaliwa Leicester City lazima utakuwa unaipenda timu hiyo , ikumbukwe muamuzi wa kati wa England Kevin Friend yeye amezaliwa katika mji huo chama cha soka cha England ‘FA’ walipanga mchezo baina yao(Leicester City) dhidi ya Manchester United, baadae baada ya kugundua kuwa Friend ni mzaliwa wa kitongoji hiko waliamua kumuondoa na kumpangia mchezo mwingine.

Hii tabia ya kuchagua chagua michezo ipo tu Afrika, angalia Ulaya kila mchezo una wapenzi wake, mbio za magari,ukiwapeleka kwa kina Hulk Hogan au Randy Orton katika mchezo wa Mieleka unakuta mashabiki wamejazana, yaani kila sehemu wamo.

Kuna wakati hata viongozi wa michezo mingine wanaharibu sana na inawezekana ikawa sababu ya wengi kutovutika huko, zamani hapa Tanzania hakukuwa na mapenzi ya mpira wa wanawake lakini kwa sasa tayari kila mmoja anapenda kutokana na mfumo kuwekwa sawa.

Dozi hii iwafikie na michezo mingine ambayo pia inataka msukumo sana wawatu wakati viongozi wapo hawaonesha hamu na kiu ya kuupelekea mbele mchezo husika.

Inayokuja na kuja na beech soccer kwa namna ilivyochukuliwa hapo awali na kwa sasa iko wapi.

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

Leave a Reply

Exit mobile version