INAONEKANA Mashabiki wa klabu ya Simba na wadau wa soka nchini wanajiamini, na hivyo nami nasisitiza hakuna sababu ya kukosa ubingwa wa Shirikisho. Ratiba ya iliyotolewa CAF inaonesha mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania wataingia dimbani kuchuana na klabu ya Al Masry ya nchini Misri. Hii ni miongoni mwa vilabbu vinavyofanya vizuri katika Ligi Kuu ya Misri ndiyo maana ikafuzu kuwakilisha kwenye mashindano ya Afrika. TANZANIASPORTS inakuleta sababu muhimu ambazo zinawafanya washabiki, viongozi na wadau wa soka kuamini Simba wanaweza kunyakua taji hilo msimu huu wakiwa chini ya kocha asiye na maneno mengi Fadlu Davids.
Deni la Yanga
Hakuna kitu kinachowanyima raha mashabiki wa Simba kama rekodi hii ya Yanga. Yanga chini ya Nasredine Nabi ilifanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo uliukosa ubingwa huo kwa tofauti ya bao moja tu. Yanga walipoteza mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam, hivyo walitakiwa kushinda mabao 2-0 nchini Algeria. Hata hivyo ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya USM Alger hakuwapa ubingwa hali ambayo ilimfanya kocha wao kumwaga machozi. Kitendo cha Yanga kutinga fainali kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho kinawapa deni mashabiki,wachezaji, viongozi na benchi la ufundi la Simba. Ni lazima deni hili lililipwe ndipo litafutwa. Yanga kwa upande wao wanaiona Simba kama klabu inayotaka kufukuzia rekodi yao, lakini kiutani wa jadi wanatamani wana Msimbazi hao waukose ubingwa. Hata hivyo katika hali ya maendeleo ya soka letu kila mdau na shabiki wa timu yoyote anatamani kuona Simba wananyakua taji hili kufuta deni lao kwa Yanga.
Waarabu si wageni kwao
Samba wamecheza mashindano haya kwa muda mrefu pamoja na Ligi ya Mabingwa. Katika mashindano yote hayo wamekutana na timu mbalimbali kama vile Al Ahly, Zamalek, Ismailia, Arab Catractors na nyinginezo. Kwahiyo linapofika suala la mashindano ya CAF, Klabu ya Simba ina mengi ya kuwaonesha waarabu ikiwemo utemi wao kwenye mechi za nyumbani pamoja na ugenini. Simba wanao uzoefu namna timu za kiarabu zinavyocheza, mbinu zao, uimara wao na jinsi ya kuwatoa. Simba wana kila sababu ya kuwadhihirishia Waarabu kuwa wao ni walewale ambao wanatetemesha vigogo wa kiarabu kila wanaposhiriki mashindano ya CAF. Simba hawana cha kuhofia na wanatakiwa kuwa wao kama wanavyocheza kila mechi za mashindano kutafuta ushindi kwa kila hali.
Rekodi zao CAF ni safi
Zamaleki waliwahi kuonja machungu ya kufungwa na Simba. Al Ahly wamewahi kuonja machungu ya kufungwa na Simba. Hii ina maana timu za Misri zinafahamu zinakwenda kucheza na Simba tishio kwa kuanzia jina lake hadi sifa zake kwenye mashindano. Al Ahly walipigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa. Zamalek walipigwa kwenye dimba lao la nyumbani kwao kwa matuta 3-2. Katika mashindano ya CAF, klabu ya Simba ina rekodi nzuri katika mipambano yao dhidi ya timu za Misri, Tunisia, Algeria na Morocco. Kimashindano Simba wanawazidi mbali sana Al Masry kuanzia uzoefu, rekodi na uimara mashindanoni. Al Masry wamefika robo fainali kwa sababu ya uwezo wao, hilo ndilo linalowafanya waheshimiwe, lakini si kuogopwa.
Samba ni tishio
Hakuna ubishi timu mbalimbali kwenye mashindano ya CAF zinatambua shughuli pevu wanayokutana nayo kwa Simba. Baadhi ya timu zimewahi kuambulia vipigo vikali kwenye mashindano ya CAF ndiko ulikoibuka msemo “Kwa Mkapa hatoki mtu,”. Kwenye dimba la Benjamin Mkapa ni jambo la kawaida timu za kigeni kufungwa mabao matano. Kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa na sasa Kombe la Shirikisho, Simba wameweka alama yao muhimu sana ambayo inawafanya watembee kifua mbele. Simba wanaonekana kuwvautia wachezaji na makocha wengi kwani ndiko sehemu wanakoandika majina yao kwneye mashindano.
Makocha mbalimbali wamepita Simba wamefanikiwa kupata ajira nyingine kubwa. Kwahiyo klabu ya Simba nayo ni tishio, na bila shaka Al Masry wanatambua watakachokutana nacho kwneye uwnaja wa Benjamin Mkapa. Simba imecheza kwa mafanikio mara kwa mara kwenye mashindano ya Afrika na kuvutia vigogo mbalimbali ambao husajili wachezaji wao. Kwahiyo katika mchezo unaokuja kati ya Simba na Al Masry ni dhahiri waarabu wanajiandaa kukutana na kitu kizito kwenye ardhi ya Tanzania.
Vita ya ndani na nje
Timu kuwa tishio maana yake inafanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali na ndiyo maana naamini Waarabu wamejiandaa kupmbana na Simba. Ukiwatazama Simba wa sasa na Al Masry huwezi kujaribu kuamini kuwa mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania wana kila sababu ya kuwatupa nje waarabu hao. Vita ya mchezo wa robo fainali itachezwa ndani na nje ya uwanja kwa sababu ikila mmoja anahitaji kuibuka na ushindi kisha kujinyakulia fedha za za CAF. Kama vita ndani ya uwanja, Simba wanajua namna ya kukabiliana na washindani wagumu. Na kama nje ya uwanja Simba wanao uzoefu wa kutosha kwenye vita vya mpira nje ya uwanja.