Menu
in , ,

‘Kombe la Dunia halitafanyika Qatar’

Ofisa wa ngazi za juu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) amedai kwamba fainali za Kombe la Dunia 2022 hazitafanyika nchini Qatar, tofauti na ilivyopangwa.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya FIFA, Theo Zwanziger kutoka Ujerumani amedai kwamba wataalamu wa afya wameeleza hawataweza kuwajibika kwa namna yoyote iwapo michuano hiyo itafanyika katika hali ya joto kupita kiasi.

Msimu wa kiangazi jotoridi hupanda hadi zaidi ya nyuzi 40 Mashariki ya Kati, na FIFA walijikuta wakiwapa Qatar uenyeji, na sasa wanadaiwa walifanya hivyo kwa shinikizo la mlungula kutoka kwa matajiri hao wa mafuta.

“Binafsi nadhani kwamba hatimaye Kombe la Dunia 2022 halitafanyika nchini Qatar na hata madaktari wamesema hawatafanya kazi huko katika wakati wa joto kiasi hicho,” amesema kiongozi huyo anayeaminika.

Qatar wenyewe wamekuwa wakisisitiza kwamba wanaweza kuendesha mashindano hayo wakati huo kwa kutumia teknolojia ya kupooza hali ya hewa na sasa wanaendelea kujenga viwanja vya mechi na vya mazoezi pamoja na maeneo kwa ajili ya washabiki.

Hata hivyo kuna sintofahamu juu ya hatima ya kiafya kwa wachezaji na washabiki, kwa sababu ya ukali wa joto la majira ya kiangazi. Hiyo itawawia vigumu zaidi wachezaji waliokaa muda mrefu Ulaya, ambako kuna baridi karibu majira yote ya mwaka.

Katika fainali zilizopita nchini Brazil, baadhi ya timu zilifanya vibaya kwa wachezaji wake kuzidiwa na joto, licha ya kwamba halikuwa kali kiasi hicho. Moja ya timu zilizoathiriwa ni Uholanzi, ambapo Robin van Persie alifika mahali akashindwa na kutolewa nje.

“Huenda wataweza kupooza joto viwanjani lakini Kombe la Dunia ni zaidi ya viwanja, kwani halifanyiki hapo tu. Washabiki kutoka pande zote za dunia watakuwa wanasafiri kuja upande huo na katika mazingira hayo, kuna hatari ya vifo na itabidi waendesha mashitaka waanzishe uchunguzi,” akatishia Zwanziger.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version