Klabu za soka zilianzishwa kuwakilisha jamii na washabiki, sio wamiliki..
Uwapo wa wamiliki kadhaa klabu moja unavyoonesha kwamba mchezo, hasa nchini England, umepoteza lile wazo au utamaduni uliokuwapo kabla wa kwamba soka ni kwa ajili ya jamii.
Klabu ya soka ni nini? Ni moja ya maswali yale yanayoonekana kuwa rahisi lakini mara yanageuka kuwa magumu kupata majibu. Si klabu zote zipo sawa, na si kila mmoja ataichukulia klabu kwa namna ile ile lakini – na hii labda ni kwa sababu zama hizi imekuwa kawaida kwa taasisi Fulani kumiliki klabu kadhaa – pengine ni muhimu kuelezea klabu ni nini, au kipi tunachotaka iwe, kama sehemu ya kufanyia kazi uelekeo sahihi kwa soka.
Klabu za kwanza zilianzishwa katikati hadi mwishoni mwa karne ya 19 kwa ajili ya wanachama waliopenda kucheza. Kadiri muda ulivyokwenda, ikaonekana kwamba iliwapendeza watu kulipa kiingilio ili kutazama mechi; lakini hawakuwa washabiki baki au wasio na upande kama ilivyokuwa kwenye kumbi za maonesho; bali hawa walikuwa na upande, wakionesha wazi kwamba soka ni burudani.
Ilipofika mwaka 1882, wakati mamia ya washabiki waliposafiri Kwenda Kusini mwa England, kwa ajili ya kuwaunga mkono Blackburn Rovers kwenye fainali za Kombe la FA, klabu zilishageuka kuwa nembo za Fahari kwa watu wa eneo husika au jamii ile, kitu kilichothibitishwa mwaka uliofuata pale maelfu ya washabiki walipojitokeza kuwakaribisha nyumbani Blackburn Olympic, baada ya kuwa klabu ya kwanza ya Kaskazini kutwaa Kombe la FA.
Kulitokea vichocheo vikubwa kwa soka, kwani wamiliki wa viwanda na migodi walizigharamia klabu za kwenye miji ya viwanda kule Kaskazini na Kati mwa nchi, kuwatuliza washabiki, wakilenga kuboresha nyumbani kwao kupitia soka, hasa Scotland.
Nchini England mambo yakaja kuwa tofauti, klabu zikawa zikiwakilisha watu wasiozimiliki. Ikaonekana pia kwamba, walau kwa kiasi Fulani, klabu zilikuwa zikiendeshwa kwa kuziletea mema jamii za eneo husika.
Viingilio vikaja kuanza kuwa chanzo kikuu cha mapato, kwa hiyo ikawa kwamba ni muhimu kuhakikisha kuna kitu cha maana kinatokea dimbani chenye thamani ya kuvutia watu ambao wangeridhika na fedha waliyoitoa. Pili, hadi mwaka 1981 gawio liliwekwa kwa asilimia 7.5 na hakuna mkurugenzi ambaye angelipwa na klabu. Hizi klabu hazikuonekana kama taasisi za kutengeneza faida.
Uchukuliaji wa soka kuwa kwa ajili ya jamii (chukulia kwa mfano makasiriko na maandamano ya kupinga kupanda kwa viingilio wakati ule wa gharama za Maisha zilipopanda, kana kwamba klabu hazihusiani na kuanguka kwa uchumi) ilikuwa kawaida, lakini kwa sasa itakuwa kichekesho kutoifanya soka kama shughuli kubwa ya kiuchumi.
Kuongezeka kwa umuhimu wa mapato kutokana na urushwaji wa matangazo ya mechi, wakati huu, umekuwa kama mapinduzi, kwa klabu kupokwa kutoka kwa jamii zilimo. Klabu nyingi haziwezi kusonga mbele bila ya kuwa na washabiki wanaolipa viingilio, kama ilivyoshuhudiwa wakati wa janga la Covid-19, lakini pia wamiliki hawatakiwi kuchukulia kwa unyeti sana madai ya jamii za wananchi wanaozizunguka klabu, japokuwa ni sahihi kusema kwamba wana wajibu kwa washabiki wao kidunia.
Kadiri mtiririko wa fedha kupitia klabu ulivyoongezeka, pia wafanyabiashara wenye uhusiano mdogo, au wasiokuwa nao kabisa na jamii zinazozizunguka klabu walianza kujihusisha, wakipelekea Ligi Kuu ya England (EPL) ya kisasa, haki, fedha za serikali na kampuni za uwekezaji kutoka ng’ambo.
Luton inayomilikiwa na wakfu wa washabiki, unatoa wakilisho kwa wachache kabisa wa jinsi hiyo. Kwa ujumla, hata hivyo, mgawanyiko baina ya washabiki na wamiliki haukupata kuwa mkubwa kiasi hicho.
Kwa kiwango kikubwa, malengo la wamiliki na washabiki yanatakiwa kuwekwa Pamoja. Iwe wamiliki wanatafuta faida ya kifedha, ushawishi wa kisiasa au kuleta mapinduzi, mafanikio kwenye dimba kiuchezaji yatasaidia – japokuwa upo uwezekano wa wakurugenzi kuchukua gawio kubwa hata kama timu zao hazijasogelea nafasi ya kukaribia kutwaa ubingwa.
Kwa wengi, hiyo inatosha; wamiliki wazuri ni wale wanaotumia fedha, wamiliki wabaya ni wale wasiotumia katika kujenga timu, kwenye mambo kama ya usajili.
Sheikh Mansour hawekezi Manchester, wala Saudi Arabia Public Investment Fund hawawekezi Newcastle, kwa sababu ya mioyo safi – japokuwa hilo linaonesha kwamba klabu sasa ni sehemu kubwa ya jamii na kwamba uwekezaji huja na miradi.
Lakini, hivi ndivyo klabu sasa imekuwa? Kwa kuwa viwanda vya jadi vimepungua, wajibu wao kama nembo ya jamii imekuwa muhimu zaidi. Hata hivyo, klabu sasa zimekuwa njia kubwa ya kutengeneza faida, iwe ya kiuchumi au kisiasa.
Wakati klabu zinashinda, washabiki wanaweza kujizuia kwa mengine yote yanayotokea lakini si kile kinachotokea uwanjani; hatari na viosingizio huja wakati wanapofanya vibaya uwanjani.