Menu
in , ,

Kipa City yuko hatua moja tu kufungiwa

Gianluigi Donnarumma

• Kipa wa Manchester City yuko hatua moja tu kufungiwa
• Meneja anatumaini Phil Foden atamalizia maisha yake ya soka ndani ya klabu

Pep Guardiola hatamzungumzia Gianluigi Donnarumma kuhusu kupokea kadi nne za njano katika mechi 10 za Premier League kwa sababu kipa huyo wa Manchester City ana “utu uzima wa kutosha” kuelewa kuwa anahitaji kupunguza mwenendo wake uwanjani.

Tatu kati ya kadi za njano za Muitaliano huyo ni kwa malalamiko (dissent), ikiwemo ile ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Leeds Jumamosi, na nyingine kwa kupoteza muda. Iwapo ataonyeshwa kadi ya njano katika mojawapo ya mechi sita zijazo, atakuwa kipa wa kwanza kufungiwa mechi moja kutokana na kufikisha kadi tano za njano katika Premier League.

Ingawa makipa 12 wamewahi kufikisha angalau kadi tano katika msimu mmoja wa Premier League, hakuna aliyefanya hivyo mapema kiasi cha kusababisha kufungiwa – rekodi iliyopo ni kufikisha kadi tano katika mechi 19 za mwanzo.

Guardiola aliulizwa kama atazungumza na Donnarumma, usajili wao wa majira ya kiangazi akitokea Paris Saint-Germain. “Hapana, ana utu uzima wa kutosha,” alisema meneja huyo. “Kwa hakika ataelewa taratibu tabia na mienendo mipya ya ligi hii.”

Tanzania Sports
Phil Foden

Mkataba wa Phil Foden, aliyefunga mabao mawili dhidi ya Leeds ikiwemo la ushindi, unaisha majira ya kiangazi 2027, na Guardiola alisema: “Natamani akae hapa maisha yake yote. Ni mchezaji maalumu, shabiki wa Man City aliyekulia akademi yetu.”

Foden ana mabao matatu katika mechi 11 za ligi msimu huu, akiwa wa pili ndani ya klabu nyuma ya Erling Haaland aliyefunga mabao 14 katika mechi 13. Guardiola anaamini Foden anaweza kumaliza msimu akiwa na idadi ya mabao zaidi ya 15, kama alivyofanya miaka miwili iliyopita alipofikisha 19.

“Miaka ambayo tumekuwa na mafanikio, si tu washambuliaji bali hasa wingers na viungo wakabaji wa kizushi ndiyo wamekuwa wakifunga mara nyingi,” Guardiola alisema. “Tunahitaji hilo tena.”

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version