Baada ya timu ya Yanga kutangaza kuachana na aliyekuwa kocha mkuu Zlatko Krmpotić sasa waelekeza nguvu kwa kocha raia wa Burundi Cedric Kaze.
Siku tano nyuma tuliwahi kuandika juu ya kiu ya Yanga kuhitaji huduma ya Kaze kwa muda mrefu kipi kilikwamisha wawili hao kuungana yote tuliyaelezea vizuri katika makala hiyo.
Baada ya mchezo ambao Yanga walitoka na matokeo ya ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Coastal Union uwanja wa Mkapa, masaa mawili taarifa za kumfuta kazi Zlatko zilienea katika mitandao ya kijamii na kupitia ukurasa wao wa Instagram.
Wengi hawakuamini kwani takwimu za kocha huyo tangu afike licha ya kutokuwa na mchezo mzuri uwanjani lakini matokeo yanaridhisha.
Katika mechi tano ligi kuu Tanzania Bara ameshinda michezo 4 na kutoa sare mmoja hivyo kakusanya alama 13 na ameruhusu goli moja tu.
Kilichowashangaza zaidi kwanini aondolewe wakati matokeo amepata wakati watu wamezoea kuona kocha anafukuzwa kwa kukosa matokeo mazuri.
Timu ya Wananchi hawakuangalia matokeo bali wameangalia ‘Performance’ ya timu nahii ndio sababu kubwa na tutaelezea chini.
KWANINI AMEFUTWA KAZI?
Sababu namba moja ya wazi kabisa iliyomuondoa Zlatko ‘Performance’ timu haikuwa inacheza vizuri licha ya kupata matokeo.
Katika mechi tano bado haionekani ikicheza kitumu yaani kama inaungana kwa kipindi cha hivi karibuni, hivyo wameona mapema walishughulikie tatizo kabla ya nyumba kuwaka moto.
Timu ilikuwa inapiga pasi moja ya pili ipo kwa mshambuliaji, mpira haukai mbele kwakuwa mipira inayopigwa huko haifiki sehemu sahihi.
Lakini pia hata uchaguzi wa wachezaji imekuwa ngumu kwa kocha huyo kwani kuna nyota ambao inasemekana wangesaidia timu yeye anawaacha nje mfano , Haruna Niyonzima na Farid Mussa.
Sehemu ya nyuma inaonekana iko vizuri kwakuwa mabeki wote walio katika sehemu hiyo wanacheza vizuri ila kuunganishwa sasa kwa kikosi chote ndio imekuwa shida.
Sabau ya pili ni mechi ya ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya watani wao Simba ambayo itafanyika Oktoba 18 nayo imekuwa sababu kubwa kocha huyo kunyofolewa.
Viongozi wameona kabisa hakuna namna kabisa ya kutoka katika mchezo wa Okotba 18 kwa aina wanavyocheza lazima wangekula nyingi hivyo wameamua kuachana naye ili waanagalie namna wanaweza kujikomboa katika mchezo huo.
Msomaji utakuwa unajiuliza sasa kumuondoa kocha ndio kutaondoa kipigo , swali hilo mimi sijui labda Yanga wenyewe wangekuwa na jibu.
Wachezaji wenyewe hawamuelewi, kuna siri imevuja kuwa hata wachezaji wenyewe hawamuelewi kwa namna anavyofundisha wamepenyeza siri kwa viongozi.
Wazo la kurudi kwa kaze nalo likawa akilini mwao na wameshafanya mazungunzo tena juu ya yeye kuja kufundisha kikosi hiko licha ya matatizo na familia yake hayaja koma vizuri.
Ukichanganya yote haya utapata jibu la kwanini kocha huyo kutoka Serbia kafutwa kazi haraka ili mambo wayaweke sawa.
KAZE KUCHUKUA MIKOBA
Dili la kocha huyu liko wazi kabisa na wameshawasiliana tayari juu ya kuja kufundisha Yanga.
Tatizo la familia ambalo linaendelea kwa kocha huyo wamezungunza na wamefikia pazuri juu ya kuja kufanya kazi Yanga.
Familia itakaa karibu na mgonjwa huku akiwa anapata ruhusa ya kwenda kumuona mara kwa mara.
Hivyo kete inaangukia kwa kocha huyo na ndio kiu yao wana yanga kwani wakishamchukua kocha huyo watamuwekea ulinzi mkubwa kwani ndio mtu wanayetaka kwenda naye katika mabadiliko.
MAKOCHA WENGINE
Licha ya kupewa nafasi kubwaKaze bado kuna tetesi zinawaelezea makocha wengine kutokaAfrikaKusini, Misri na pembe za dunia hivyo hkama Kaze bado basi watamchukua kocha wa muda ili aifundishe timu au watamuachia Mwambusi alisukume gurudumu.
Yanga watacheza mchezo mmoja dhidi ya Polisi Tanzania kisha watacheza na Simba katika uwanja wa Mkapa ikiwa Yanga ndio wenyeji.
TUMMULIKE ZLATKO
Mserbia huyu amekaa Yanga kwa siku 37 tu na ndio chache zaidi katika timu zote alizotoka.
Japo rekodi zake hazimuoneshi kukaa hata miezi kumi katika timu moja.
Tangu afike amefanikiwa kucheza michezo 7 miwili ikiwa ya kirafiki na mitano ligi kuu Tanzania bara.
Ameshinda michezo yote ya kirafiki, ule wa kwanza katika siku ya Mwananchi Yanga ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Aigle Noir Makamba ya Burundi.
Japo alikaa katika benchi alisema kuwa majukumu yote atamuachia Mwambusi kwa kuwa yeye ndio kaanza kufanya nayo mazoezi.
Bahati nzuri timu ilishinda 2-0 hivyo tunamtoa katika zile mechi alizosimamia.
Vipi ndugu yangu unaelewa nini naenda kukieleza hapop chini , basi usichoke wewe tiririka namie utaunga tela na tutaelewana.
Baada ya hapo ligi kuu Tanzani Bara ikaanza na mchezo wa kwanza na majukumu yake mapya dhidi ya Tanzania Prisons, mfumo aliotumia hasa wa Mwambusi lakini tunaanza kumpa yeye majukumu maana alikubali zigo la mwiba.
Bahati nzuri akaambulia alama moja katika mchezo ule uliomalizika kwa goli 1-1. Goli la Yanga limefungwa na Michael Sarpong huku la Prisons limefungwa na Lambert Sabiyanka.
Tuangalie mbinu aliyotumia mchezo huo
Katika viungo aliwapanga Feisal Salum na Zawadi Mauya ambao waliutambaliza mpira chini, washambuliaji walikuwa Farid Mussa, Michael Sarpong na Ditram Nchimbi.
Mechi ya kwanza walicheza mpira kwakweli na nafikiri alitumia mbinu ile ile ya Juma Mwambusi ilimsaidia sana hasa kwa ugumu wa Tanzania Prisons.
Baada ya wiki timu hiyo ikaingia tena uwanjani kucheza na Mbeya City akabadilisha sehemu ya kiungo alimuweka Mukoko Tonombe na Feisal Salumu balaa likaanzia hapa sasa.
Mwisho kabisa hadi tiketi inamkuta hapo jana ambapo ilicheza na Coastal Union jumla ya magoli 3-0 amebadilisha mfumo kidogo akamuweka Yacouba Sogne akizungukwa na Tuisila Kisinda na Carlinhos.
Yanga hadi sasa imeshinda michezo 4 imetoa sare 1, imefunga magoli 7 imefungwa goli moja.
Ushindi wote wa alama 12 umepatikana kipindi cha pili.