“FAIR PLAY” KATIKA SOKA LETU….
Imekuwa ni kawaida sana katika soka la Tanzania kukuta klabu inafungiwa kusajili wachezaji kwa makosa yanayotokana na kushindwa kutekeleza mkataba wa mojawalpo ya wachezaji ima anayeendelea kuitumikia klabu au ambaye ameitumikia klabu hiyo huko nyuma. Hii inatokana mara nyingi na ima dharau au wachezaji hususani wa kigeni kutambua nguvu waliyonayo kupitia mikataba ambayo waliisaini.
Kanuni za uchezaji wa haki za kifedha (financial fair play) ni kanuni ambazo zinazotoa miongozo ya mapato ya klabu na matumizi yake. Kwa mujibu wa kanuni hizi kuamrishwa zisifanye matumizi makubwa kuliko kipato wanachokitengeneza na lazima vitabu vya mahesabu ya fedha vya klabu hiyo lazima viwe na uwiano na vikae sawa.chimbuko la kanuni hizi ni shirikisho la soka barani ulaya ambapo liliamua kuweka kanuni hizo ili kuhakikisha kwamba vilabu haviingizi hasara endelevu kwa miaka mingi mfululizo. Shirikisho hilo limeweka mwongozo kwamba vilabu vishiriki vinatakiwa visiwe vimeingia kwenye hasara ya Zaidi ya pesa za Euro Milioni 60 kwa miaka 3 mfululizo.
Kanuni hizo zimezibana klabu kubwa dhidi ya kutumia pesa ovyo kwani kwa sasa vilabu havitumii pesa ovyo kwenye usajili wa wachezaji bila ya kuangalia mapato ambayo wanaingia kwani mahesabu ya pesa yasipowiana basi klabu itakachokumbana ni rungu kutoka UEFA.
Mnamo mwaka 2021 shirikisho la soka duniani FIFA liliifungia klabu ya Yanga kusajili wachezaji mpaka watakapomlipa aliyekuwa mchezaji wao ambaye anatokea katika taifa la Burundi Gael Bigirimana. Hiyo ilikuwa ni baada ya kuvunja mkataba na mchezaji huyo bila ya kumlipa baadhi ya stahiki ambazo zilikuwa zinapatikana kwa mujibu wa mkataba ambao walikuwa wamekubaliana.
Tarehe 2/11/202 Klabu ya Simba ilifungiwa kusajili mpaka pale ambapo itakapoiilipa klabu ya Tengeuth ya Senegal malipo yanayohusiana na aliyewahi kuwa mchezaji wao Pape Osmane Sakho. Hiyo ilikuwa baada ya kushinda kesi ya madai dhidi ya Simba kutokana na mauzo ya mchezaji huyo kwenda kucheza katika klabu ya ligi ya Ufaransa.
Mnamo tarehe 11/12/202 Shirikisho la soka Tanzania TFF lilitoa taarifa ya kufungia kusajili klabu ya ……… mpaka itakapokamilisha malipo ya mchezaji Rodrigo Carvalho. Mchezaji huyo alifungua kesi dhidi ya klabu hiyo na kushinda.
Klabu ya Singida Fountain Gate imekuwa ni mhanga mkubwa sana wa adhabu hizo kutoka shirikisho la soka la Tanzania kwani ndani ya miezi isiyozidi imefunguliwa mashauri yasiyopungua manne na kushindwa mashauri na kupelekea kupewa adhabu ya kutosajili mpaka walipe stahiki ambazo walikuwa wanadaiwa na wachezaji ambao waliwavunjia mikataba yao. Adhabu hizo ni kama ifuatavyo:
Mnamo tarehe 7/12/2023 shirikisho la soka Tanzania TFF lilifungia klabu ya Singida Fountain Gate kusajili baada ya mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Ivory Coast Pascal Wawa kushitaki klabu hiyo.
Mnamo tarehe 11/12/2023 TFF ilitoa taarifa ya adhabu kwa klabu ya Singida Fountain Gate kutosajili mpaka itakapomlipa mchezaji wake Nicolaus Gyan ambaye alikuwa amefungua kesi dhidi ya klau hiyo katika shirikisho la soka duniani FIFA.
Mnamo tarehe 10/1/2024 klabu ya Singida Fountain Gate ilifungiwa na TFF kusajili mpaka itakapomlipa beki wa kimataifa kutoka nchini Uganda Shafiq Batambuze ambaye naye alifungua kesi dhidi yake katika shirikisho la soka la kimataifa FIFA.
Mhanga mwingine wa adhabu hizi za kutosajili ni klabu ya Taora United ama Nyuki wa Tabora kama wanavyopenda kujiita wenyewe. Klabu hii kwa mara kadhaa nayo imejikuta inaangukia katika rungu hilo la TFF ambalo huwa linatoka FIFA moja kwa moja. Walipata rungu hilo kupitia matukio yafuatayo:
Mnamo tarehe 7/1/2023 TFF ilifungia klabu ya TABORA UNITED kutosajili wachezaji mpaka itakapimlipa mchezaji wa kimataifa Evariste Mutambayi kutoka Congo
Mnamo tarehe 1/11/2023 shirikisho la soka Tanzania liliifungia klabu ya TAORA UNITED kutosajili mpaka itakapomlipa mchezaji wa kimataifa kutoka katika taifa la Congo Fabrice Ngoyi
Mnamo tarehe 1/11/2023 klabu ya TABORA UNITED ilipewa adhabu ya kutosajili mpaka watakapomlipa mchezaji wa kimataifa kutoka GHANA Asante Kwasi aliyekuwa anawadai stahiki zake na ambaye aliwafungulia shauri katika shirikisho la soka duniani FIFA
Mnamo tarehe 02/10/2023 shirikisho la soka la Tanzania TFF lilitoa adhabu ya kuwafungia kusajili wachezaji klabu ya TABORA UNITED kutokana na kuwa wanadaiwa malimbikizo ya mshahara pamoja na ada za usajili wachezaji wao wawili ambao ni Emmanuel Lamptey na Collins Gyamfi.
Kwa ujumla adhabu hizo ambazo zimezikuta vilabu hivyo zimeziathiri kwa sana kwani kwa mara nyingi zimekuwa zinapewa mda mchache kukamilisha malipo ya hao wachezaji. Siku 45 ni siku chache sana huku ukifuatilia wachezaji wengi huwa wanadai pesa nyingi sana. Na pindi wanapowalipa wachezaji hao huwa wanajikuta wanashindwa kutekeleza aadhi ya majukumu yao ya kawaida ya kiuendeshaji kwa ufanisi mkubwa kwani kunakuwa na rasilimali fedha ambazo wamezipeleka mahala sio.
Ukitaka kujua kwamba adhabu hizo zinaathiri kwa namna moja ama nyingine utaona mnamo Januari 18 mwaka 2024 klabu ya Singida Fountain Gate ilitangaza kuachana na wachezaji wa kigeni 9. Moja ya sababu ambazo uongozi ulizitaja ni kwamba wameamua kufanya hivyo kutokana na changamoto za uendeshaji wa klabu kwa hiyo wakaamua kufanya maamuzi ya kuuza wachezaji hao ili wapate fedha.
Kwa hakika usajili mkubwa wa wachezaji wa kimataifa kwa baadhi ya hivi vilabu umekuwa na fursa zake na changamoto zake. Na katika changamoto zake hawa wachezaji huwa wanalipwa hela nyingi na pindi wakivunjiwa mikataba basi wamekuwa wanaziumiza vilabu vyao kwani wao kupitia mawakala wao huwa wanawahi FIFA kwenda kufungua mashauri ambayo mara nyingi huwa hukumu zinakuwa zinabeba upande wa wachezaji hao. Mwarobaini kwa siku za usoni ni kuwa na kanuni ambazo zitadhiiti matumizi makubwa kwa hivi vilabu kuliko mapato wanayotengeneza.